Mchango wa Mbunge Shabiby kuhusu vigogo wanaokwamisha viwanda vya dawa kujengwa nchini, wananchi wamuunga mkono, watoa neno

Mchango wa Mbunge Shabiby kuhusu vigogo wanaokwamisha viwanda vya dawa kujengwa nchini, wananchi wamuunga mkono, watoa neno

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Mbunge wa Gairo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mheshimiwa Ahmed Shabiby amesema anaweza kuwataja vigogo wanaokwamisha viwanda vya dawa za binadamu kujengwa Tanzania huku akiwaita ni wachawi.

Akichangia Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2026-2027 iliyosomwa bungeni jana Mei 12, 2026 na waziri mwenye dhamana ya Afya, mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, Shabiby alianza kwa kusema kuwa, dawa nyingi zonazoingizwa nchini ni feki na alifanya utafiti.

Alitolea mfano kuwa, kuna dawa zimeandikwa ujazo wa miligramu 500 lakini usahihi ni miligramu 250 jambo ambalo ni kosa.

Alitoa mfano wa dawa aina ya Magnesium ambapo alisema akiwa nje ya nchi, aliwahi kwenda kununua dawa hiyo ambayo alikuwa ameshika 'sampo' aliyotoka nayo nchini, muuzaji akamwambia dawa hizo zimepigwa marufuku kuuzwa nchini humo na kama atakuwa tayari apewe boksi zima bure.

Aidha, alisema kuwa, baadhi ya dawa zinazoingizwa nchini Tanzania siyo zinazouzwa kwenye nchi zinazotengenezwa dawa hizo akimaanisha kuwa, zinazoingizwa nchini zina ubora mdogo kuliko zile zinazouzwa kwenye nchi husika.

Mheshimiwa Shabiby aliendelea kuweka wazi kuwa, endapo viwanda vya dawa vitajengwa nchini kama Bajeti ilivyosomwa, itakuwa rahisi kuwawajibisha wamiliki wake kama watatengeneza dawa zilizokosa ubora.
Alitoa mfano wakati wa Ugonjwa wa Covid 19 ambao ulitikisa dunia mwaka 2019-2021, kwamba kuna sindano za chanjo ziliingizwa nchini kutoka nje huku zikikosa mapokezi kutoka kwa wananchi kwa sababu wengine walidai wanaume wakichomwa wanapungukiwa na nguvu za kiume, wanawake wakichomwa hawazai.
Mheshimiwa Shabiby akasema kuwa, kuna vigogo 'mapapa' ambao wamekuwa wakikwamisha ujenzi wa viwanda vya dawa nchini kwa makusudi na kwa maslahi yao wenyewe.

Akasema: "Na safari hii nikimwona mtu anakwamisha mpango huu (wa kujenga viwanda vya madawa nchini) nitatafuta majina na nitayaleta hapa. Bora niitwe kamati ya maadili kujieleza."

Akasema atawataja watu hao wanaokwamisha sababu ni sawa na wachawi wa nchi hii.
Mheshimiwa Shabiby alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, vita ya kupambana na watu hao ni sawa na mapambano ya madawa ya kulevya. Watu hawataki viwanda vya madawa vijengwe nchini Tanzania.
Hata hivyo, mwisho wa hotuba ya mchango wake, mbunge huyo aliunga mkono hoja ya wizara huku akimwambia waziri Mchengerwa, wabunge wako na yeye.

Sasa baadhi ya wananchi waliyomsikiliza mbunge huyo, wamemuunga mkono wakisema kuwa, Watanzania wengi 'wanateketea' kwa dawa zisizo na ubora na zilizokwisha wakati wake hasa zile ambazo zinatoka nje ya nchi.

Mfamasia kutoka Duka la Dawa lililopo Tegeta-Kibo, Kinondoni, Dar es Salaam, Anna Kimbu alisema anamuunga mkono mheshimiwa Shabiby kuwepo kwa 'watu wazito' kwenye nchi ambao wamekuwa wakikwamisha ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili wao waendelee kuwa waaguzaji wakubwa wa dawa kutoka nje ya nchi huku dawa hizo zingine zikiwa feki kabisa.

"Mtu anajua viwanda vikijengwa nchini dili lake la kuwa muagizaji dawa litakufa. Kwa hiyo anafanya juu chini kuhakikisha viwanda havijengwi. Lakini kama alivyoongea Shabiby, wabunge wapya wengi hawana njaa ya vijisenti," alisema mfamasia huyo.

"Nilimsikia mheshimiwa Shabiby akisema kuwa, kuna dawa ambazo ujazo wa kwenye maboksi siyo ujazo wa dawa zenyewe. Sasa hii si hatari jamani! Namuungamkono Shabiby kama alivyounga mkono Wizara ya Afya kwamba, viwanda vya madawa vijengwe kwa wingi nchini itakuwa rahisi kufuatilia ubora wake," alisema Stella Mfungalo, mkazi wa Ilala-Dar es Salaam.

Erasto Mikidadi mkazi wa Kawe Ukwamani, Dar es Salaam yeye alisema anaunga mkono Wizara ya Afya kujenga viwanda vya dawa nchini kwa kuwa kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imelinda afya za wananchi wao.
"Dawa ni kitu sensitive (nyeti) sana. Kwa hiyo nchi kutegemea dawa za kutoka nje ya nchi ni hatari kwa sababu ziko nchi zinaangalia pesa badala ya kuangalia afya za raia wake," alisema Erasto.
Wakati huohuo, akiongea mjini Nairobi, Kenya, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba amesema serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaokwamisha ujenzi wa viwanda vya dawa nchini.
Screenshot_20260513_194732_YouTube.jpg
 
Zaidi ya sheria zilizopo,serikali na maofisa wake nani anaweza kuzuia visijengwe? usanii mtupu
 
Back
Top Bottom