Mchele wa pakistani nihatari kwa wakulima watanzania..!

Mchele wa pakistani nihatari kwa wakulima watanzania..!

pazzy

Senior Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
194
Reaction score
60
Serikali imeamua kuwafutia kodi wafanyabishara wakubwa wa mchele Ili waingize mchele kutoka pakistani...hatua hii niusariti kwa wakulima wakitanzania kwani Imeharibu soko landani na kuwatengenezea wakulima wapakistani soko!Dawa yakupunguza mfumuko wa bei hasa kwenye chakula niserikali Ikubali kupunguza bei za pembejeo,mbegu,madawa na mafuta ya Diesel kwaajili ya trekta...Magodaoni makubwa yamefulika mpunga makamambako,ubaruku,rujewa,chimala,namanyele na kyela!Mpunga mpya upo tayali shambani lkn wakulima wamekwama kuvuna hakuna sehemu yakuhifadhia hawako tayali kuuza kwahasara kwani watashindwa kulipa madeni waliokopa kwa ajili ya shughuli za kilimo..!
 
Katika hili siilaumu serikali kabisa, tatizo wakulima wakubwa na wachuuzi wa kati wamekuwa na kawaida ya kununua mpunga mwingi kwa wakulima wadogo kwa bei chee na kuuhifadhi wakisubiri bei ipande ili wauze kwa bei kubwa na kupata faida mara dufu pasipo kujali hali halisi ya wananchi walio wengi, enzi za Sokoine aliwafunga jela wafanya biashara wenye tabia za kiuaji namna hii. Kama hamtaki kuuza kwa bei tunayoimudu endeleeni kuhifadhi si twajilia wa Thailand siku zaenda.
 
Hapa hakuna haja ya kuilaumu serikali kwani wafanya biashara wa kitanzania ndio wanafanya biashara za kizamani!mfano mimi mwaka jana nilikuwa mpanda mkoa mpya wa katavi,watu wananunua mpunga mwingi toka kwa wakulima,wanaufungia kwenye maghala,wakisubiri bei zipande,mwezi wa 11,ulifikia tsh.1600 kwa kilo kwa bei ya jumla ya mchele,bado hawakutaka kuuza wakisubili mwezi kuanzia mwezi feb,kweli Mungu c mzee mkumba,wamevuna walichopanda wanalia kwa sasa mchele hadi tsh.900,na bado wanunuzi hawaonekani!na ndio hawa hawa wanaleta shida kwa wananchi,wanafungia mzigo wakisubilia faida mala dufu,matokeo yake supply inakuwa ndogo,huku demand inaongezeka,acha walie wala c wakuonea huruma hata kidogo.
 
Mkuu White Wizard nakubariana nawe kabisa, mleta mada yawezekana ni muathirika wa hili tatizo ndio maana anadai serikali inaua soko la ndani, jukumu kubwa la serikali ni kuhakikisha usalama wa chakula kwa watu wake kwa kiwango wanachokimudu. Haingii akilini kabisa mleta mada anayataja maghala yote kuwa yamejaa mpunga wa mwaka jana wakati masokoni hakuna bidhaa, imamaana hakuna usafiri? Wao hawana huruma kwa raia wenzao wanalalamika nini sasa? Nashauri serikali isiishie kwenye mchele tu.
 
Hongera kubwa kwa serekali yetu,mungu azidi kuwapa hekima ya kutusaidia wananchi
 
Ha haa mchele kwa sasa sio biashara tena.kwa wale waliolima mpunga imekula kwao.MIA!
 
Hapa hakuna haja ya kuilaumu serikali kwani wafanya biashara wa kitanzania ndio wanafanya biashara za kizamani!mfano mimi mwaka jana nilikuwa mpanda mkoa mpya wa katavi,watu wananunua mpunga mwingi toka kwa wakulima,wanaufungia kwenye maghala,wakisubiri bei zipande,mwezi wa 11,ulifikia tsh.1600 kwa kilo kwa bei ya jumla ya mchele,bado hawakutaka kuuza wakisubili mwezi kuanzia mwezi feb,kweli Mungu c mzee mkumba,wamevuna walichopanda wanalia kwa sasa mchele hadi tsh.900,na bado wanunuzi hawaonekani!na ndio hawa hawa wanaleta shida kwa wananchi,wanafungia mzigo wakisubilia faida mala dufu,matokeo yake supply inakuwa ndogo,huku demand inaongezeka,acha walie wala c wakuonea huruma hata kidogo.

Mkuu nakuunga mkono kwa 100%. Tatizo la nchi hii ni hawa "wadudu" wanaojiita wafanyabiashara hasa hawa wachuuzi uchwara; wanaharibu sana mwenendo wa bei za bidhaa hususan vyakula kwa makusudi mazima. Mimi nisingekuwa na tatizo kwa mfano kama bei ya mchele ingefikia hata sh. 5000/= kwa kilo lakini wakulima wetu wakafaidika na bei nzuri ya wanachozalisha lakini hali halisi ni kinyume kabisa.

