Mchango mkuu wa Chomsky kwanza ni katika isimu kwa jumla na halafu ktk taaluma ya Kiswahili. Ktk isimu kwa jumla ni kuibua swali hili: Watoto wanawezaje kujifunza lugha tunavyowaona ktk muda mfupi sana, bila kufundishwa sarufi, na kwa hatua zile zile katika kila lugha? Jibu lake ni katika nadharia tete kwamba tumeumbwa na lugha. Lugha iko katika mfumo wetu wa utambuzi. Hii inaitwa sarufi bia. Toka hapo, wanasarufi wengi wanajishughulisha na kujaribu kugundua kanuni, sheria, na ruwaza ambazo tunaweza kuziita sarufi bia na pia kwa kuangalia tofauti za lugha zinatokana na nini hasa. Chomsky aliweka kiunzi kikuu cha nadharia ya isimu ni kuweza kutoa majibu kwa swali hilo la sarufi bia kwa namna ambayo inaonesha jinsi watoto wanavyojifunza lugha kwa urahisi.
Kiswahili ni lugha moja ambazo zimechunguzwa mintarafu masuala kadha ya sarufi bia. Chomsky mwenyewe hakukichunguza Kiswahili. Wako watu kadha washirika wake na wanaofuata mkabala wake ambao wameangazia mambo kadha katika Kiswahili. Sehemu kubwa ni katika kujaribu kuangalia ni kanuni gani zinazohusika katika uundaji wa maneno. Kuna wanaosema kwamba kanuni za uundaji wa virai na sentensi ndizo pia zinatumika katika kuunda maneno. Mfano mkubwa ni jinsi tunavyoweza kuunda sentensi kwa kutumia neno moja tu la kitenzi. Basi wanaisimu wanaangazia unyambulishaji na uambishaji, nk