Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kwa kumpongeza Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb) kwa uwasilishaji wake mzuri wa hotuba yake ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2024/2025.
Mheshimiwa Spika, Niwapongeze Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na taasisi nyingine chini ya Wizara hii kwa namna wanavyofanya kazi.
Aidha nimeshindwa kujizuia kumpongeza kwa dhati Mhandisi Victor H. Seif, Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Boniface Mkumbo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Gaston Pascal, Meneja wa TARURA Mkoa wa Simiyu na Mhandisi Elieza Mayengo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Meatu kwa namna wanavyosimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja katika Jimbo la Kisesa na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla. Hongereni Sana.
Hotuba ya Waziri Ibara ya 18 na baadhi ya Ibara zingine imeorodhesha miradi mingi ya barabara na madaraja yaliyokamilika miaka ya nyuma na kuanza kutumika na hivyo siyo sehemu ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2023/2024 na mipango ya bajeti ya 2024/2025. Nini sababu za Waziri kurejea miradi iliyokamilika tangu mwaka 2021 kwenye hotuba ya bajeti yake?
Barabara hii ipo kwenye ahadi zilizotolewa na Viongozi wakuu wa kitaifa na katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020. Waziri atuambie, Je ni nini kinachosababisha Serikali kuwapiga danadana wananchi wa Jimbo la Kisesa na Mkoa wa Simiyu kuhusu barabara yao hiyo ya lami?
mipango miradi inayoorodheshwa ni ile iliyopangiwa fedha katika mwaka husika.
Waziri wa Ujenzi awe makini na mipango ya aina hii ambayo inaweza kuwa ni sehemu ya kufuja fedha za umma na kufanya upendeleo katika ugawaji wa raslimali za nchi.
Miradi mingi imetajwa katika hotuba ya Waziri lakini haina kasma ya fedha na miradi mingi ni ahadi za muda mrefu, Deni la
wakandarasi zaidi ya Tsh. Bilioni 900, Kamati kwa kuliona hilo imeomba bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo iongezwe hadi kufikia Trilioni 5 ili kuwezesha ujenzi wa viwanja vya ndege, barabara na madaraja kote nchini. Lakini pia kuna miradi hewa ya EPC+F.
Waheshimiwa wabunge nawaomba tuungane na Mheshimiwa Flatei Gregory Massay (Mb), Mbunge wa Mbulu Vijijini tuikatae bajeti hii na tuirudishe Serikalini ikafumuliwe na kuandaliwa upya.
Mafinga-Mtwango-Mgolololo (Km 81)
Majibu na Maelezo mawaziri hao yapo kwenye Hansard za Bunge. Leo tena Bunge linaletewa majibu mengine kwamba Serikali inaendelea na mazungumzo na wafadhili ili kupata fedha za
utekelezaji wa miradi hiyo. Majibu yote matatu yametolewa kwa nyakati tofauti tofauti Bunge lishike majibu gani?
Maelezo ya kwamba wakandarasi wanafanya upembuzi yakinifu kwa kipindi cha mwaka mzima ni ya uongo na hayakubaliki na kwamba wakandarasi hao wasingekubali kusaini mikataba bila kujua mahitaji na gharama za miradi wanayokwenda kuitekeleza.
Wizara na TANROADS wasingefikia hatua ya kusaini Mikataba bila kujiridhisha mahitaji na gharama za miradi. Hata inapodaiwa kuwa wakandarasi watafanya upembuzi yakinifu ni marudio ya kazi ambayo tayari imeshafanywa na wataalamu wetu wa Wizara na TANROADS. Pia suala la kutafuta fedha za kugharamia miradi kwa utaratibu wa EPC+F siyo la Serikali hivyo majibu ya mawaziri yanalenga kulipotosha Bunge kwa makusudi.
Awali siku ya kusaini mkataba huu ambapo baadhi ya waheshimiwa wabunge tulishiriki tukio hilo liliofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convection Dodoma tarehe 16 Juni 2023, nilipinga wasilisho la Waziri la kuitambulisha miradi hiyo kwa kuwa hapakuwa na uwazi wala maelezo ya kina, miradi hiyo inatekelezwa kwa utaratibu upi kwani masharti na vigezo vya mikataba hiyo havikuwekwa wazi ilikuwa ni siri kati ya Waziri na Wakandarasi.
Nilihoji siku ya kusaini Mikataba na ndani ya Bunge nini faida ya kutumia EPC+F badala ya utaratibu wa kawaida wa Serikali kuajiri na kulipa wakandarasi, Wakandarasi wa EPC+F watalipwa kwa utaratibu gani baada ya miradi kukamilika au kila baada ya kipindi gani.
