SoC03 Mchango mkubwa unaofanywa na mafundi ujenzi anayejenga majengo ya serikali kwa mfumo wa force account

Stories of Change - 2023 Competition

Mkandarasi mdogo

New Member
Joined
Jun 1, 2023
Posts
2
Reaction score
4
Mimi ni fundi ujenzi nimesomea chuo cha ufund Arusha, Mwaka 2018 nilipata kazi ya kitui cha afya umaliziaji wa jengo la mama na mtoto. Nilifanya kazi hiyo nikiwa kama fundi msaidiz kwani alishika tenda ni fundi mwingine tulikubaliana kuwa atanilipa tsh 15000 kwa siku hata hivyo kwa huku kijijin ilikua ni bei kubwa zaidi nilianza kazi hiyo vizuri aliomba kuwa hatakuwa na hela ya kulipa kila siku hivyo atanlipa atakapo lipwa na kamati ya ujenzi ya kituo hicho cha afya niliendelea na kazi hiyo kwa muda wa mwezi mmoja na Zaid hata hatimaye alilipwa na kamati hiyo tayari nlikua na dai zaid ya laki sita alikuja site na kuniambia kuwa hela haikutoka yote hivyo atanipa tu laki mbili na ingine atanlipa akilipwa tuliendelea hivyo hivyo nkiamini ntalipwa pesa baadae deni lika fika milion nkamwambia tuandikishane sasa ili niwe na uhakika kuwa utanlipa akasema kua atanlipa hakuna shida basi mm nkasimama kufanya kazi akaja akaniomba tufanye kazi tufanye kazi tumalizie ili tulipwe nkiamini kuwa ntalipwa nkaenda kumalizia kazi hiyo iliyo kua hatua za mwisho ya rangi na vipande vichache vya tiles nkiwa na malizia alinilipalipa tena kama laki nne kwa hawamu tofauti tofauti

Baada ya kazi kuisha kulikua na mvutano mkubwa baina ya kamati hizo na mafundi walio shiki tenda kwani kazi iliisha mwezi wa saba ambapo serikali ufunga akaunti zake kwaajili ya kuanza hesabu za Mwaka wa fedha hivyo mafundi hawakulipwa. Basi nlikua naendelea na kazi nyingine ndogondogo za mtaani nkiwa naulizia ulizia malipo yangu ambapo nlikua nadai laki saba na tisin na tano niliendelea kumuulizia hivyo bila majibu ya msingi.

Siku moja nikaamua kwenda kuuliza pale kituo cha afya nikamkuta daktari mfawizi wa kituo hicho ambaye alikua katibu wa kamati hiyo nkamuuliza mbona hamjatulipa hadi sasa ni mwezi tisa tangu kazi ilipo Isha mwezi wa sita? Akanjibu akaniambia "hakuna pesa inayo daiwa kwenye kituo hicho tumesha lipa mafundi wote pesa ambayo wanaisubiri ni pesa ya muda wa matazamio ambayo hulipwa baada ya jengo kumalizia muda wa matazamio kipindi cha miez sita. Pesa hiyo huwa ni asilimia tano ya mkataba, fundi huyo alikua akidai kiasi cha tsh laki sita tu. Niliwaza Sana maana endapo atalipwa pesa hiyo hawezi nilipa kwakua bado kuna watu wengine Wana mdai.

Nliondoka kituon hapo nkiwa na majonzi nkiamini nsharushwa tayari,nliamua kuacha kufuatilia hiyo pesa na kuamua kusonga mbele

Nilikaa nikafikiria Sana kama nimeweza kufanya kazi ya mtu na kuwekeza nguvu kubwa kiasi hicho na mm pia ni mzoefu wa kazi hizi kwani nshafanya kazi na makampuni ya ujenzi na taasisi nyingine nyingi kwanini na mm nisitafute mtaji na kuomba kazi ya kujenga vituo vya afya zahanat madarasa na majengo mengine ya serikali Basi nlianza mchakato wa kutafuta mtaji.

Nlifungua akaunt ya benk na nlianza kwa kuweka hela kila nkipata. Nlijiwekea mtaji hadi ikafika laki nane niliendelea kusogea kufanya kazi za serikali ili kupata uzoefu zaid.

Hatimaye shule moja kati ya nlizofanya kazi walitangaza mradi wa ujenzi wa maboma ya madarasa manne na ofisi mbili na mm nlikua mmoja kati ya walioomba kazi ambapo tulikua mafundi watatu nlipata changamoto kubwa kwani kamati walinijua kama fundi msaidiz na mpizani wangu alikua ni fundi nliyefanya naye kazi shulen hapo. Mpinzan wangu alinishinda na kupewa kazi ile sikukata tamaa Sana kwani nlijua tu kuwa changamoto ni lazima kuwepo.

Nlirudi mtaani kufanya kazi za watu binafsi kwani kwani nisingeweza tena kufanya kazi chini ya mtu ili nisikutane na changamoto kama hiyo. Mtaani haswa kijijin kwetu watu wengi huamini kuwa fundi anayejenga majengo ya serikali wapo makini Sana na hata bei zao zipo juu hivyo na watu wengi wanapenda kujenga nyumba kwa bei nafuu hivyo kutumia mafundi wa kawaida Sana na ambao hawajasomea na pia hawana uzoefu kwaiyo mtaani ni shida Sana kupata kazi ukiwa ww unajenga majengo ya serikali au umesomea na unauzoefu.

