BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,122
- 4,060
Mchango wa Banda!
Na BabaDesi
Wazo nililipata wakati nikipopokea Kadi ya Saba kwa Mwezi huu ikinitaka kuchangia Sherehe za Harusi ya Binti mmojawapo wa ndugu zangu kadhaa nilio nao jijini. Ndugu ambao ajabu idadi yao inakuwa chax che sana nikitaka ndugu wanikope hela kidogo ili tarehe zikutane lakini idadi yao inakuwa kubwa sana kukiwa na michango ya Harusi, kama huyu.
Wazo likaniingia. Kwa sababu Watanzania ni Watu wanaopenda sana kutoa michango kwa nini nisitengeneza Kadi nzuri ya kuomba Michango kwa ajili ya kumalizia Ujenzi wa Banda langu la Kuishi ambao ulikuwa umesimama kwa muda mrefu sasa kutokana na Sababu hizi na zile!
Ilikuwa dhahiri sasa kwamba kama sitachemsha akili zangu haraka nilikuwa na hatari ya kuishia kuwa kama Manyani ambayo Wazee wetu wametuhakikishia kwamba wameshindwa Kujanga Nyumba za kujihifadhi kwa vile wamekuwa watu wa Ahadi tu za ‘Kesho, Kesho’! Kwamba Jua likiwaka Hakumbuki kujenga Makazi lakini Mvua ikinyesha na Kuwanyeshea wanakumbusha kuwa Kesho wajenge Nyuma!
Na katika hili la Manyani mimi sikuwa tofauti sana nao maana tumeishaambia sisi tumetoka kwenye Uzao wa Manyani, Kasoro Mikia tu! Kwa Kutojenga Nyumba mimi nilikuwa ninaelekea huko kwa ‘Ndugu’ zangu Manyani na tofauti yetu ingekuwa tu kwenye kuwa ‘Nyani kasoro Mkia!’
Sikuwa tayari kuwa ;Nyani Kasoro Mkia’ na ngoja ngoja yake ya ‘Kesho’. Nikachemsha Akili Haraka; Je Wabongo walio tayari kuchangia mtu hata kwenye kusherehekea Siku yake ya kuzaliwa na ya kuozesha ama kumuoza kijana wa familia kwa sherehe ya masaa Sita tu, hawatakuwa tayari kunichangia mimi kwenye jambu muhimu linalohusu Uhai wa Binadamu mwenzao la kumchangia kumalizia Banda lake la kuishi na Wategemezi wangu ambalo litadumu kwa miaka Mia Moja ijayo na litakuwa faida hata kwa vizazi vijavyo?
Nikamuleza wazo langu huyu Kiumbe tunayebanana naye kitanda kimoja kwa miaka kadhaa sasa. Kwanza akaguna tu kuonyesha kwamba alikuwa hakubaliani nalo sana. Lakini nilipomkazania sana kunieleza sababu za kwa nini hakubaliani na wazo langu, akaishia kuniambia atanisaidia lakini akaweka tahadhari ya “Huwajui WaTanzania wewe!” Pale sikumulewa. Nikajua hataki tu maendeleo yetu.Nikajua analeta ubishi wa Kike tu kwa wazo Babu Kubwa la Kiume. Ole Wangu.
Katika kumfanya Kiumbe akubaliae na Wazo langu, nikamuambia kuwa mimi sio binadamu wa kwanza kufanya hivyo, labda kwa hapa Tanzania. Nikamuambia kuwa kule Nchi Jirani wameishapita hapo pa kuchangiana Send-off, Kitchen Party na hata Siku za Kuadhimisha Kuzaliwa! Wao sasa walikuwa wanaitishana Harambee za kuchangiana Mastibabu na Elimu ya Juu! Kwa Umuhimu huu, Mimi nikianzisha Wazo la Kuchangiana Ujenzi wa Nyumba za Kuishi si Wazo litashika Moto wa Nyika! Bibie akaishia tu kusema “We haya Wee!” Sikumuelewa.
Basi Bwana, nikaingia gharama kubwa za kuteneza Kadi za Mwaliko wa kuchangia Banda kwa wale wote ambao Kadi zao za kunitaka nichangie kwenye Sherehe zao zilipata kukatisha kwenye macho yangu, na zikachangiwa kilichowezekana…na zikanifilisi zaidi!