Pia nilihoji madhara ya kutumia utaratibu wa EPC+F kuwa ni wa gharama kubwa kwani gharama zinapatikana kwa matamko ya
mkandarasi na mara nyingi EPC+F hutumiwa na nchi ambazo hazikopesheki, mkandarasi ana hiari ya kununua vifaa vya ujenzi kokote Duniani na kuajiri wafanyakazi kutoka sehemu yoyote na hivyo kuwaacha vijana wa kitanzania bila ajira. Kupanua goli la ukopaji mikopo nje ya utaratibu uliowekwa na kuliingiza Taifa kwenye mzigo mkubwa wa madeni, Usimamizi dhaifu wa miradi kwa kuwa mkandarasi anatoa fedha mwenyewe na hivyo jicho la Bunge na CAG haliwezi kuwafikia, na kuna hatari kubwa ya kujenga miradi chini ya kiwango na kwa gharama kubwa.
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Mwaka 2022/2023 imethibitika kuwa mikataba hii ilisainiwa bila kuwa na ufadhili wa uhakika wa miradi hiyo na wakandarasi wameshindwa kuwasilisha dhamana ya Benki ya utendaji kazi (Performance Bonds) yenye Thamani ya Tsh. Bilioni 375.51 kama matakwa ya mkataba na ndiyo sababu ya miradi hii kushindwa kuanza hadi sasa.
Bunge limekuwa likipewa majibu tofauti tofauti ya ucheleweshaji wa kuanza utekelezaji wa miradi hii lakini CAG ameenda kubainisha wazi ukweli uliokuwa unafichwa kwa nguvu kubwa na Mawaziri kwa faida wanazozijua wao. Hapa inazua maswali mengi ya kujiuliza wakandarasi walipatikanaje hadi wakasaini mikataba wakiwa hawana sifa na uwezo wa kifedha, mkataba wa EPC+F uliwezaje kusainiwa bila kujiridhisha na masuala ya msingi ikiwemo ufadhili wa fedha za mradi. Hadi sasa Serikali haijachukua hatua yoyote dhidi ya wakandarasi kwa kuchelewa kuanza utekelezaji wa miradi ya EPC+F kwa mujibu wa mikataba na badala yake Serikali imekuwa msemaji wa Makampuni hayo.
Hapa kuna kila dalili ya harufu ya Rushwa na taifa letu kuingizwa kwenye Mikataba ya kinyonyaji, kwa sehemu kubwa Makampuni yaliyopewa kazi kwa utaratibu wa EPC+F ni ya kutoka China na ni
yale yale yanayopewa kila mradi mfano Kampuni ya CCECC inatekeleza mradi wa SGR, Mradi wa Maji wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na miradi mingine ya maji, barabara na madaraja, ujenzi wa Bandari nk. vigezo na masharti ya mikataba hadi sasa hayafahamiki kwa umma.
Kutokana na mkanganyiko wa maelezo ya mawaziri wanayoyatoa hapa Bunge na kukosekana kwa hatua zilizochukuliwa kwa wakandarasi hao hadi sasa, inawezekana Mawaziri hao na watendaji wengine wa Serikali walikula njama na Makampuni hayo kufanikisha kusainiwa kwa mikataba hiyo ili kuyawezesha Makampuni hayo ya kichina kuitumia Mikataba hiyo kama dhamana ya kupata mikopo katika Taasisi za Fedha za kimataifa kwa ajili ya matumizi mengine tofauti na utekelezaji wa miradi yetu ya EPC+F. Hivyo dhamana ya Mikataba yetu kutumika kufanikisha biashara ya Makampuni ya Kichina na watu binafsi.
Pia unaweza kuwa ni mkakati wa makusudi wa kuliingiza taifa letu kwenye mizozo na migogoro ya kisheria kimataifa na baadaye nchi yetu kutakiwa kulipa matrilioni ya shilingi.
Aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amekuwa akitumia nguvu kubwa kulipotosha Bunge na Umma wa Watanzania kwa makusudi kuhusu faida za miradi ya EPC+F na akituita baadhi ya wabunge tuliohoji Mikataba hii kuwa ni wapotoshaji na tuna nia mbaya.
Nchi yetu imejenga mtandao mkubwa wa barabara za lami na madaraja makubwa na madogo kwa utaratibu wa kawaida wa kutangaza na kuajiri wakandarasi kwa kutumia fedha zetu za ndani na mikopo kutoka nje. Leo Serikali imesukumwa na nini kwa siku 1 kusaini mikataba ya ujenzi wa Kilomita 2035 kwa mara
moja yenye thamani Tsh. Trilioni 3.75 tena kwa kutegemea mikopo kutoka nje.
Pia Waziri Mbarawa siku ya kusaini Mikataba hii alikiri kwamba hata alipowashirikisha TANROADS kwa hatua za awali walipinga utaratibu wa EPC+F lakini yeye akatumia madaraka yake kulazimisha kusainiwa mikataba hiyo.