Siku moja nliambiwa Kuna mwalim ananitafuta Basi na
Mm nkaomba namba yake nkampigia akaniambia wanao mradi wa ujenzi wa choo shulen kwao na kunipa maelezo kuwa tayari wamesha tangaza na ameomba fundi mmoja hivyo kwa mujubu wa Sheria za force account nilazima tenda ishindanishwe kwa watu Zaid ya watatu hivyo alinishauri niombe kazi ili niwe mshindani. Nliandika barua ya kuomba kazi ya ujenzi wa choo shulen hapo na kuambatanisha viambatanisho vyote pamoja na form ya gharama za ujenzi niliiwasilisha shulen hapo.

Siku ya kikao cha ufunguzi wa zabuni ilipo fika sikuweza kuhudhuria

Nilipigiwa simu na katibu wa kamati akiniambia kuwa nimeshinda dhabuni kwakuwa pesa niliyoomba imeendana na makadirio yao hivyo alinitaka kwenda site kwaajili ya kujaza mkataba na kuanza kazi mara moja.

Nlipiga hesabu ambapo nakuona nitafute mafundi watatu na mm niwe wa nne na wasaidizi wasiopungua sita na nkawapata.

Tulifika site ambapo tulianza kufanya usafi eneo la kazi na kuchimba msingi tulikimbizana na kazi hiyo Hadi kufikisha mabanda yote usawa wa lenta juu ya madirisha ambapo tulisimama kutokana na kukosa mbao za form work nliomba malipo ya hatua tuliyokuwa tumefikia. Malipo hayo pia yalisumbua kwa muda hayakufanyika kwa wakati.

Baadae walifanikiwa kunilipa na kununua mbao ambapo kazi iliendelea tukamalizia maboma na kuanza umaliziaji (finishing)

Safari yangu ilianzia hapo na nikapata kazi nyingine nyingi Kuna nyingine zilikua na malipo mazuri na nyingine ninafanya tu ili kuisaidia serikali na jamii.

NILICHOGUNDUA

Mafundi wanao shika tenda za ujenzi wa madarasa, zahanat, vituo vya afya au majengo mengine ya serikali kwa muongozo wa force account hawana sapoti yeyote kutoka popote hata hivyo bado serikali haiwathamini na kujali mchango wao katika jamii, Imekuwa Jambo la kawaida fundi anapo shika kazi anawalipa vibarua wake hadi jengo kufika hatua fulan tatizo linakuja anapoanza kuomba malipo anajibiwa amsubiri injinia aje kukagua kazi,injinia anaweza asije site wiki au Zaid kumbuka fundi anawatu wanaomtegemea awalipe pia anatakiwa kukimbizana na mkataba kamati nao kupitisha malipo ya mafundi wanakua wazito hadi malipo yapitishwe fundi amehangaika haswa.

Pengine wanajenga maboma vijijin kwa fedha za michango ya wananchi Mara nyingi hizo fedha za michango ya hiari huwa mafundi hawalipwi zote lazima Kuna dosari kwenye pesa hizo na hapo tatizo huanzia unakuta fundi umeshika tenda ya darasa umewaajiri vibarua umejenga boma Hadi lina simama mwisho wa siku unaaza kuja kupewa laki au unapewa nusu ya mkataba huku ww ukiwa umetumia milion kujenga maboma Jambo hilo linaturudisha nyuma mafundi wengi.

Fundi anayeshika tenda ya serikali anapaswa kuthaminiwa maana ni kitendo cha ki uzalendo Sana kwanza anajenga kwa bei rafiki pia anawekeza nguvu kubwa pale.

Fundi wa vyuma (warlding) anakopa vyuma dukani ili atengeneze madirsha anasafirisha hadi site bado anakaa muda mrefu kusubiri malipo.

Naishauri serikali iwasaidie mafundi waweze kujiajiri kwani ukitoa bodaboda kikundi kinachofuata kwa ukubwa kwa kupunguza changamoto za ajira ni mafundi. mafundi Wana mchango mkubwa Sana kwenye jamii na serikali, pia mafundi Hawa niwalipa Kodi wazuri, serikali ije na mpango wa kuwawezesh mafundi wote ili kuwapa moyo, angalau serikali iwajengee uwezo ili mabenki yawatambue wakopeshwe wapewe mitaji kwaajili ya kukuza soko la ajira ukimpa fundi mmoja mtaji umewezesha mafundi Zaid ya 30 walio nyuma yake kujipatia riziki nakuwaondoa kwenye wimbi la umaskini pia unawawezesha mama ntilie wanaouza chakula site kujipatia ridhiki hivyo serikali iangalie kwa undani swala hilo.

Serikali iwe na utaratibu wa kuwapa mafunzo mafunzo hata kwa Mwaka Mara moja na kuinua ujuzi wao tukipatiwa elim tutafanya kazi kwa ubora zaid kwani ujenz unakua Zaid na tutaweza kuwajengea wananchi nyumba imara pamoja na kutekeleza miradi ya serikali kwa kiwango cha juu zaid hivyo tutaisaidia serikali na jamii kujenga kwa bei nzuri na kazi nzuri.

Pia serikali ituundie chama cha mafundi Tanzania kama vilivyo vyama vingine kama vya wafanya biashara vyama vya madereva na vyama vingine vingi
 
Upvote 2

Hongera sana kwa kupambana lakini Mimi pia ni shahidi wa baadhi ya changamoto mnazokumbana nazo hata zinazohusu malipo ya fedha zenu.
Lakini pia Kuna wengine miongoni mwenu siyo waaminifu msiposimamiwa mkipata nafasi hata kidogo mnaanza kuiba vifaa vya ujenzi kama vile sementi.
 
Back
Top Bottom