leta mawazo mapya,sio wote tugombee kufanya wakala wa m-pesa...maana ndio biashara mnayoadvise kila siku....:wacko:
Hiyo pesa yako iweke kwanza mpaka utakapopata au utakapojua nini majibu ya haya maswali:
1. Biashara gani ambayo una uwezo wa kuifanya (hapa tunamaanisha capacity)
2. Eneo gani unataka kuifanyia hiyo biashara-je wateja wanapatikana sehemu hiyo? na banda la kufanyia biashara, gharama ya banda?
3. Soko la hiyo bidhaa ikoje? nina maana ya je ina soko mwaka mzima au kwa kipindi fulani tu.
4. Bidhaa utakazouza zitapatikanaje?
5. Je mzunguko wa pesa katika eneo hilo ukoje?
6. Je wateja wako ni kundi gani au ni watu wa aina gani?
7. Mtaji wa biashara huo ni kiasi gani?
8. Je unataka kufanya biashara mwenyewe au kuna mtu au watu utawaajiri ili wakusaidie, kama ndivyo je ni watu wa aina gani na nini gharama zao?
9. Je hiyo biashara itahitaji kiasi gani, na unategemea kuuza kiasi gani kwa siku au kwa mwezi? na je unategmea baada ya muda gani mtaji wako ulioweka kwenye biashara iweze kurudi?
10. N.K
Kama hauwezi kujibu hayo maswali au 80 asilimia ya hayo maswali vizuri, basi hiyo pesa yako nakushauri ukatafute kiwanja eneo zuri ukanunue na mara utakapokuwa tayari unajua biashara gani ya kufanya, ndipo ukauze hicho kiwanja ili hiyo pesa utumie kwenye hiyo biashara. Kiwanja ununue sehemu ambayo ni potential ili utakapohitaji kuuza usipate shida.
Onyo.
Kamwe usipoteze pesa zako kwa kutafuta akuandalie business plan kabla hujajua bado ni aina gani ya biashara una uwezo wa kuufanya. Kama unahitaji sehemu ya kwenda kujenga capacity kwanza ili ukimaliza uweze kujua nini biashara gani unaweza kufanya. Na naamini baada ya muda mfupi sana,tena masaa 3 kwa siku ya jmosi na jpili tu na ndani ya miezi 3 tayari utakuwa na uwezo wa kujua ni biashara gani una uwezo wa kufanya. Usihofu gharama, kwani katika kipindi hicho gharama haizidi 300,000(laki tatu tu).
unaweza uni pm au tuwasiliane kwa lindinachingwea@gmail.com
Wewe kweli ni punguwani, hizo thread zote zina zungumzia M-PESA TU? Kwani huwezi kuwa na mawazo yako mwenyewe? Hizi hudumu Nchi nyingine ni pesa, tusipende vya bure sana,
Huko uliko kuna kampuni za Consultancy wafuate na uwape pesa wakushauri nini cha kufanya, Na by the way hutapata michango yoyote ya maana make watu walisha choka na marudio rudio ya vitu vile vile,
wakuu nina milioni kumi,najiuliza nifungue biashara sijui biashara gani hapa mtaniadvise au niweke msingi kny kiwanja changu kule kibaha tatizo nikiweka msingi sijui nitamaliza lini kujenga as sina uhakika/regular income na b, nikianza biashara ni biashara gani itakayonirudishia hela yangu ili niweze kujenga? msaada kny tutazzz.....:israel:
asante kwa hili wazo mkuu,ubarikiwe...nimelipenda..will definately work on it....
MISSION IMPOSSIBLE IDEA:
1 - Tafuta frem moja ya biashara kisha lipia na uikarabati katika muonekano wa kiofisi ya kisasa.(weka mlango wa alluminium, air condition, meza, kiti, viti 2 vya wageni, kompyuta, printer, shelf / kabati nk ila usiweke tangazo lolote)
2 - Watangazie watu waaminifu unaowafahamu (ambao wana uwezo wa kuingiza hela kila siku na walio na shughuli nzuri na kubwa zinazowaingizia kipato, mfano wafanyabiashara na wafanyakazi wenye mishahara mizuri) watangazie kuwa unatoa mikopo ya marejesho ya mwezi mmoja kwa riba ya 30%, kuanzia Tsh 100,000 hadi milioni moja.
3- Weka lending policy and procedures ambazo zipo secured na sustainable katika utoaji wa huduma hiyo.
4 -Anza kutoa mikopo kwa mtaji wa kiasi utakachokuwa nacho baada ya process hapo juu. Amini kuwa kama utakuwa serious na kufuatilia ipasavyo, basi baada ya miezi 12 (mwaka 1) tangu ufungue hiyo kijiofisi chako utaweza kupata return nzuri kama ifuatavyo: mfano ukaanza na mtaji wa milioni kumi (working capital)
[TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD]MWEZI
[/TD]
[TD]MTAJI (TSH)
[/TD]
[TD]RETURN (TSH)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]January
[/TD]
[TD]10,000,000
[/TD]
[TD]13,000,000
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]February
[/TD]
[TD]13,000,000
[/TD]
[TD]16,900,000
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]March
[/TD]
[TD]16,900,000
[/TD]
[TD]21,970,000
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]April
[/TD]
[TD]21,970,000
[/TD]
[TD]28,561,000
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]May
[/TD]
[TD]28,561,000
[/TD]
[TD]37,129,300
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]June
[/TD]
[TD]37,129,300
[/TD]
[TD]48,268,090
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]July
[/TD]
[TD]48,268,090
[/TD]
[TD]62,748,517
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]August
[/TD]
[TD]62,748,517
[/TD]
[TD]81,573,072
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]September
[/TD]
[TD]81,573,072
[/TD]
[TD]106,044,994
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]October
[/TD]
[TD]106,044,994
[/TD]
[TD]137,858,492
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]November
[/TD]
[TD]137,858,492
[/TD]
[TD]179,216,040
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]December
[/TD]
[TD]179,216,040
[/TD]
[TD]232,980,851
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hivyo baada ya miezi 12, unaweza kuisajiri biashara yako na kuwa kampuni na kuifanya kuwa ofisi kubwa. Najua kutakuwa na matumizi mfano, kulipa mshahara kama kuna mtu utakuwa umemwajiri, umeme nk. ila gharama zake hazitakuwa kubwa za kuweza kukushinda kulipia kwa kutafuta fedha mbadala kutoka katika vyanzo vingine ili mtaji ubaki vile vile.
Ni wazo tu.
wazo zuri.. but changamoto kubwa iko ktk kufuatilia waliokopa walipe.. na wakati mwingine wengine hushindwa kulipa