Serikali imetumia gharama kubwa kuandaa miradi hewa na kupeleka ahadi hewa kwa wananchi wa maeneo yaliyotajwa na mbaya zaidi wananchi wa mikoa inayopitiwa na miradi 7 ya barabara wameondolewa kwenye mipango na bajeti ya mwaka 2023/2024 na 2024/2025 kwa kuwa barabara zao zitajengwa kupitia utaratibu wa EPC+F.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inakiri kwamba hakuna kinachoendelea katika miradi ya EPC+F, Hotuba ya Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa katika Ibara ya 40 ukurasa wa 36 anakiri kuwa miradi hiyo haina chanzo cha fedha na bado haijaanza na kwamba Serikali inaendelea na mazungumzo na wafadhili ili kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo. Miradi tuliyoambiwa ina ufadhili wa moja kwa moja yaani mkandarasi anayejenga atatumia fedha zake na baadaye kuidai Serikali, leo tunaambiwa anatafutwa mfadhili wa kugharamia miradi hiyo. Hii inaleta sintofahamu na mkanganyiko mkubwa.
Waziri Profesa Mbarawa ameichonganisha Serikali na Mheshimiwa Rais mbele ya wananchi, amekichonganisha Chama cha Mapinduzi na wananchi kwa ahadi hewa ya ujenzi wa barabara kilomita 2,035, Na kwa kuwa, kuna dalili na harufu ya Rushwa vyombo vya uchunguzi TAKUKURU, DCI na DPP wachukue hatua kwa Prof Mbarawa na wote waliohusika kwenye kashfa hii, kwa
makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi na kwa mujibu wa Kifungu cha 27 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008.
Nashauri Mikataba yote ya EPC+F ivunjwe na miradi hiyo ifutwe kwenye vitabu vya Serikali. Pia bajeti ya Wizara ya Ujenzi ya mwaka 2024/2025 irudishwe na ifumuliwe upya ili kuwezesha majimbo, wilaya na mikoa iliyokuwa imeingizwa kwenye miradi hewa ya EPC+F ipangiwe upya fedha katika bajeti ya mwaka 2024/2025.
Tumekuwa tukihoji sana suala hili hapa Bungeni lakini hatupati majibu kutoka serikalini, binafsi nimehoji kwa kusema na kwa michango ya maandishi ya mara kwa mara bila majibu, Serikali inawezaje kuanzisha mchakato unaohusu kutwaa au kutumia ardhi ya umma bila kibali cha Bunge, Hifadhi ya Barabara tuliyonayo ni mali ya umma kwa matumizi ya umma, Wizara ya Ujenzi haina mamlaka ya kukabidhi maeneo ya hifadhi za barabara kwa mwekezaji wa sekta binafsi bila kibali cha Bunge.
Kuna mkanganyiko mkubwa wa mipango ya Serikali na pengine huoni kama kuna nia njema kwani huwezi kuja na mradi wa ujenzi wa barabara ya kulipia kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro- Dodoma (Express Way) yenye urefu wa Km 531.8 kwa utaratibu wa PPP. Huku kuna mradi mkubwa wa SGR ambao uko hatua za
mwisho kukamilika na utaanza kutoa huduma Julai 2024. Mradi huu unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari barabarani kwa zaidi ya 60%. Hii ni mipango Mibovu na matumizi mabaya ya raslimali za umma.
Uzoefu unaonyesha kuwa nchi zilizojenga barabara za kulipia huacha kwa makusudi kukarabati njia Mbadala ili wananchi walazimike kupita katika barabara za kulipia. Lakini pia Makampuni ya ubia yamekuwa yakiweka bei kubwa za tozo na kusababisha gharama za usafiri na usafirishaji kuwa juu na hivyo kuchochea mfumko wa bei za bidhaa na ugumu wa maisha. Kama nchi tumejipangaje kabla ya kuiendea miradi ya namna hii. Ikumbukwe kuwa barabara hii inatoka kwenye lango kuu la uchumi wa nchi yetu yaani Bandari ya Dar es Salaam kwenda kwenye mikoa na mataifa mbalimbali ya nchi jirani.
Mchakato unaoendelea wa kumpata mkandarasi ni kinyume cha Sheria ya Ardhi na Sheria ya Raslimali inayotaka hatua zote kuwa wazi na Bunge kujulishwa. Leo Waziri atuambie ukweli juu ya faida ya mradi huu. Nchi yetu imejenga na imeunganisha mikoa yote kwa barabara za kiwango cha lami, tumejenga mtandao mkubwa wa SGR leo hatuna fedha za kujenga njia nne kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro hadi Dodoma? Au kuna jambo lililojificha nyuma ya pazia kwenye miradi hii ya PPP.