Hawa washenzi wananunua mazao kwa bei za kutupa kutoka kwa mkulima maskini, wanayahifadhi maghalani kwa makusudi ili kuyumbisha bei ya soko kisha kuyauza kwa wananchi kwa bei ghali huku wakitengeneza faida ya kutisha - ndio mchezo unaochezwa.

Kimsingi serikali ingekuwa makini vya kutosha ilitakiwa iwe na mfumo wa udhibiti wa bei kuhakikisha kuna proportionality kati ya bei anayouzia mkulima na ile anayonunulia mlaji wa mwisho ili pande zote nne (mkulima, mfanyabiashara, mlaji, na serikali) zifaidike kwa usawa.

Zamani enzi za Mwalimu kulikuwa na chombo kinachoitwa Tume ya Bei ambayo ilikuwa na jukumu hili lakini tangu tulivyoingia kwenye soko huria kichwa kichwa haya ndio matokeo yake. Anyway, hata hivyo hatua iliyochukuliwa na serikali kuingiza mchele kutoka nje ili kushusha bei ni ya muhimu japo ya muda.
 
Tunahitaji mapato ya uwiano kutoka mzalishaji, mchuuzi na mlaji. kwa hili serikali imetenda vema.

Bado serikali inasuasua kuhusu biashara ya mafuta diesel na hususan bei ya mafuta ya taa kama watashughulika nalo

pia ili walalahoi wanunue kerosine kwa bei halali, ingekuwa bora zaidi pia. Hapa kwenye kerosine kuna watu wanatuibia

watumia vibatali kwa mtindo wa kinyonyaji kama hawa wa kuhifadhi mpunga kisha kutunyanyapaa kwa bei kali maradufu.
 
Impact kwenye Shillingi itakuwaje? Maana unapozungumza mchele ni sehemu kubwa kwenye kikapu cha mwananchi.

Hii move inasaidia ku curb inflation short term lakini huko mbele dollar inaathirika na dollar ndio hii inaenda kununua mahitaji yetu nje so sioni kama serikali imemsaidia mwananchi overall effect ni ZERO!
 
Mkuu you nailed my comments, Hongera kwa kugundua hilo, yani nisingekuwa na mazoea ya kusoma post zote ndo nichangie ningejikuta nachangia mawazo yako yaleyale.

Serikali iangalie upya hapo katika balance of trade (payments), tusije tukadhani tunawakomoa wafanya biashara na kusaidia walaji kumbe implication zake zitakuja kuwa mwiba tena kwa mwanachi baada ya muda mfupi. Nadhani chamsingi serikali inapaswa kuanzisha utaratibu wa kudhibiti hawa wafanyabiashara uchwara wanaofikiria profit maximization kila siku.

Sasa hivi kwa kuangalia tuu mzunguko wa ndani umeathirika sana kutokana na serikali kufanya project kubwakubwa na haya makampuni ya nje sasa tumejikuta dollar zote tunalipa haya makampuni mbaya zaidi hayatumii bank za ndani ya nchi wao, wanajali kuexport akiba yetu ya dollar au inatugharimu TZS nyingi ili kuweza kufacilitated USD payments ambazo hazibki ndani ya nchi instead zinakwenda kwa mataifa ya nje.
 
Mchele wa bongo bado bomba sana hata wakileta hawawezi kushindana na kitu cha asili kutoka kiela ,morogoro,shinyanga na mwanza. kitu kinanukia Bwana ,kitu kinanoga. hata wakileta watu watachukulia kama makande tuu. ukitaka kujua mchele wetu una thamani ona jinsi wakenya wanavyoangaika kuusaka vijijini.Ingekuwa huo wa pakistani ni dili si nchi yao ingeondoa kodi ili uingie kwa wingi kwao?
 
Ndo Matunda ya kuwa na serikali ya hovyo hovyo wakati mkoa wa Morogoro peke yake unatosha kulisha nchi nzima na mikoa mingine ikalisha East Africa au Afrika kwa ujumla eti tunaagiza mchele nje ya nchi na tunazuia wakulima wetu ku export hovyoooooooooo
 
Steven Robert Masatu and Maundumula .Si kweli kwamba huo mchele utaleta athari kubwa za thamani ya hela yetu dhidi ya dola kwa kiwango mnachokidhania nyinyi.Inflation kubwa inayotokea tanzania imeletwa na factors nyingine kabisa.Balance of trade (Bop) has never balanced in any where in the world.
Do you know that, The opening of the country to international trade means exposing the country to a new set of relative price.when there are different prices the producer and consumer would adjust by reallocating their production and consumption patteren (Refer: Autarky Equillibrium theory)
 
Hii ni nchi ya vituko kweli, nchi pekee ambayo kinachozalishwa ndani ni ghali kuliko kile kinachotoka nje!!! Tumeona hivyo kwenye sukari ya kutoka nje, cement ya Pakistani, na sasa tena tunaona kwenye mchele!

