Mchango Mh Joseph Mbilinyi(Sugu) toka amekuwa Mbunge kwa vijana wanao tegemea sanaa kama ajira

Mchango Mh Joseph Mbilinyi(Sugu) toka amekuwa Mbunge kwa vijana wanao tegemea sanaa kama ajira

Hivi we una akili kweli?? Akae na Ruge awaunganishe wasanii kwani Ruge ni nani ivi ujioni ulivyo mjinga.....toka lini promota akawa mtetezi wa wasanii??promota ndio awaunganishe wasanii? hivi ujui kuwa mapromota ndio sehemu ya tatizo la wasanii....wasanii wangapi wanamlalamikia uyo ruge alafu unasema eti wakae pamoja ili wafanyaje sasa? ...mtu anajaribu kurekebisha mfumo au ulitaka awagawie hela au? nani kakwambia tatizo la wasanii ni ugomvi kati yao?...tatizo la wasanii ni kipato ,watakuwaje na uhakika wa kipato ni kuubadili mfumo huu mbovu...

Ukweli ni kwamba Ruge ni muhimu kwenye hii tasnia maana ni mdau na Clouds media na Ipp media ndio vyombo vinavyo tumiwa sana na wasanii kupromote kazi zao hilo halina ubishi.
Hivi kwanini mnafikiri hao wasanii nao hawana tatizo?
 
Huyu hawezi kuwa na mchango wa maana hata siku moja hata sina haja ya kufuatilia hotuba zakeee
 
HABARI KAMA HIZI ZIMAAAAAAAAAAAAAAAA mleta mada yupo kisiasa zaidi na kaegemea upande wa wafu fm
 
Harakati zake za anti virus zimewafanya wasanii wanaojua kuimba wajitambue kuwa wanaweza bila kubebwa na media flani flani na kudhihirisha nguvu ya umma a.k.a mashabiki ndio wenye uamuzi sio media

vinega imekufa, sugu amewasaidia sana wasanii wa vinega kuvuta bangi na kuwa mateja
 
Mmekazaana ruge ruge ruge ruge....!! Hyo wafu fm ya kinafki sana hyo..! Tangu nijue nyuma ya pazia lao kuna nn! Aaah nkawa natyun 93.7, magic, ear, timez na tbc taifa. Nkazimaaaaaa wanafk fm..!! Sasa wajiandae na ujio wa Efm 2naxubr prgrms zake kwa hamuuuuu!!
 
Vilio vya wasanii wa mikoani ni vipi ambavyo viko tofauti na hawa wa dar hata afande Sele pia ni wamkoani maana maisha yake yote yako Moro na Mike t pia na Soggy Doggy pia hawa ni wasanii wa mikoani...

Suala ni je kunajipya gani Sugu hajalisemea kuhusu wasanii... je hiyo serikali yenu sikivu imewafanyia nini tangu Sugu asome hotuba ya waziri kivuli since 2011 to 2014 yapi wameyatimiza kwenye hotuba zake japo kaongea sana.

Issue ya studio mkaona bora mumpe promota Ruge wakati harakati alizianza Sugu na wasanii wasiojielewa baada kumuunga msanii mwenzao ili wamiliki studio wakamuunga yule promota ili studio aihamishie kwenye nyumba yake ya vipaji.

What do you need from Sugu wakati hao wasanii mnaosema hawasaidii wenyewe hawataki hata kumsikia akili na masikio yao yapo mawingu kwa promota wao.

Naona unarudi pale pale...kwanza nasisitiza wasanii si wa muziki pekee...na Sugu ni waziri kivuli anayepaswa kusimamia sanaa zote na ndio maana anafeli coz akili yooote kaweka kwenye muziki na kushindana na Ruge.

Na huo ndio udhaifu unaomnyima hadhi ya kuwepo pale...hiyo studio inayoimbwa kila kukicha ina gharimu shilingi ngapi ?...miaka yooote hapo kivulini ameshindwa kuhamasisha ndugu, jamaa, marafiki, wanachama au wadau wa muziki kutengeneza studio mbadala ?...kama Vicky alichangisha karibu milioni mia moja kwa ajili ya harusi, ni vipi Sugu yeye kabaki kuumiza kichwa afanye nini kupambana na Ruge.