Tulishaanza safari ya upanuzi wa barabara ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo ujenzi wa barabara wa njia 8 umeshakamilika kutoka Kimara hadi Kibaha na hivyo tunaweza kuendelea kutenga bajeti kwa awamu hadi Chalinze na baadaye Morogoro na Dodoma ikizingatiwa kuwa miradi mingi ya kimkakati iliyokuwa inachukua fedha nyingi inakamilika ya Bwawa la Nyerere, Daraja la JPM (Kigongo Busisi), SGR.
Tume ya Mipango iko wapi hadi mipango mibovu kama hii kuendelea kwenye nchi.
Miradi mingine inayoanishwa kutekelezwa kwa njia ya PPP haina tija na inaweza kusababisha hasara kubwa mfano Daraja la Pili la Kigamboni (Magogoni-Kivukoni) daraja hili linapendekezwa kujengwa wakati tunalo Daraja la Nyerere (Kigamboni) lilojengwa na Mfuko wa NSSF hivyo kujengwa daraja lingine la kulipia litaua biashara ya Daraja lililopo na kushindwa kurejesha mtaji wa uwekezaji wa shirika hilo. Lakini pia eneo linalopendekezwa kujengwa daraja la pili kuingilia Meli katika Bandari ya Dar es Salaam.
Nashauri Serikali ifute michakato inayoendelea wa kutafuta mkandarasi wa kujenga mradi wa barabara ya kulipia kutoka Kibaha hadi Dodoma kwa utaratibu wa PPP na badala yake ifanye tathmini upya kubaini maeneo na miradi yenye faida Kiuchumi kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP.
Ni jambo la kushangaza kuona udhaifu wa usimamizi wa Mikataba na mipango mibovu kiasi hiki wakati tuna Tume ya Mipango, Wizara inayotekeleza miradi mikubwa ya madaraja, barabara za lami na changarawe, viwanja vya ndege na vivuko kutengewa fedha ndogo kiasi cha Tsh. Trilioni 1.6 tu huku miradi mingi ya
kimkakati iliyokuwa inachukua fedha nyingi imekamilika na mingine iko hatua za mwisho kukamilika.
Aidha ifahamike kuwa mipango Mibovu inaliangamiza taifa letu kwa kiasi kikubwa, hivyo kupitia Tume ya Mipango ni lazima kufuatilia upya na kuongeza fedha katika Wizara hii na miradi yote isiyo na tija ifutwe katika vitabu vya Serikali.
Mambo mengine ni mepesi hayahitaji hesabu ngumu ni rahisi mno it does not need hot calculations to do it like calculus, statistics, combination and permutation, it is a low hanging fruits. Ni lazima mipango yetu iwe ya wazi na Uwajibikaji katika kuliletea taifa letu maendeleo endelevu.
Mheshimiwa Spika, Niwapongeze Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na taasisi nyingine chini ya Wizara hii kwa namna wanavyofanya kazi.
Aidha nimeshindwa kujizuia kumpongeza kwa dhati Mhandisi Victor H. Seif, Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Boniface Mkumbo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Gaston Pascal, Meneja wa TARURA Mkoa wa Simiyu na Mhandisi Elieza Mayengo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Meatu kwa namna wanavyosimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja katika Jimbo la Kisesa na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla. Hongereni Sana.
MAMBO YA KIUJUMLA
Miradi ya Ujenzi wa Barabara na Madaraja yaliyokamilika miaka ya nyuma kurejewa kwenye hotuba ya Waziri ya Mwaka 2024/2025
Hotuba ya Waziri Ibara ya 18 na baadhi ya Ibara zingine imeorodhesha miradi mingi ya barabara na madaraja yaliyokamilika miaka ya nyuma na kuanza kutumika na hivyo siyo sehemu ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2023/2024 na mipango ya bajeti ya 2024/2025. Nini sababu za Waziri kurejea miradi iliyokamilika tangu mwaka 2021 kwenye hotuba ya bajeti yake?
Ujenzi wa Kiwango cha Lami wa Barabara ya Bariadi-Kisesa-Mwandoya –Ngh’oboko Km 102
Barabara hii kwa muda mrefu imekuwa ikiripotiwa iko kwenye hatua upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na tulitegemea leo tutaambiwa hatua ya awali imekamilika na ujenzi umeanza lakini cha kusikitisha Hotuba ya Waziri Ibara ya 131 (C) (viii) ukurasa wa 73 inaeleza kuwa Serikali ipo katika taratibu za Manunuzi kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.Barabara hii ipo kwenye ahadi zilizotolewa na Viongozi wakuu wa kitaifa na katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020. Waziri atuambie, Je ni nini kinachosababisha Serikali kuwapiga danadana wananchi wa Jimbo la Kisesa na Mkoa wa Simiyu kuhusu barabara yao hiyo ya lami?
