DOKEZO Mchele uliopakwa mafuta na athari kwa afya zetu, Serikali itoe tamko tujue usalama wetu

DOKEZO Mchele uliopakwa mafuta na athari kwa afya zetu, Serikali itoe tamko tujue usalama wetu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Kumeingia wimbi la kuuziwa michele ambayo imepakwa mafuta hasa Dar es saalaam na Pwani, Je serikali kupitia wizara na taasisi zao hawajaliona hili?

Je, ni mafuta gani hayo yanapakwa kwenye mchele ikiwa na lengo la kuufanya uonekane mzuri je, ni mafuta ya aina gani?

Tunashuhudia kansa kuongezeka nchini kila kukicha je hawa wa mchele hawasababishi hili?

Tunaomba majibu ya kina ili tujue hatima ya afya zetu.
 
Kuna mtaalamu wa lishe humu JF aliwahi kusema kuwa hiyo ni njia ya kuuhifadhi mi nikamuelewa maelezo yake.

Watz sio kila kitu ni kupigwa.

Anyway fanya utafiti mdogo wa madhara ya kupaka mchele mafuta ya kula utuletee, vinginevyo.
 
Kuna Report ya Utafiti KUHUSU mchele wa MBEYA au basi.....yaishe!!
 
Kuna mtaalamu wa lishe humu JF aliwahi kusema kuwa hiyo ni njia ya kuuhifadhi mi nikamuelewa maelezo yake.

Watz sio kila kitu ni kupigwa.

Anyway fanya utafiti mdogo wa madhara ya kupaka mchele mafuta ya kula utuletee, vinginevyo.
Siyo kweli, hilo ni changa la macho, nunuwa peleka kwenye sherehe ambayo unapikwa wali mwingi au pilau kama watu hawajaondoka bila kula.
 
Kuna mchele kutoka Tanzania tani za kutosha pia ulikataliwa NCHI fulani wakati wa tukio KUBWA, sio Waziri wala Serikali waliwahi kutoa tamko kuhusu hili. Wacha tuendelee kumsifia....
 
Mchele huwa unapakwa mafuta ya kupikia, huwa inasaidia wadudu hawaingii na unakaa muda mrefu zaidi.
Siyo kweli, hujui ukweli halisi kwa nini wanapaka mafuta, fuatilia wanaouza samaki wakavu wa kwenye mabwawa wao ndio wako na brush kabisa kama shoshiner vile.
 
Kumeingia wimbi la kuuziwa michele ambayo imepakwa mafuta hasa Dar es saalaam na Pwani, Je serikali kupitia wizara na taasisi zao hawajaliona hili? Je ni mafuta gani hayo yanapakwa kwenye mchele ikiwa na lengo la kuufanya uonekane mzuri je ni mafuta ya aina gani?

Tunashuhudia kansa kuongezeka nchini kila kukicha je hawa wa mchele hawasababishi hili?

Tunaomba majibu ya kina ili tujue hatima ya afya zetu
Una umri gani?
Ndo unalijua hilo leo?
Michele inapakwa mafuta ya kolie,ili isivubae/kuharibika/kuharibiwa na wadudu haraka, ndo maana ukienda dukani unaona inang'aa ata ukikaa muda mrefu,hakuna mchele unaenda sokoni bila kupakwa wese baada ya kukobolewa
 
Kumeingia wimbi la kuuziwa michele ambayo imepakwa mafuta hasa Dar es saalaam na Pwani, Je serikali kupitia wizara na taasisi zao hawajaliona hili?

Je, ni mafuta gani hayo yanapakwa kwenye mchele ikiwa na lengo la kuufanya uonekane mzuri je, ni mafuta ya aina gani?

Tunashuhudia kansa kuongezeka nchini kila kukicha je hawa wa mchele hawasababishi hili?

Tunaomba majibu ya kina ili tujue hatima ya afya zetu
Mhh hatari sana imefikia huko!
 
Siyo kweli, hilo ni changa la macho, nunuwa peleka kwenye sherehe ambayo unapikwa wali mwingi au pilau kama watu hawajaondoka bila kula.
Mkuu sio kila kitu unapinga bila sababu ya msingi. Mchele unapotoka kiwandani kabla kupakiwa kwenye mifuko wanapaka mafuta kama njia ya kuuhifadhi usiharibike na kuvamiwa na wadudu hatarishi. Hii inafanyika kwa muda mrefu sana labda kama hamkua mnajua. Tembelea viwanda utashuhudia haya na watakupa elimu zaidi nini wanakifanya
 
Kumeingia wimbi la kuuziwa michele ambayo imepakwa mafuta hasa Dar es saalaam na Pwani, Je serikali kupitia wizara na taasisi zao hawajaliona hili?