Soko limeachiwa wafanyabiashara walitawale walifisadi wanavyotaka na wanachofanya ni zaidi ya soko huria, hawataki sukari ya nje ije sababu itakuwa bei nafuu kushinda ile tu inayozalishwa pale Mtibwa Morogoro !

Sasa inakula kwao kwenye mchele, naunga mkono serikali walichofanya wala siwaonei huruma hao wahujumu uchumi!!!
 
Impact kwenye Shillingi itakuwaje? Maana unapozungumza mchele ni sehemu kubwa kwenye kikapu cha mwananchi.

Hii move inasaidia ku curb inflation short term lakini huko mbele dollar inaathirika na dollar ndio hii inaenda kununua mahitaji yetu nje so sioni kama serikali imemsaidia mwananchi overall effect ni ZERO!

embu funguka kwa kirefu hapo kwenye red
 
Katika hili siilaumu serikali kabisa, tatizo wakulima wakubwa na wachuuzi wa kati wamekuwa na kawaida ya kununua mpunga mwingi kwa wakulima wadogo kwa bei chee na kuuhifadhi wakisubiri bei ipande ili wauze kwa bei kubwa na kupata faida mara dufu pasipo kujali hali halisi ya wananchi walio wengi, enzi za Sokoine aliwafunga jela wafanya biashara wenye tabia za kiuaji namna hii. Kama hamtaki kuuza kwa bei tunayoimudu endeleeni kuhifadhi si twajilia wa Thailand siku zaenda.
sure acha wa kwao uozee ndani,mchele ulikua unafika hadi 3000 kwa kilo.
Mwaka huu zengwe limewakuta,mchele utashuka hadi 700/kg.
 
Watu wanatumia dollar kuagiza mchele sasa unacurb inflation kwa kuraise dollar demand si WEHU Huo. Kuna matatizo ya msingi bei za mchele au biadhaa za Tz kuwa juu kuu ni high cost of production. Mbolea bei iko juu tena zaidi ya 30% feki Matrekta hayashikiki maana yanauzwa kwa bei ya kukomoa mpaka wameanza kukopesha Na mbaya zaidi mbolea na matrekta imekuwa miradi ya wakubwa walivyo na akili kama kuku mwaka huu WAKULIMA watakufa moyo wa kulima na ivyo mbolea yao itaganda kwenye maghala Mpunga kuna mahala wameshaanza kuvuna sasa si uhujumu huu JAMANI kama ungeletwa miezi kati ya DEC to MARCH ningeelewa sasa mpunga umeanza kuvunawa wewe unaleta mwengine. Hakuna wa kupigania haki za wakulima ila msife MOYO mchele wa Tz huwezi fananisha na hayo makapi/mashudu toka Pakistan. Mdau kaongelea cement ya Pakistani kumbuka ghalama zao za uzalishaji ziko chini unlike Tz umeme tuu kuna kampuni inalipa ALMOST 1 Billion kama bili ya umeme Ilo la SUKARI pia wakubwa wana hisa zao kwa ivyo viwanda na hata wakiimport kunakuwa na controls
 
Tatizo la wakulima wa Bongo ni kukosa Ubunifu na kubakia kulia la tu, na kulaumu Serikali, Wakulima wa Tanzania wanao uwezo wa Kufikia hao wa Pakstan,

Ni kweli Tazania tunazalisha Mchele mzuri sana, Ila Wakulima badala wajikite Kulima Kibiashara wao wako bise na mambo mengine, Hiawezekani Uanze kilimo ha Mpunga miaka ya 90 alafu bado eti unataka Seriklai iwakopeshe Mtrekta,na iwape bure Mbolea,

Tuliwahi fanya Research Fulani Magugu wanapo lima Mpunga kwa wingi, Wengi wa wakulima wanapo uza Mpunga hakuna hata mmoja anaye kuwa na wazo la kupanua kilimo chake na kununua mitambo ya kisasa ya kulimia badala yake ni Kujenga Gest na na kununua magari ya kutembelea, na hii iko kwa wakulima wengi, jaribu kuwauliza wakifanikiwa kupata pesa nyingi kweny kilimo watafany nini,

Na hapo ndo wakulima wengi wa Bongo anappo kosea, Ubunifu hakuna na watu wanafanya kilimo kama Daraja l kupitia kwenda kufnya ishu zingine, watu hawafanyi kilimo kama Biashara, sasa ni kwa nini tusizidiwe na pakstani na wengineo?

NI LAZIMA WAKULIMA WABADILIKE NA WALIME KIBIASHARA NA WAJIKITE KUWEKEZA KWNYE KILIOMO ZAIDI NA SI MTU WAKATI WA MAVUNO NDO ANAPANGA KUOA AU KUNUNUA GARI AND THEN HUYO HUYO MTU ATAKUJA KULAUMU SERIKALI KWA KUTO KUMPATIA TREKTA
 
Back
Top Bottom