Miradi mingi imeorodheshwa ikiwa haina kasma ya bajeti
Mfano barabara ya Kolandoto-Lalago-Sanga Itinje-Ng’ohoboko- Mwanhuzi Kilomita 122 na Miradi mingi ya barabara na madaraja imeorodheshwa na Serikali lakini haijatengewa fedha hali inayopelekea matumaini hewa kwa wananchi. Utaratibu mzuri wamipango miradi inayoorodheshwa ni ile iliyopangiwa fedha katika mwaka husika.
Ujenzi wa Viwanja vya Ndege
Hotuba ya Waziri Ibara ya 20 ukurasa wa 19 anaripoti viwanja vya ndege ambavyo vilishajengwa miaka mingi iliyopita na kuanza kutumika. Nini sababu ya Waziri kurejea kutaja majina ya viwanja hivyo?Barabara za michepuo
Hotuba ya Waziri imeonyesha orodha ndefu ya miradi ya ujenzi wa barabara za michepuo zinazofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili baadaye zijengwe kwa lengo la kupunguza msongamano katika miji mbalimbali nchini. nimepitia miradi hiyo mingi haina ulazima kwa sasa na Serikali isiondoke kwenye jukumu la msingi la kupeleka barabara za lami maeneo mengine ambayo hayajafikiwa, haiwezekani tukaanza kuweka vipaumbele vya barabara za michepuo na kuwaacha watanzania wengine wakiwa na shida ya barabara za lami kwa miaka mingi.Waziri wa Ujenzi awe makini na mipango ya aina hii ambayo inaweza kuwa ni sehemu ya kufuja fedha za umma na kufanya upendeleo katika ugawaji wa raslimali za nchi.
Fedha zilizoombwa
Fedha za maendeleo zinazoombwa ni Tsh Trilioni 1.628 ikiwa ni ongezeko la 14.88% ya bajeti ya mwaka 2023/2024 ambapo pia ongezeko hilo ni fedha za kutoka nje.Miradi mingi imetajwa katika hotuba ya Waziri lakini haina kasma ya fedha na miradi mingi ni ahadi za muda mrefu, Deni la
wakandarasi zaidi ya Tsh. Bilioni 900, Kamati kwa kuliona hilo imeomba bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo iongezwe hadi kufikia Trilioni 5 ili kuwezesha ujenzi wa viwanja vya ndege, barabara na madaraja kote nchini. Lakini pia kuna miradi hewa ya EPC+F.
Waheshimiwa wabunge nawaomba tuungane na Mheshimiwa Flatei Gregory Massay (Mb), Mbunge wa Mbulu Vijijini tuikatae bajeti hii na tuirudishe Serikalini ikafumuliwe na kuandaliwa upya.
Mikataba ya ujenzi wa Barabara kwa utaratibu wa EPC+F
Tarehe 16 Juni 2023 Serikali ilisaini mikataba saba (7) ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya kilomita 2,035 kwa gharama ya Tsh. Trilioni 3.75 kwa kiwango cha lami kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F) kama ilivyoelezwa kwa kina katika Kiambatisho cha Jedwali namba 1 ambacho kinaonyesha jina la mradi, namba ya mkataba, jina la mkandarasi na gharama za kila mradi. Pia katika Hotuba ya Waziri miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-Mafinga-Mtwango-Mgolololo (Km 81)
Igawa-Songwe-Tunduma (Km 218)
Uyole-Songwe (Km 48.9)
Masasi-Nachingwea-Liwale (Km 175)- Arusha-Kibaya-Kongwa JCT (Km 453.42)
- Ifakara-Lupiro-Malinyi-Kilosa,Kwampepo-Londo- Lumecha/Songea (Km 435)
- Karatu-Mbulu-Haydom-SibitiRiver-Lalago- Maswa(Simiyu) (Km 339)
- Handeni-Kibirashi-Kijungu-Kibaya-Njoro-Olboroti- Mrijochini-Chambalo-Chemba-Kwa Mtoro-Singida (Km 374.24)
Tangu kusainiwa kwa mikataba hii leo ni takribani mwaka mzima umepita ujenzi haujaanza, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi wa sasa, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa walikuwa wakieleza kuwa wakandarasi bado wanafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na baadaye maelezo yakabadilika kuwa Serikali inatafuta fedha za kuwalipa wakandarasi malipo ya awali 10% ya thamani ya mradi kiasi cha Tsh. Bilioni 375.51 ndiyo kazi ya ujenzi iweze kuanza.Majibu na Maelezo mawaziri hao yapo kwenye Hansard za Bunge. Leo tena Bunge linaletewa majibu mengine kwamba Serikali inaendelea na mazungumzo na wafadhili ili kupata fedha za
utekelezaji wa miradi hiyo. Majibu yote matatu yametolewa kwa nyakati tofauti tofauti Bunge lishike majibu gani?