Je, ni mafuta gani hayo yanapakwa kwenye mchele ikiwa na lengo la kuufanya uonekane mzuri je, ni mafuta ya aina gani?

Tunashuhudia kansa kuongezeka nchini kila kukicha je hawa wa mchele hawasababishi hili?

Tunaomba majibu ya kina ili tujue hatima ya afya zetu
Wala usiwe na shaka ni mafuta haya haya ya kula, ndiyo nayotumika, kama soko la CONGO DR, bila na kuongeza kitunguu, utauza mchele wako kwa tabu sana, hata kama umenyooka kama ule wa biriani, lakini haunukii,!!! Ushaharibuuu!!
 
Mimi nadhani ni kusaidia kupunguza kiwango cha mafuta wakati wa kupika maan mchele wenyewe unakuja tayari una mafuta. Na Uchumi ulivyo mgumu wao wazidi tu kumwaga mengi ili kutusaidia bajeti ya kununua mafuta wakati wa kupika 😂😂
 
Kumeingia wimbi la kuuziwa michele ambayo imepakwa mafuta hasa Dar es saalaam na Pwani, Je serikali kupitia wizara na taasisi zao hawajaliona hili?

Je, ni mafuta gani hayo yanapakwa kwenye mchele ikiwa na lengo la kuufanya uonekane mzuri je, ni mafuta ya aina gani?

Tunashuhudia kansa kuongezeka nchini kila kukicha je hawa wa mchele hawasababishi hili?

Tunaomba majibu ya kina ili tujue hatima ya afya zetu
Hilo limeanza muda mrefu sanaaa
 
Siyo kweli, hilo ni changa la macho, nunuwa peleka kwenye sherehe ambayo unapikwa wali mwingi au pilau kama watu hawajaondoka bila kula.
Ushawahi kuuza mchele?

Yale ni mafuta ya kawaida kabisa ya kula, hayana madhara ikiwa utakula mchele uliopikwa. Labda utafune mchele mbichi.

Na mchele huwa unapauka na yale mafuta yanayopakwa hayaathiri ubora wa mchele.
Mchele mbaya ni ule uliokatika katika, huo hata kwa macho tu unaukataa, unaweza kupakwa mafuta na umenyooka ukawa vizuri na unaweza usipakwe mafuta ukang'aa wenyewe na ukawa mbaya.
 
Mkuu sio kila kitu unap8nga bila sababu ya msingi. Mchele unapotoka kiwandani kabla kupakiwa kwenye mifuko wanapaka mafuta kama njia ya kuuhifadhi usiharibike na kuvamiwa na wadudu hatarishi. Hii inafanyika kwa muda mrefu sana labda kama hamkua mnajua. Tembelea viwanda utashuhudia haya na watakupa elimu zaidi nini wanakifanya
Sipingi kila kitu ila ninaona mengi, yuko mtu namjuwa anatumia dawa za kuhifadhia maiti kusafirisha mboro za ng'ombe Kenya kwenye soko lake ambazo zinatumika kama law material.

Nimetembelea Warundi kule nyuma ya breweries ilala mpaka sinywi tena hizi kahawa za wagogo au kwenye vijiwe vya kahawa ingawa niliachaga kutumia muda kwa sababu ya caffeine.
 
Nimefanya sana hiyo kazi ya kupaka mafuta na kimsingi ni hayahaya ya kula na lita Moja unaweza paka gunia hata tatu za mchele ili kuhifadhi dhidi ya wadudu ukienda kuosha unakua kawaida
Nimeishi sehemu wanapolima mpunga Kwa wingi, nimeshuhudia sana Hilo zoezi la kupaka mafuta, ni mafuta ya kupikia.....ugomvi wangu ni namna ya upakaji tu, mchele unamwagwa kwenye turubai, unamwagiwa mafuta kisha unachanganywa Kwa miguu.
Pia kuna kipindi nilikuwa nanunua gunia la mpunga nakoboa lote naweka ndani, usipoweka mafuta wadudu wanashambulia mapema....
Kama kuna lengo lingine sifahamu, si mbaya ukitujuza.
 
Nimefanya sana hiyo kazi ya kupaka mafuta na kimsingi ni hayahaya ya kula na lita Moja unaweza paka gunia hata tatu za mchele ili kuhifadhi dhidi ya wadudu ukienda kuosha unakua kawaida
Nyie ndo mnavuaga na masharti halafu mnapaka mafuta Kwa miguu?🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom