DOKEZO Mchele uliopakwa mafuta na athari kwa afya zetu, Serikali itoe tamko tujue usalama wetu

DOKEZO Mchele uliopakwa mafuta na athari kwa afya zetu, Serikali itoe tamko tujue usalama wetu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
TBS ni takataka tu, usithubutu kunywa hizi kahawa zinazotembezwa ni takataka, kahawa inasagwa pamoja na maharagwe meusi ya burundi ili wapate faida kubwa.
Yale wanaita maharoo. Ndio wauza kahawa wote wanayatumia.ukitaka kuyajua kwanza inakua chubgu balaa na ina harufu mbaya. Roasted coffee ina ladha yake. Hayo mambegu sidhan hata kama tbs wanajua hata kama yapo.wale madogo wa vibirika wanachkua buni robo yale maharage kilo. Kahawa yenye buni halisi harufu yake tu inavutia.ukitaka kuthibitisha njoo grano hapa usikie vyuma
 
Mchele unapotoka kiwandani kabla kupakiwa kwenye mifuko wanapaka mafuta kama njia ya kuuhifadhi usiharibike na kuvamiwa na wadudu hatarishi. Hii inafanyika kwa muda mrefu sana labda kama hamkua mnajua. Tembelea viwanda utashuhudia haya na watakupa elimu zaidi nini wanakifanya
Viwanda hivi, mimi imetembea maeneo ya Tinde na Kahama, hawana wataalamu wowote wa mambo ya afya na chakula. Ni vibarua tu wanaosimamiwa na wafanyabiashara, wasio na elimu bali pesa. Hivyo elimu unayozungumzia utaipata huko ni zero. Serikali ingefaa iwe inapitia humu kutoa majibu/ushauri panapojitokeza hoja kama hizi.
 
Sipingi kila kitu ila ninaona mengi, yuko mtu namjuwa anatumia dawa za kuhifadhia maiti kusafirisha mboro za ng'ombe Kenya kwenye soko lake ambazo zinatumika kama law material.

Nimetembelea Warundi kule nyuma ya breweries ilala mpaka sinywi tena hizi kahawa za wagogo au kwenye vijiwe vya kahawa ingawa niliachaga kutumia muda kwa sababu ya caffeine.
Ni kweli lakini uliyoyaeleza yana uhusiano Gani na mchele kupakwa mafuta
 
Mafuta ya kupikia wanaupaka ili ung’ae
 
Nyie ndo mnavuaga na masharti halafu mnapaka mafuta Kwa miguu?🤣🤣🤣
Mamy K ni ili kuhifadhi ya tunatumia miguu kama vile unatembea TU maana kuinama mda mrefu ni shida😥
Ukija ifakara ndio kazi zetu
 
Back
Top Bottom