Mchele unapogeuka pumba................

hivi kuna wanawake wanajitongozesha kwa wanaume waliolegea?? wa nini sasa?? just thinking loud....l.o.l
 
😛opcorn:naona matangazo yanapita hapa kuna movie litaanza muda si mrefu na inaonekana litakuwa si la kitoto:wink2:
 
Jasiri umekuwa, kwa kutoa lako sononeko
Hongera nnakupa, kwa kujikaza moyo wako
Na pole nafuatisha, kukufariji mwenzangu.
Ya juzi siyo ya jana, na ya leo kesho sahau
Maumivu yatakwishwa, burudani yako roho
Jamvi litakuwa zulia, usitamani kubanduka.

Shukrani nazitoa kwako wewe muhisani
Pole yako napokea atakulipa manani
Kumbe umalenga mahiri wa vina na mizani

Mistari yako imetulia hilo halina ubishi
Hayachoshi kwa hakika wala si hashi hashi
Yanawafunza wa mbali dar mpaka moshi

Salute mkuu...........
 
😛opcorn:naona matangazo yanapita hapa kuna movie litaanza muda si mrefu na inaonekana litakuwa si la kitoto:wink2:

mimi nitaangalia hiyo movie....wewe je?

umepotea dear....tuko hapa na Shossi tunafurahia mashairi.....
 
hivi kuna wanawake wanajitongozesha kwa wanaume waliolegea?? wa nini sasa?? just thinking loud....l.o.l

Kulinda yako heshima Si jambo la kununua
Bure silaumu mama Mzazi alokuzaa
Hafundishi ya zahama Mabaya kukutakia
 
mimi nitaangalia hiyo movie....wewe je?

umepotea dear....tuko hapa na Shossi tunafurahia mashairi.....

Mimi natoa mashairi wewe unatukana ikiwa nimelegea umeshawahi kunipa nikashindwa kwani usipo changia kwenye thread yangu utapungua?
 
Kulinda yako heshima Si jambo la kununua
Bure silaumu mama Mzazi alokuzaa
Hafundishi ya zahama Mabaya kukutakia

kuuliza si ujinga ndugu yangu
mama yangu atoka wapi kwa swali langu
samahani kama nimekukera.
 
Im watching vere vere. Hiyo movie isiwe ya jak chen tu maana patachimbika.
 
Huyo kama kavinjari
Wewe vuka bahari
Nenda Zanzibari
Kule mambo shwari

Bahari sitaivuka tatafuta wa tabora
Binti wakinyamwezi asie na harara
Awe mwenye huba asiwe na papara
Nikitoka kazini anikune upara........
 
Mimi natoa mashairi wewe unatukana ikiwa nimelegea umeshawahi kunipa nikashindwa kwani usipo changia kwenye thread yangu utapungua?
:bathbaby:nkimaliza:washing:nkimaliza:A S-coffee:nkimaliza:fish2:
 
kuuliza si ujinga ndugu yangu
mama yangu atoka wapi kwa swali langu
samahani kama nimekukera.

Kulinda yako heshima Si jambo la kununua
Bure silaumu mama Mzazi alokuzaa
Hafundishi ya zahama Mabaya kukutakia
HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

Heshima inaposimama Mja mwema unakua
Heshima inapoparama Utu thamani potea
Heshima nayo tizama Hifadhi kishikilia
HESHIMA KITU CHA BURE ,WAJIBU KUWAZINDUA

Mimi natoa mashairi wewe unatukana ikiwa nimelegea umeshawahi kunipa nikashindwa kwani usipo changia kwenye thread yangu utapungua?

wewe nimekutukana saa ngapi? na nimekutukanaje? usianze usichoweza kukimaliza tafadhali.....siko JF kutukana bila sababu....nimekuuliza swali,kama huwezi jibu unasema....acha kujishtukia na kusingizia wenzio....loh......!!!!!!!!!!.....nachangia thread yeyote tu nayojisikia.....
 
nina mapera na apples hapa na mabis nimeagiza....movie ndo inaanza....:decision:

kwa haya uliyokaaa nayo mapera na maapples na kwa hili movie nadhani yatatukwama,maji yenyewe ya kidebe:rain:
 
kuuliza si ujinga ndugu yangu
mama yangu atoka wapi kwa swali langu
samahani kama nimekukera.

Originally Posted by Michelle
hivi kuna wanawake wanajitongozesha kwa wanaume waliolegea?? wa nini sasa?? just thinking loud....l.o.l

Namsuhuru Mungu Kiswahili nakijua tena kiswahili hasa nimezaliwa mwambao wa pwani R siweki L na L siweki R. Naweza nikasoma maneno mawili tu nikajua mtu anaelekea wapi naweza nikakuchambulia tungo ya ubeti mmoja siku nne. Bahati yako Mwalimu Mrimi Mnandi amekufa ningekuambia umtafute halafu umuulize habari zangu kuhusu kiswahili angekuambia.................. kwahiyo chukua tahadhari na tuishi kwa amani.

Shukrani.
 
na bado.....mashairi utatungia watu sana.....!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…