SoC02 Mchango wa utalii katika maendeleo ya taifa letu. "Tuuthamini basi"

Stories of Change - 2022 Competition

NYANOHA

Member
Joined
Sep 2, 2022
Posts
5
Reaction score
4
MCHANGO WA UTALII KATIKA MAENDLEO YA TAIFA LETU. "TUUTHAMINI BASI"

Utalii una mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa letu la TANZANIA, hivyo basi ni jukumu letu sote kuuthamini utalii huu ili uendelee kuleta tija ndani ya nchi yetu na katika nyanja na idara mbalimbali, kama vile, miundo mbinu, huduma za kijamii, pato la taifa kwa serikali, makapuni binafsi na raia wa kawaida. "tuuthamini basi."

Taifa la Tanzania Lina tegemea utalii kua ndo chanzo chake kikubwa Cha uchumi kutoka serikali hadi kwa raia mmoja mmoja, si dhambi kusema kua %65 ya kipato cha watanzania kinategea utalii kwa namna moja au nyengine. "tuuthamini basi."

serikali inapwaswa kuelekeza juhudi zake nyingi kuhakikisha utalii unaendelea kukua kwa kasi ya 4G, hapo ulipo fika usirudi nyuma badala yake uende mbele zaidi ili tuweze kuwapita wapinzani wetu na tuwache mbali sana mpaka wakate tamma ya kushindana na sisi. "tuuthamini basi."


SABABU ZINAZO WAFANYA WATALII WAPENDELEE KUJA TANZANIA

Watalii wanapendelea sana kuja kutembea tanzazia kwa sababu tofauti, kuna vitu vingi ambavyo huwavutia watalii kote duniani kuja nchini kwtu, vitu hvyo ni kama vifuatavyo.
⦁ usalama uliopo nchini
⦁ vivutio vilivyopo nchini
⦁ ukarimu,uaminifu na upendo tuliokua nao watanzania
⦁ na uwepo wa nyumba za wageni zenye hadhi ya kuwapokea watalii wa aina zote kulingana na hali zao za kiuchumi.
hebu sasa tuangalie hizis ababu moja baada ya nyengne zinawashawishi vpi watalii kupendelea kuja taznzainia kwa wingi kuliko nchi nyengine hapa barani africa.


USALAMA ULIOPO TANZANIA. Usalama ndo sababu kuu ya watalii mbalimbali duniani kuichagua tanzania kama ni sehem salama ya wao kuja kutembea ukizingatia kila binadamu anaangalia usalama wake kwanza kabla ya kufanya jambo lolote, Tanzania ni nchi ya amani, unatembea sehem yoyote bila ya kua na hofu juu ya kitu chochote kinacho weza kuleta madhara kwa binadam, tuipongeze serikali yetu kwa juhusi mbali mbali inazozichukua kuhakikisha usalam unakuwepo kila kona ya nchi."


UKARIMU, UAMINIFU NA UPENDO TULIOKUA NAO WATANZANIA. Ukarimu, uaminifu na upendo tuliokua nao watanzia ni kivutio chengine kinacho wafanya watalii kuja kutembea nchini kwetu kwani wakifika hapa sisi tunawakarimu na tunawapenda kama ni ndugu zetu wa damu, pia tuna sifa moja ambayo ni adimu kupatikna sehem chengine ambayo ni uaminifu, watanzia ni waaminifu sana, utaacha kitu chako sehem ya wazi na utakikuta kama ulivo kuweka, ukidondosha kitu unarudishiwa mwenyewe, hatuna sifa za wizi, nk."

VIVUTIO VILIVYOPO TANZANIA. Tanzainia ni nchi iliyojaaliwa na vivutio vingi sana vya utalii ambavyo vime wafanya watalii kutoka sehem mbalimbali duniani kuja tanzainia ili wavione kwa macho yao wenyewe, vivuyio kama vile, mbuga za wanyama, mlima wa kilimanjaro, makumbusho ya kale, mashamba ya viungo na amtunda, mapango ya kale, visiwa vidogovidogo, miji ya kihisitoria, nk."


UWEPO WA NYAMBA ZA WAGENI ZENYE HADHI TOFAUTI YA KUWAPOKEA WAGEINI KULINGANA NA HALI ZAO ZA KIUCHUMI. Tanzania tumejaaliwa kwa kua na nyumba za wageni zinazo weza kuwapokea wageni tofauti kulingana na hali zao za kiuchumi haijaalishi tajiri wala masikini, watalii wa matabaka yote wanaweza kupata sehem ya kulala nchini kwa kuzingitia kipato chao, kuna baadhi ya nchi zinapokea wageni wenye hali nzur kichumi tu.


NI VIPI UTALII UMECHANGIA MAENDELO YETU

Utalii umechangia maendeleo ya ya taifa letu katika nyanja tofauti, na ni sababu ya taswira nzuri ya nchi yetu kijiograghia yaani kimuonekano, tuangalie kwa uchache tu maendeleo hayo yaliyoletwa na utalii. "tuuthamini basi."

BARABARA ZA KISASA ZA KIWANGO CHA LAMI. Moja ya kipaumbele cha wawezekaji kuja ni sharti nchi iwe na barabara za kisasa ambazo zinarahisisha usafiri, na kwa sasa tukiangalia katika nchi, miji yote imezunguukwa na barabara nzur zenye kuvutia, hayo yote nikwa sababu ya utalii. "tuuthamini basi."

VIWANJA VYA NDEGE. Utalii ni sababu kubwa ya kujengwa kwa viwanja vya ndege vya kisasa na vyenye uwezo wa kuhimili ndege kubwa kutua nchini, ili wawekezaji na watalii waweze kuja nchini ni lazima tuwe na viwanja vya ndege, kwani hii ndio njia kuu ya usafir katika dunia ya sasa. "tuuthamini basi."

HUDUMA ZA KIJAMII. Utalii umechangia kiasi kikubwa katika kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa haraka na urahisi hudma kama vile umeme, maji safi na salama, usafiri, huduma za afya na misaada mbali mbali kwa walengwa wa aina tofauti, nk. "tuuthamin basi".

PATO LA TAIFA. Utalii umechangia kwa kiasi kikubwa pato lataifu kukua kwani serikali inakusanya kiwango kikubwa cha mapoto kwa wawekezaji, watalii, makampuni yanayo jishughulisha na utalii na raia wanaofanya shughuli mbalimbali za kitalii katika kutoa kuduma kwa watalii. "tuuthamini basi."

AJIRA NCHINI. utalii umechangia kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza nafasi nyingi za ajira hapa nchini hali iliyopelekea kupunguza mzigo kwa serikali juu ya suali la uhaba wa ajira kwa raia. mfano, kuna walio ajiriwa na kuna walio jiajiri.

WALIO AJIRIWA. Secta ya utalii imechangia asilimia kubwa katika kutengeneza ajira kwa vijana wa kitanzania, vijana wengi wameajiriawa katika Secta ya utalii, sehem ambazo vijana wameajiriwa ni kama zifuatazo.
⦁ MAHOTELINI
⦁ MIGAHAWANI
⦁ KITE SURFING
⦁ TOUR GUIDING COMPANY
⦁ SUPPLYING COMPANY
⦁ WASTE MANAGEMENT COMPANY
⦁ INTERNET SERVICES PROVIDERS COMPANY
⦁ CONSTRUCTION COMPANY
⦁ SECURITY GUARD COMPANY
⦁ DIVING COMPANY

WALIOJIAJIRI. kuna kundi kubwa la vijana ambao wamejiajiri wenyewe katika Secta hii ya utalii kwa maana Hawa hawajaajiria na kampuni yoyote, ispokua wameamua kufanya baadhi ya shughuli za kitalii kwa kujisimamia wenyewe bila ya kutegemea kwa upande wowote, tuangalie vijana Hawa wamejiajiri kivipi.

Vijana hawa wamejiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile kuuza madafu na matunda kwa watalii, kufanya shughuli za upapasi na usafiri, kufungua local restaurants, kubadilisha pesa za kigeni kwa shilingi kwa rate ndogo na kwenda kuuza bank kwa rate kubwa, nk. "tuuthamini basi."

Kwa kuhitimisha naomba nitoe wito kwa serikali, makampuni binafsi na ya serikali, raia, na wawekezaji kwa ujumla kuuthamini utalii, utalii ni roho ya uchumi wa nchi hii hivyo ni jukumu letu kilinda roho hii kwa hali na mali ili iendelee kuishi kwa afya njema, iweze kutuletea yale mazuri yaliyokusudiwa. "tuuthamini basi."

BY NYANOHA.
 
Upvote 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…