Mchanganyiko wa Flagyl na pombe; hatari inayopuuzwa kimyakimya

Mchanganyiko wa Flagyl na pombe; hatari inayopuuzwa kimyakimya

Apotheker

New Member
Joined
Jul 8, 2025
Posts
3
Reaction score
2
Habari wakuu

Leo ni alhamisi na kwa watu wapenda viti virefu na kamnyweso wao wameshaanza wikiendi tayari, lakini tunapoelekea kwenye wikiendi hebu tujikumbushe jambo moja la muhimu hususani afya zetu.

Je, umeshawahi kusikia mtu amefariki ghafla na rafiki zake wakasema ni jana tu tulikua nae kiwanja tukinywa akaenda kwake ndo hakuamka tena ? au ushawahi kuona mtu ametoka kiwanja kupata kamnyweso ghafla ameamkia ICU ?

Ziko sababu nyingi zinaweza kuleta hayo yote lakini leo hii tuangalia sababu moja kuu inayoweza sababisha matatizo yote haya nayo ni combination ya Flagyl (Metronidazole)💊 + Pombe 🍻.Zifahamu sababu za kwanini usitumie Pombe ukiwa kwenye dozi ya Flagyl(Metronidazole ).

Athari Unazoweza Kupata ukitumia Pombe ukiwa kwenye dozi ya Flagyl

Matumizi ya Pombe ukiwa kwenye dozi ya Metronidazole husababisha hali inayofahamika kitaalamu kama "Disulfiram like reactions" ambapo hali hii husababisha mambo mbalimbali kama ifuatavyo
  • Mapigo ya moyo kwenda kasi
  • Kichefuchefu Kikali
  • Kutapika
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Presha Kushuka kupita kiasi
  • Kupoteza fahamu na kupata mshtuko wa moyo
Kwanini unapata "Disulfiram Reactions " ukichanganya Metronidazole na pombe ?
Metronidazole huzuia uvunjwaji wa pombe mwilini hivyo kusababisha accumulation ya "Acetaldehyde" kemikali inayotokana na pombe ambapo ikibaki mwilini huleta madhara mbalimbali.

Jambo la Kuzingatia ⚡
Epuka Pombe ukiwa kwenye dozi ya metronidazole hakikisha unafata maelekezo ya mtaalamu wako wa Afya

Happy Wikiend Amigos,
# Kunywa kistaarabu
 
Back
Top Bottom