Mchango wa mawazo

Mchango wa mawazo

Dodo18

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2011
Posts
315
Reaction score
93
Salaam Wapendwa wangu,,....!!
Poleni kwa majukum na mikiki mikiki ya hapa na
pale katika jitihada za kutafuta rizki,,...!!
Sina mengi ila nahitaji ushauri wenu wenye
busara,,....!! Kwa kiufupi tu, tumeuza nyumba ya marehem mama yetu iliopo kariakoo aliekua akimiliki na ndungu zake wawili ambao pia wamefariki kwa kiasi cha tsh750 million hivi karibuni na kuigawanya kwa mafungu matatu yaani kila mtoto anarithi tumbo la mzazi wake kwahyo mimi na mdogo wangu tukapata 250 ya mama yetu na wengine wakapata share ya wazazi wao.. Sasa naomba mnishauri biashara gani ambayo itamudu kiasi cha hiyo pesa na kutuingizia faida mimi na mdogo wangu? Sina uzoefu sana wa biashara...
 
Ni PM nikupe mchakato mzuri wa kufaya....!!

Ogopa kuingia ubia
 
Kuwa makini na matapel, kuna haja gani ya PM wakati ushauri unaweza tolewa hapahapa na watu wote wakanufaika?
 
Nenda kwa wataalam wa biashara, utapata ushauri mzuri. Hapa pia wapo ila changanya na zako, usikurupuke.
 
kwanza mna umri gan pili mnafanya kaz au la tatu mna elim gan na mwisho mna ujuz au fani yoyote. Baada ya hapo ndo nitakushauri vizur kadir nitakavyojaaliwa.
 
Nina miaka 27 na bado sijafanikiwa kupata kazi ya kudumu, ila mdogo wangu ana miaka 24 na anafanya kazi kwenye kampuni ya ki-swedish inaitwa oriflame iko potsa, she's a receptionist..
 
I'm an a- level graduate na mdogo wangu kamaliza form 4
 
hahahah kama ni kweli basi ujue matapeli na Majambazi wameshaipigia hesabu kama yao!
 
Last edited by a moderator:
Nina miaka 27 na bado sijafanikiwa kupata kazi ya kudumu, ila mdogo wangu ana miaka 24 na anafanya kazi kwenye kampuni ya ki-swedish inaitwa oriflame iko potsa, she's a receptionist..

mnayo nyumba nyingine ya kukaa au iyo pesa ndo kila kitu?
 
weka fixed account wakati unafanya uchunguzi ujue biashara gani utafanya vinginevyo hiyo pesa itapotea kiajabu
 
hatuna nyumba ya kwetu kabisa tunaishi kwa shangazi yetu sinza yaani hii hela ndio kila kitu kwa mi na mdogo wangu maana bahati kama hii haiji mara mbili
 
I'm an a- level graduate na mdogo wangu kamaliza form 4

Sawa, kwa iyo hauna fani yoyote zaidi ya form 6 na mdogo wako form 4. Unaweza ukanunua nyumba 2 zisizozidi milion 50 had 60 kila moja kisha mkawa mnapata kodi ambayo ni laki 3 had 4 kwa mwez kwa kila nyumba, na au ukanunua bajaji 2 au bajaji moja na suzuki carry moja na kila siku ukawa unaletewa elf 30 had elf 40 kwa siku. Pia unaweza ukanunua hisa salama ambazo zina interest ya 10-12% kwa mwaka ukilinganisha na fixed deposit ambayo unapata 3-6% kwa mwaka. Au pia unaweza ukaja mkoani kama huku kilombero kisha ukanunua matrekta mawili mapya na ukaanza kuwalimishia wakulima mashamba yao na kila heka ni elf 45 had elf 50. Kiufupi ni kuwa tumia nusu ya hiyo hela kuinvest na nusu (mil 125) uiweke akiba lakini kwa kuiweka fixed deposit au kununua hisa kutoka kwenye kampun imara kama nmb,twiga cement, tcc, tbl, N.k waweza ni pm ukitaka tuongee vzur kwan mimi ni bussiness consultant na pia ni mtaalam wa mambo ya biashara.
 
Kijana biashara inaweza kukutia hasara coz hazitabiriki,tafuta kiwanja cha bei rahisi jenga nyumba mtakayoishi na ndugu yako then kiasi kilichobaki ndo ufanyie biashara onyo ucwekeze pesa yote kwny biashara
 
Usifanye haraka kujitosa kwenye biashara !! huko kuna maPapa watakumeza kijana !! tuliza mawazo, usifanye papara !!

chukuwa ushauri wa maana hapo kwanza. pili haraka ufungue account benki. ukaziweke benki hakuna kutoa Ovyo ovyo....!kayimukaa
 
kabla ya yote, tafadhari mkuu naomba unikopeshe angalau mil 1
baada ya mwezi nitakurudishia mil 1 na nusu!
 
jenga nyumba za gharama nafuu sehemu tofauti tofauti.
 
Kitu cha kwanza tulichokifikiria ni nyumba ila bei za nyumba nazo zinatisha na sitaki hela yote iende kwenye nyumba nataka mi na mdogo wangu tuwe na maisha mazuri kutokana na hii hela
 
Back
Top Bottom