Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 262
- 361
Hellow JF.
Hii inaweza kuwa mwendelezo wa makala zangu za hapa na pale japo sijazipangalia katika mtiririko sahihi kwasababu ninaishi ninachokiandika.
Nataka nikukumbushe kitu, najua wajua lakini nakujuza.
Toka kuumbwa kwa dunia kumekuwa na aina mbalimbali za watu, mfano, Watu wema (Watu wezeshi, na Watu watetezi). Kwa bahati mbaya sana watu wabaya au watu vikwazo ni wengi kuliko watu wema na mbaya zaidi watu wabaya tunaishi nao katika maisha yetu ya kila siku.
Watu hawa wabaya nao wamegawanyika katika makundi mawili kulingana na wanavyopatikana:
Mara baada ya kujua tunaishi katika dunia ambayo watu wabaya ni wengi na wengi wao ni watu waliokaribu yetu kwa sehemu kubwa sana. Ni wazi kwamba tupo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yetu, mafanikio yetu, Ndoto zetu na kadhalika. Sasa nakueleza kwamba usikubali kupoteza vitu ulivyoteseka kwa miaka mingi kuvitengeneza, usikubali kupoteza mafanikio yako, usikubali kupoteza maisha yako kizembe, usikubali kubaribiwa maisha yako kizembe. Kitu pekee na cha msingi unachopaswa kukifanya ili kujilinda na watu hao ambao wengi kama nilivyosema hapo awali ni watu waliokaribu yetu ni:
Usiishie tu kumchanganya adui maana kila chenye mwanzo huwa hakikosi mwisho. Hivyo tengeneza mazingira ambayo itakuwa vigumu adui yako kukujua meanwhile, hakikisha unaweka mikakati thabiti ya kuwabaini kwa haraka maadui zako au watu wenye nia mbaya nawe.
Pili, hakikisha unajibu mapigo kimya kimya bila kushukiwa kwa namna yoyote ile, yaani usiende kwenye umma ukasema nimekujua wewe ndo unanifanyia hivi [huo utakuwa ni upumbavu uliokomaa] wewe fanya mambo yako kimya kimya huku ukichukua tahadhari kubwa katika kila hatua unayopiga ili kumpoteza kwenye ramani adui yako.
Next time nakuletea uzi wa namna ya kumpiga adui.
Byeeee

- Watu wabaya tunaowatengeneza wenyewe (mfano, Visasi, Dhuruma, kurogana na mambo mengine mabaya tunayowatendea watu wengine).
- Watu wabaya ambao hujawatengeneza wewe (mfano, Majambazi, watu wenye kijicho na husda, Watu wenye wivu na wasiokupenda tu).
Mara baada ya kujua tunaishi katika dunia ambayo watu wabaya ni wengi na wengi wao ni watu waliokaribu yetu kwa sehemu kubwa sana. Ni wazi kwamba tupo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yetu, mafanikio yetu, Ndoto zetu na kadhalika. Sasa nakueleza kwamba usikubali kupoteza vitu ulivyoteseka kwa miaka mingi kuvitengeneza, usikubali kupoteza mafanikio yako, usikubali kupoteza maisha yako kizembe, usikubali kubaribiwa maisha yako kizembe. Kitu pekee na cha msingi unachopaswa kukifanya ili kujilinda na watu hao ambao wengi kama nilivyosema hapo awali ni watu waliokaribu yetu ni:
- KUWACHANGANYA TU
- Kuonesha udhaifu ambao sio halisia (displaying fake weaknesses) yaani mara zote lalamika kuhusu mambo ambayo unayaweza na ambayo hayawezi kukutetelesha kwa namna yoyote kwamba huo ndio udhaifu wako mkubwa.
- Epuka marafiki wanaojifanya waaminifu kwako kwa kukuelezea sana mambo yao au mambo kuhusu wao (mfano, anaekueleza kuhusu mafanikio yake na mali zake, Changamoto alizonazo za kifamilia na mambo mengine nyeti). Marafiki wa namna hii wanakuelezea habari zao ili uwaamini kwa haraka na ushawishike kutoa taarifa zako kwao, hawa kuwa nao makini muda wote na ili kutomkatisha tamaa anapokuelezea mambo yake nawe mpe ushirikiano kwa kumuelezea mambo kama yake (hakikisha husemi jambo lako hata moja la ukweli na usifanye story yako hiyo ya uongo kuwa ndefu utasahau na atajua unamdanganya, ifanye kuwa fupi na nyepesi ili iwe rahisi kukumbuka na kuitetea ili adui mwenye interest asikuelewe kwa haraka).
- Kama umeoa/kuolewa (familia), hakikisha unatengeza pattern ya maisha mnayoishi katika familia yenu. Yaani usiwe mjinga kwa kuonesha au kusema kwa watu lifestyle yenu kwa kuwa mfumo wako wa maisha unaweza kutumika kupata msingi wa wewe ni nani? Na una umahiri kwa kiasi gani katika maisha au unafanya nini au unapanga kufanya nini. Unaweza usielewe lakini ipo hivyo adui hutumia nafasi moja tu kukusambaratisha kwa hiyo, lifestyle yako ni sehemu muhimu sana ya kuikarabati ili uendelee kumchanganya adui yako.