Mchecheto wa mafanikio

Mchecheto wa mafanikio

Umenigusa Mkuu.
Ngoja nijipange upya.
 
Daaaaaaah booooonge LA uzi,nimebaki mdomo wazi!!!
Umenigusa Sana, nimekosea maeneo mengi sana na kupoteza pesa nyingi kwa sababu ya Mchecheto tu Wa Mafanikio
Asante Sana Mkuu,Pamoja Sana!!! Ubarikiwe!!!!
 
huu uzi ungepaswa kila mtanzania ausome.lakinikutokana na uvivu wa kusoma wengi wanaokimbilia kuinvest kichwa kichwa watapoteana tu
 
Ukweli siku zote unasimama kuwa ukweli, mkuu umelenga mule mule vijana wengi tunapenda mafanikio ya haraka, Well said and much RESPEK to your thread, atleast nimeambulia kitu kipya.
 
Kwenye maisha kuna kitu huwa kinaitwa mchecheto wa mafanikio.Hii ni ile hali ya kutaka kufanikiwa kwa haraka hasa baada ya kugundua kuwa kama umechelewa,umri umeenda,rafiki zako wanapiga hatua kwa kasi ama ulikuwa hujui mambo ambayo ulipaswa kuyajua kwa muda mrefu sana huko nyuma.Hii hutokea pale ambapo unakutana na watu ambao wakikupa mahesabu ya biashara fulani basi unaanza kujiona tajiri kabla hata haujaanza kuifanya.Matokeo ya hali hii ni kujikuta unajiingiza katika kufanya jambo fulani si kwa sababu moyo wako umeridhika bali kwa sababu uroho wa pesa unakuendesha.

Sababu mbili kubwa zinazowasababisha watu wasifanikiwe katika maisha yao ni;moja ni kujua vitu na huwa na hawafanyi kabisa lakini nyingine ni kujua vitu na kisha kufanya bila kuwa na maarifa ya kutosha.Mara nyingi watu wanaopata mchecheto wa mafanikio huwa wanakumbwa na ugonjwa wa kuanza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja na matokeo yake basi huwa wanajikuta wamefeli katika yote ambayo walikuwa wanafanya.

Utajijua kama wewe upo kwenye kundi hili kwa kuangalia kwa ufupi tangu mwaka huu uanze umeshajiingiza katika kufanya mambo mangapi na yote hayajafanikiwa hata kidogo,tena unafanya yote kwa wakati mmoja.Hakuna mtu ambaye anafanikiwa kwa kutapanya nguvu zake,muda wake na rasilimali zake maalumu hasa unapokuwa unaanza safari ya mafanikio yako.Watu ambao huwa hawazingatii jambo moja la kufanya kwa ubora na uhakika huwa hawafanyi vizuri maishani.

Ni rahisi kwa matajiri wakubwa kama vile Dangote au Bakhresa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na wakafanikiwa kwa sababu kinachofanya wafanikiwe sio kutumia nguvu zao tena bali ni mifumo ambayo wameiimarisha inawasaidia kufanya kazi.Wengi tunapokuwa tunaanza huwa hatuna mifumo ya kutubeba na kutufanikisha,hivyo lazima tutumie rasilimali zetu kwa uangalifu wa hali ya juu.

Kuna watu huwa wakisikia habari za wengine waliofanikiwa basi huwa na mchecheto usio wa kawaida kuhusu mafanikio na matokeo yake hujikuta wanafanya kila kitu.Kuna watu kwa sababu wamesikia kilimo cha matikiti kinalipa tayari wameshakimbilia huko,wengine kwa sababu “green house” zinalipa tayari wamekimbilia kuwekeza,mwingine amesikia bidhaa za forever au trevo yumo nako;Ukifuatilia unakuta hakujiandaa kabisa kimaarifa.Unakuta mtu na mtaji wa milioni moja na anafanya biashara tano;Huu ni upotezaji wa nguvu,muda na pesa.

Kumbuka siku zote mafanikio katika biashara/Kilimo hayatokani na ukubwa wa mtaji wako bali yanatokana na kiwango cha maarifa na uzoefu juu ya kufanya biashara/Kilimo.Kuna watu wengi sana wanaishia katika vilio baada ya kuwekeza pesa nyingi kwa sababu huwa hawazingatii mambo ya msingi na wanajikuta wamenasa katika mtego wa mchecheto wa mafanikio.