Maelezo ya kwamba wakandarasi wanafanya upembuzi yakinifu kwa kipindi cha mwaka mzima ni ya uongo na hayakubaliki na kwamba wakandarasi hao wasingekubali kusaini mikataba bila kujua mahitaji na gharama za miradi wanayokwenda kuitekeleza.
Wizara na TANROADS wasingefikia hatua ya kusaini Mikataba bila kujiridhisha mahitaji na gharama za miradi. Hata inapodaiwa kuwa wakandarasi watafanya upembuzi yakinifu ni marudio ya kazi ambayo tayari imeshafanywa na wataalamu wetu wa Wizara na TANROADS. Pia suala la kutafuta fedha za kugharamia miradi kwa utaratibu wa EPC+F siyo la Serikali hivyo majibu ya mawaziri yanalenga kulipotosha Bunge kwa makusudi.
Awali siku ya kusaini mkataba huu ambapo baadhi ya waheshimiwa wabunge tulishiriki tukio hilo liliofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convection Dodoma tarehe 16 Juni 2023, nilipinga wasilisho la Waziri la kuitambulisha miradi hiyo kwa kuwa hapakuwa na uwazi wala maelezo ya kina, miradi hiyo inatekelezwa kwa utaratibu upi kwani masharti na vigezo vya mikataba hiyo havikuwekwa wazi ilikuwa ni siri kati ya Waziri na Wakandarasi.
Nilihoji siku ya kusaini Mikataba na ndani ya Bunge nini faida ya kutumia EPC+F badala ya utaratibu wa kawaida wa Serikali kuajiri na kulipa wakandarasi, Wakandarasi wa EPC+F watalipwa kwa utaratibu gani baada ya miradi kukamilika au kila baada ya kipindi gani.
Pia nilihoji madhara ya kutumia utaratibu wa EPC+F kuwa ni wa gharama kubwa kwani gharama zinapatikana kwa matamko ya
mkandarasi na mara nyingi EPC+F hutumiwa na nchi ambazo hazikopesheki, mkandarasi ana hiari ya kununua vifaa vya ujenzi kokote Duniani na kuajiri wafanyakazi kutoka sehemu yoyote na hivyo kuwaacha vijana wa kitanzania bila ajira. Kupanua goli la ukopaji mikopo nje ya utaratibu uliowekwa na kuliingiza Taifa kwenye mzigo mkubwa wa madeni, Usimamizi dhaifu wa miradi kwa kuwa mkandarasi anatoa fedha mwenyewe na hivyo jicho la Bunge na CAG haliwezi kuwafikia, na kuna hatari kubwa ya kujenga miradi chini ya kiwango na kwa gharama kubwa.
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Mwaka 2022/2023 imethibitika kuwa mikataba hii ilisainiwa bila kuwa na ufadhili wa uhakika wa miradi hiyo na wakandarasi wameshindwa kuwasilisha dhamana ya Benki ya utendaji kazi (Performance Bonds) yenye Thamani ya Tsh. Bilioni 375.51 kama matakwa ya mkataba na ndiyo sababu ya miradi hii kushindwa kuanza hadi sasa.
Bunge limekuwa likipewa majibu tofauti tofauti ya ucheleweshaji wa kuanza utekelezaji wa miradi hii lakini CAG ameenda kubainisha wazi ukweli uliokuwa unafichwa kwa nguvu kubwa na Mawaziri kwa faida wanazozijua wao. Hapa inazua maswali mengi ya kujiuliza wakandarasi walipatikanaje hadi wakasaini mikataba wakiwa hawana sifa na uwezo wa kifedha, mkataba wa EPC+F uliwezaje kusainiwa bila kujiridhisha na masuala ya msingi ikiwemo ufadhili wa fedha za mradi. Hadi sasa Serikali haijachukua hatua yoyote dhidi ya wakandarasi kwa kuchelewa kuanza utekelezaji wa miradi ya EPC+F kwa mujibu wa mikataba na badala yake Serikali imekuwa msemaji wa Makampuni hayo.
Hapa kuna kila dalili ya harufu ya Rushwa na taifa letu kuingizwa kwenye Mikataba ya kinyonyaji, kwa sehemu kubwa Makampuni yaliyopewa kazi kwa utaratibu wa EPC+F ni ya kutoka China na ni
yale yale yanayopewa kila mradi mfano Kampuni ya CCECC inatekeleza mradi wa SGR, Mradi wa Maji wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na miradi mingine ya maji, barabara na madaraja, ujenzi wa Bandari nk. vigezo na masharti ya mikataba hadi sasa hayafahamiki kwa umma.