Na tusiseme wasanii wa Dar kuwa ndio wanamajibu ya wasanii woote wa mikoani...na sio ushujaa kwa wasanii wote kuhama kwao na kuja kusongamana Dar....kwa kuwa wabunge ni wahanga wa hiyo kasumba basi isihalalishwe kuwa Dar kuna majibu ya nchi nzima....muda wote ameshindwa hata kutenga siku moja kwa mwezi kufika mkoa mmoja na kuwasikiliza, kuwashauri na kuwahamasisha wasanii ?

Nadhani Sugu, dhamana waliyompa ni kwa ajili ya nchi nzima....unless unipatie taarifa tofauti na hiyo leo hii.

What I need from Sugu ? mmmmmmh.....nadhani muda aliokwishakaa hapo ameshanidhihirishia kuwa hana uwezo wa kusaidia sanaa na wasanii kama waziri kivuli.........so, nadhani nimuache alale.
 
Mkuu FYATU, hawa wanao mtetea Sugu wanatakiwa kujua kuwa Sugu hawezi kupata ushiikiano wa wasanii kama ataendelea na Migogoro na kujihusisha na Migogoro ya makundi.

Hata hilo swala la studio lengo la Sugu lilkuwa ni kupambana na Ruge wala si kuwasaidia wasanii na ndio maana hilo swala halifatilii tena baada ya kuhakikisha ameshinda dhi ya Ruge.
 
Last edited by a moderator:
Mmekazaana ruge ruge ruge ruge....!! Hyo wafu fm ya kinafki sana hyo..! Tangu nijue nyuma ya pazia lao kuna nn! Aaah nkawa natyun 93.7, magic, ear, timez na tbc taifa. Nkazimaaaaaa wanafk fm..!! Sasa wajiandae na ujio wa Efm 2naxubr prgrms zake kwa hamuuuuu!!
Hapa swala la Msingi ni kuhakisha migogoro ina tatuliwa na hata kama Radio zitaendelea kuanzishwa lakini Clouds fm ataendelea kuwa mdau wa sanaa kama vyombo vya habari vingine.

Na hii Migogoro wala haijengi.
 
Usitake kuuthibtishia uma kuwa kabila lako limebobea kwa majungu!
 
Mkuu matumbo hatutaki mtu mwenye nia ya kuwagawa watu bali kuwaunganish.

Anacho kosea Sugu ni kutaka kuwagombanisha wasanii na wadau wa sanaa. Tunajua wadau nao wana mapungufu lakini Sugu ana anzisha umoja kwa lengo la kugombanisha watu si kujenga.

Leo hii kwenye mgogoro wa Ruge na Jide ame take side na hili ndio tatizo.

Sugu alitakiwa kuacha mambo ya Malumbano na akajaribu kukaa na Ruge wakajaribu kuwaunganisha wasanii.

Hivi kwanini tuamini kuwa wanao gombana na Ruge hawajamkosea Ruge?

Kwakweli tukiacha migogoro Sugu hana mchango kwenye tasnia ya muziki.

Nyie wahaya mbona mna ukabila sana? Kwa hiyo Ruge kwa kuwa Ni mhaya mwenzio Nshomile, hana makosa.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mleta mada ukiangalia post zake nyngi n kuisifia clouds..
Hvo najua anachohitaji..
ATAWATETEAJE WASANII WAKATI HAWAMUUNGI MKONO:??(REF::ant virus sagga)
 
Wanajamvi, Wasalaam.

Ni ukweli usiofichika kabisa wasanii na wadau wa sanaa Tanzania walikuwa na mategemeo makubwa baada ya kuona mtu ambaye alikuwa kwenye sanaa ya muziki muda mrefu amekwenda bungeni.

Wengi walitegemea Mh Joseph Mbilinyi (Sugu )angekuwa kiungo kikubwa cha wasanii na wasanii au wasanii na wadau wa sanaa hasa muziki.
Kila mtu anajua fika sanaa ya Tanzania ina matatizo mengi ambayo kwa nafasi yake angeweza kuyatatua haraka hasa hii migogoro ya wasanii kwa wasanii au wadau wa sanaa au muziki na wasanii.Lakini kinacho sikitisha zaidi yeye amekuwa akichochea mivutano hiyo kwa kujionesha yuko upande fulani kwa wakwaruzanao,wakati tulitegemea yeye ndio angekuwa msuluhishi mkuu wa hiyo migogoro hiyo jitokeza na kupata suluhu.