Ili Ufanikiwe katika jambo lolote uliloamua kulifanya,ni lazima uzingatie mambo haya mawili:

La kwanza ni kutafuta ujuzi zaidi ya unavyotafuta mtaji.Watu wengi sana huwa wanafeli katika yale wayafanyayo sio kwa sababu hawana pesa za kutosha bali kwa sababu hawana ujuzi wa kutosha.Eti unakuta mstaafu hajawahi kumiliki hata bodaboda amepata milioni mia za mafao anaenda kununua daladala na anasimamia mwenyewe;Huyu kwanza ataugua ugonjwa wa moyo kisha atafeli tu,kwa sababu hana ujuzi.Au unakuta mtu hajawahi hata kuuza vocha anaenda kuchukua mkopo anaanzisha duka la jumla,hapo unakaribisha anguko.Kabla haujafanya chochote kile jiulize nina ujuzi?Na hapa sizungumzii ujuzi wa kusimuliwa na wenzako,kuangalia kwenye TV ama kusoma vitabu-Nazungumzia ujuzi wa kufanya kwa vitendo.Kama unataka kunielewa zaidi,kakusanye maprofesa na madokta wanaofundisha ujasiriamali vyuo vikuu halafu waulize wao wanafanya biashara gani utashangaa!!

Ujuzi wa mafanikio unapatikana kwa kufanya kwa vitendo.Usilime miti Iringa kwa meseji na kupiga simu,utachekwa,nenda shambani kawatafute waliotangulia jifunze kisha uweke ratiba ya kwenda mara kwa mara,nunua sehemu yako ya kiasi anza kufanya ukikusanya ujuzi.Kuna maarifa huwezi kuyapata kwa “distance learning”(masomo ya mbali).Unatakiwa uende eneo la tukio.
Jambo la pili ni kuwa kabla haujaruhusu mchecheto wa mafanikio uendeshe maamuzi yako basi jitahidi kupata taarifa za ndani na za uhakika.Mara nyingi taarifa za mafanikio huwa zinatiwa chumvi nyingi sana ili kukufanya uone kuwa ni rahisi sana.Wakitupia picha kwenye facebook an Instagram wanavyokula maisha basi inaonekana jambo rahisi sana;ukipewa makadirio ya pesa utakazopata unaona kesho unaamka tajiri lakini mara nyingi kuna mambo yaliyojificha.Ukikutana na mtu anayefanya biashara ya mtandao(network marketing) ndio utaelewa ninachokuambia;atakuonyesha urahisi wa biashara na mafanikio makubwa lakini bila kukuonyesha changamoto na wengi wamekata tamaa kwa sababu hawakujiandaa kukabiliana na changamoto.

Kama hutaki kukatishwa tamaa na matokeo na changamoto utakazokutana nazo basi jitahidi kujua mapema.Kwenye kila fursa kubwa unayopewa na kuambiwa jiulize:Hivi hapa kuna changamoto gani?Kumbuka siku zote,Hakuna fursa isiyo na changamoto ndani yake,Na kadiri fursa inavyoonekana kubwa basi ujue na changamoto nayo itakuwa kubwa-Jipange kuitatua.Ukiambiwa twende vitani utakuwa mfalme,ujue kuna Goliath wa Kumkabili.

Kabla haujaamua kupiga hatua kuelekea kufanya kitu kipya-Hebu jiulize:Haya ni maamuzi thabiti ama ni mchecheto wa mafanikio.Ulishawahi kufeli kwa sababu ya mchecheto wa mafanikio?unataka kuepuka kufeli?Punguza mchecheto!

Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana.

Nimejifunza kitu hapa tena kikubwa n cha samani sana kuliko mtaji
 
Mkuu umetisha kila kitu umeongea ni ukweli mtupu..Naamini sisi vijana tutajifunza jambo hapo ili tusipate mchecheto wa mafanikio
 
Hii elimu inahitajika sana kwa vijana wengi tunaojaribu kujiongeza kuwa kudaka fursa zilizo mbele yetu. Sishangai kuona wengi wetu tunafanya mambo blindly au kwa kufuata mkumbo tu tukitamani tu kupiga hela! Kama vile tunavyoweka mtaji basi na maarifa ya kutosha ni muhimu sana!
 
Back
Top Bottom