Kutokana na mkanganyiko wa maelezo ya mawaziri wanayoyatoa hapa Bunge na kukosekana kwa hatua zilizochukuliwa kwa wakandarasi hao hadi sasa, inawezekana Mawaziri hao na watendaji wengine wa Serikali walikula njama na Makampuni hayo kufanikisha kusainiwa kwa mikataba hiyo ili kuyawezesha Makampuni hayo ya kichina kuitumia Mikataba hiyo kama dhamana ya kupata mikopo katika Taasisi za Fedha za kimataifa kwa ajili ya matumizi mengine tofauti na utekelezaji wa miradi yetu ya EPC+F. Hivyo dhamana ya Mikataba yetu kutumika kufanikisha biashara ya Makampuni ya Kichina na watu binafsi.
Pia unaweza kuwa ni mkakati wa makusudi wa kuliingiza taifa letu kwenye mizozo na migogoro ya kisheria kimataifa na baadaye nchi yetu kutakiwa kulipa matrilioni ya shilingi.
Aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amekuwa akitumia nguvu kubwa kulipotosha Bunge na Umma wa Watanzania kwa makusudi kuhusu faida za miradi ya EPC+F na akituita baadhi ya wabunge tuliohoji Mikataba hii kuwa ni wapotoshaji na tuna nia mbaya.
Nchi yetu imejenga mtandao mkubwa wa barabara za lami na madaraja makubwa na madogo kwa utaratibu wa kawaida wa kutangaza na kuajiri wakandarasi kwa kutumia fedha zetu za ndani na mikopo kutoka nje. Leo Serikali imesukumwa na nini kwa siku 1 kusaini mikataba ya ujenzi wa Kilomita 2035 kwa mara
moja yenye thamani Tsh. Trilioni 3.75 tena kwa kutegemea mikopo kutoka nje.
Pia Waziri Mbarawa siku ya kusaini Mikataba hii alikiri kwamba hata alipowashirikisha TANROADS kwa hatua za awali walipinga utaratibu wa EPC+F lakini yeye akatumia madaraka yake kulazimisha kusainiwa mikataba hiyo.
Serikali imetumia gharama kubwa kuandaa miradi hewa na kupeleka ahadi hewa kwa wananchi wa maeneo yaliyotajwa na mbaya zaidi wananchi wa mikoa inayopitiwa na miradi 7 ya barabara wameondolewa kwenye mipango na bajeti ya mwaka 2023/2024 na 2024/2025 kwa kuwa barabara zao zitajengwa kupitia utaratibu wa EPC+F.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inakiri kwamba hakuna kinachoendelea katika miradi ya EPC+F, Hotuba ya Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa katika Ibara ya 40 ukurasa wa 36 anakiri kuwa miradi hiyo haina chanzo cha fedha na bado haijaanza na kwamba Serikali inaendelea na mazungumzo na wafadhili ili kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo. Miradi tuliyoambiwa ina ufadhili wa moja kwa moja yaani mkandarasi anayejenga atatumia fedha zake na baadaye kuidai Serikali, leo tunaambiwa anatafutwa mfadhili wa kugharamia miradi hiyo. Hii inaleta sintofahamu na mkanganyiko mkubwa.
Waziri Profesa Mbarawa ameichonganisha Serikali na Mheshimiwa Rais mbele ya wananchi, amekichonganisha Chama cha Mapinduzi na wananchi kwa ahadi hewa ya ujenzi wa barabara kilomita 2,035, Na kwa kuwa, kuna dalili na harufu ya Rushwa vyombo vya uchunguzi TAKUKURU, DCI na DPP wachukue hatua kwa Prof Mbarawa na wote waliohusika kwenye kashfa hii, kwa
makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi na kwa mujibu wa Kifungu cha 27 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008.
Nashauri Mikataba yote ya EPC+F ivunjwe na miradi hiyo ifutwe kwenye vitabu vya Serikali. Pia bajeti ya Wizara ya Ujenzi ya mwaka 2024/2025 irudishwe na ifumuliwe upya ili kuwezesha majimbo, wilaya na mikoa iliyokuwa imeingizwa kwenye miradi hewa ya EPC+F ipangiwe upya fedha katika bajeti ya mwaka 2024/2025.
Miradi ya Barabara na Madaraja ya PPP
Maelezo yaliyotolewa katika Hotuba ya Waziri katika Ibara ya 215 ya Hotuba kuhusu utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara (Express Way) kwa utaratibu wa PPP ni maelezo hayo hayo yaliyotolewa mwaka jana na Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa Waziri wa Ujenzi ambapo iliahidiwa kuwa mikataba ingekuwa imesainiwa kufikia Juni 2023 na kuanza ujenzi.Tumekuwa tukihoji sana suala hili hapa Bungeni lakini hatupati majibu kutoka serikalini, binafsi nimehoji kwa kusema na kwa michango ya maandishi ya mara kwa mara bila majibu, Serikali inawezaje kuanzisha mchakato unaohusu kutwaa au kutumia ardhi ya umma bila kibali cha Bunge, Hifadhi ya Barabara tuliyonayo ni mali ya umma kwa matumizi ya umma, Wizara ya Ujenzi haina mamlaka ya kukabidhi maeneo ya hifadhi za barabara kwa mwekezaji wa sekta binafsi bila kibali cha Bunge.
Kuna mkanganyiko mkubwa wa mipango ya Serikali na pengine huoni kama kuna nia njema kwani huwezi kuja na mradi wa ujenzi wa barabara ya kulipia kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro- Dodoma (Express Way) yenye urefu wa Km 531.8 kwa utaratibu wa PPP. Huku kuna mradi mkubwa wa SGR ambao uko hatua za
mwisho kukamilika na utaanza kutoa huduma Julai 2024. Mradi huu unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari barabarani kwa zaidi ya 60%. Hii ni mipango Mibovu na matumizi mabaya ya raslimali za umma.
Uzoefu unaonyesha kuwa nchi zilizojenga barabara za kulipia huacha kwa makusudi kukarabati njia Mbadala ili wananchi walazimike kupita katika barabara za kulipia. Lakini pia Makampuni ya ubia yamekuwa yakiweka bei kubwa za tozo na kusababisha gharama za usafiri na usafirishaji kuwa juu na hivyo kuchochea mfumko wa bei za bidhaa na ugumu wa maisha. Kama nchi tumejipangaje kabla ya kuiendea miradi ya namna hii. Ikumbukwe kuwa barabara hii inatoka kwenye lango kuu la uchumi wa nchi yetu yaani Bandari ya Dar es Salaam kwenda kwenye mikoa na mataifa mbalimbali ya nchi jirani.
Mchakato unaoendelea wa kumpata mkandarasi ni kinyume cha Sheria ya Ardhi na Sheria ya Raslimali inayotaka hatua zote kuwa wazi na Bunge kujulishwa. Leo Waziri atuambie ukweli juu ya faida ya mradi huu. Nchi yetu imejenga na imeunganisha mikoa yote kwa barabara za kiwango cha lami, tumejenga mtandao mkubwa wa SGR leo hatuna fedha za kujenga njia nne kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro hadi Dodoma? Au kuna jambo lililojificha nyuma ya pazia kwenye miradi hii ya PPP.
Tulishaanza safari ya upanuzi wa barabara ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo ujenzi wa barabara wa njia 8 umeshakamilika kutoka Kimara hadi Kibaha na hivyo tunaweza kuendelea kutenga bajeti kwa awamu hadi Chalinze na baadaye Morogoro na Dodoma ikizingatiwa kuwa miradi mingi ya kimkakati iliyokuwa inachukua fedha nyingi inakamilika ya Bwawa la Nyerere, Daraja la JPM (Kigongo Busisi), SGR.
Tume ya Mipango iko wapi hadi mipango mibovu kama hii kuendelea kwenye nchi.
Miradi mingine inayoanishwa kutekelezwa kwa njia ya PPP haina tija na inaweza kusababisha hasara kubwa mfano Daraja la Pili la Kigamboni (Magogoni-Kivukoni) daraja hili linapendekezwa kujengwa wakati tunalo Daraja la Nyerere (Kigamboni) lilojengwa na Mfuko wa NSSF hivyo kujengwa daraja lingine la kulipia litaua biashara ya Daraja lililopo na kushindwa kurejesha mtaji wa uwekezaji wa shirika hilo. Lakini pia eneo linalopendekezwa kujengwa daraja la pili kuingilia Meli katika Bandari ya Dar es Salaam.
Nashauri Serikali ifute michakato inayoendelea wa kutafuta mkandarasi wa kujenga mradi wa barabara ya kulipia kutoka Kibaha hadi Dodoma kwa utaratibu wa PPP na badala yake ifanye tathmini upya kubaini maeneo na miradi yenye faida Kiuchumi kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP.
HITIMISHO
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa anashauriwa kuwa makini katika uandaaji wa bajeti na kuepuka kurudia miradi iliyokwishatekelezwa miaka ya nyuma, kutokuorodhesha miradi ambayo haina kasma ya fedha na kujiepusha kuanzisha miradi isiyo na tija kwa taifa.Ni jambo la kushangaza kuona udhaifu wa usimamizi wa Mikataba na mipango mibovu kiasi hiki wakati tuna Tume ya Mipango, Wizara inayotekeleza miradi mikubwa ya madaraja, barabara za lami na changarawe, viwanja vya ndege na vivuko kutengewa fedha ndogo kiasi cha Tsh. Trilioni 1.6 tu huku miradi mingi ya