Tunajua fika hakuna mwanadamu aliye kamilika na hata hao anao watetea kwenye hiyo migogoro nao wana matatizo yao pia na unaweza kukuta wao ndio chanzo. Tunajua Mh Mbilinyi aliwai kuwa na migogoro na baadhi ya wadau wasanaa lakini asiwafanye wasanii wote nao wawe na migogoro nao bali alitakiwa aoneshe njia kwa kuhakisha ana waunganisha wasanii.

Pia tulitegemea kuona Mh mbilinyi angekuwa wa kwanza kuanzisha mfuko maalum wa wasanii ambao ungetumika kuwaunganisha na kuwasaidia wasanii wakati wa shida hasa wanapo patwa na misiba waache kuwa omba omba.

Hivi Mh mbilinyi hadi sasa kafanya nini kuokoa sanaa hii?Hivi atakumbukwa kwa lipi? Yani hata hili la kutatua migogoro kati ya wasanii na wadau wa sanaa limemshinda? Kwanini asiitwe waziri kimvuli mzigo?

Nilitegmea Mh Mbilinyi ange shirikiana bega kwa bega na waziri Fenela kutatua matatizo yale yanayo weza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka at least wasanii na wadau wafaidike na uwepo wake,kinyume chake ameweka siasa mbele na kuona kila mdau au waziri wana nia mbaya na sanaa, na hili analifanya ili kupandikiza chuki wakati anajua fika chuki haijengi.

Naulize tena Mh mbilinyi amefanya nini kwenye sanaa tangu awe mbunge?Bado najiuliza kwanini amekuwa akiwa katisha tamaa wadau wasanaa na kuonesha wao ni wezi na wana wanyonya wasanii. Yeye hadi leo kafanya nini?

T bnolB54YUjgAAAABJRU5ErkJggg==

Hili ndio tatizo kubwa tulilonalo waTZ, tunataka mtu fulani "atufanyie" au "atusaidie" kufanya kitu fulani bila sisi wenyewe kufanya lolote. Huyo Sugu hata afanye nini kama wasanii wenyewe hawatasimama kudai haki zao itasaidia nini? By the way alipokuwa akigombea ubunge wasanii walio wengi walimbeza na baadhi yao kukipigia debe chama tawala sasa hata ungekuwa ni wewe ungekuwa na moyo wa kuwasaidia watu hao?

Pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu, ni msanii gani aliyepinga unyonyaji kwenye tasnia ya muziki zaidi ya Sugu? Hao mnaotaka awatetee wengi ndio walikuwa upande wa wanyonyaji wakimshambulia. Kuhusu Uwaziri kivuli let's be realistic, kwa mfumo wetu wa uendeshaji wa Serikali Mawaziri kivuli hawana impact yoyote kwani Serikali haijawahi na wala haitawahi kuwasikiliza. Huwa tunawaona wakati wa Bunge wakiwasilisha altenative budgets, policies n.k. Baada ya hapo huwasikii tena mpaka Bunge linalofuata.

Mwisho hapo kwenye red naona mwenyewe umeshaonyesha mchango wake, sasa kama wadau wa sanaa ni wanyonyaji si ni lazima waambiwe? Wewe ulitaka asaidie vipi tena?
 
Sugu ni mbunge wa mbeya na sio mbunge wa viti maalum wa sanaa
 
Sugu kapigania sana muziki wa bongo kuwa hapo ulipo. Alipigania sana serikali kuwapa wasanii studio yao ikaishia mikononi mwa kina ruge kwa ushirikiano wa wasanii wenyewe. Na huwezi unganisha wasanii pamoja wakati mna itikadi tofauti, ni lazima siasa zitaingia tuu.. Kuna wasanii wao kutwa kuvaa nguo za kijani unadhani watakaa pamoja na kupigania haki zao? Na ccm wanakuahidi mambo mengi kabla hawajakupata ukikubali tuu kuwa nao ndio mwisho wako.
 
Back
Top Bottom