Nikaziandaa Kadi zangu za bei mbaya za Mualiko.: “Bwana na Bibi BabaDesi wanayo heshima kukualika Bwana/Bibi/ Ndugu/Professor Mwanagutu Mwafulani kwenye Kikao cha kwanza cha kuchangia Mchango wa Kumalizia Ujenzi wa Banda lao la kuishi linalojengwa huko Mbezi Mwisho Darisalama. Kufika kwako ndio kufanikisha shughuli hii Muhimu. Asante.
Nikazigawa kadi zangu kwa ndugu,jamaa na marafiki ambao niliona kwamba panga pangua wasingekosa hata kuchangia hata gharama za Ladi tu za Bei Mbaya nilizotengeneza kwa ajili ya Kuwaita kwenye Mchango nikijipa matumaini kuwa kwa vile mimi niliwachangia wengine hata kwenye Birthday zao achilia mbali Harusi za Watoto wao basi na wao wasingeniangusha kwenye jambo muhimu sana kama la Kumalizia Ujenzi wa Makazi ya Kuishi!
Ilikuwa ni zamu yao sasa kufanya ‘Vitu Vyao’ vya kunichangia Mimi. Ndio, Watoto wangu walikuwa bado wadogo sana na bado walikuwa hawastahili kujiingiza ama kuingizwa kwenye mambo ya kuchangiwa sherehe za kuoa ama kuolewa. Lakini huu ulikuwa Mchango wa ujenzi w Nyumba! JKwa nini Wasichangie Suala muhimu sana kama hili?
Siku ya siku ilipokaribia nikayeyusha Mshahara wangu ili kukodisha viti Sitini na kununua Soda na sambusa Mia mbili Mia Mbili ili watu wachange vizuri bila kiu! Siku ya Siku ikafika na mimi na Mwenza wangu tukajiandaa kupokea wageni. Hakuna aliyekuja. Tukasubiri, Tukasubiri, Tukasubiri weee. Hakuna aliyetokea. Ndio, hakuna hata Mmoja aliyetokea kwenye Kikao Chetu cha Mchango wa Kumalizia Ujenzi wa Makazi!
Viti Sitini vile vikabaki kutukodolea Macho kama Vikitusuta Kwamba kweli inaelekea hatujawajua Vema Watanzania! Kwamba walikuwa tayari kuchangia hata Birthday ya Mtu na hata Kumuzesha Mwanawe lakini sio Kuchgia Kumalizia Ujenzi wa Nyumba ya Ndugu yao, hata kama itakaa Miaka 100 na inaweza Kuja kuwasaidia hata Watoto wao.
Tukaishia kukaa kwenye Viti vyetu Sitini kama watoto yatima na kula Sambusa na soda Mia Mbili wenyewe na kuzigawa bure nyingine kwa Wapangaji wenzetu! Viti Mia Sitini vile vikanimbia wazi kuwa Jamii yetu ilikuwa bado sana. Kwamba walikuwa radhi kuchangia Sherehe za Masaa yasiyozidi Sita za Kula, Kunywa na kucheza muziki lakini sio kuchangia ujenzi wa nyumba ya binadamu mwenzao itakayodumu hata Miaka Mia!
Angalau Usiku wa Siku ile Familia yangu haikuwa na Gharama ya kuandaa Chakula cha Usiku. Sambusa na Soda Mia Mbili, hata kama Nyingine tuligaia Majirani, ni Msosi tosha wa Usiku! Pamoja na ‘Majeraha’ yangu, bado ninafikiria kuliendeleza Wazo langu. Wana Jamii, tusichangiane tu kwenye Birthday, Kitchen Party na Send Off, bali tuitishe Harambee kuchangia Elimu ya Juu, Matibabu na Kadhalika. Wenzetu Majirani wana nini cha Ziada waweze Hivyo, na sisi tushindwe tuna nini, wakati wote Asili yetu niNyani?
Maneno ya huyu kiumbe ninaye banana naye kitanda kimoja yakatimia “Bado Huwajui wabongo wewe!” Nahisi Sasa nawajaua.
babaDesi / 0754 340606

Attachments
Upvote
0