SAMIA CUP SAKA VIPAJI MTAANI KWAKO
Tarehe 24/3/2022, DODOMA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mchengerwa, akiwa anazungumza katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ameelezea dhamira yake ya kuleta mageuzi makubwa katika Tasnia za Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kati ya vitu atakavyoanza ni pamoja na kuanzisha Ligi ya Vipaji ya Samia ambayo itafanyika Mtaa kwa Mtaa, Kijiji kwa Kijiji, Nchi Nzima.
Mpango huu unaandaliwa na Wataalam wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo; na tayari Wadau mbalimbali wameshajitokeza kuchangia Vifaa Vya Michezo. Waheshimiwa Wabunge wanategemewa kusimamia katika maeneo yao ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.
Sambamba na Uchezeshwaji wa Ligi hiyo, Mhe Mchengerwa aliipa taarifa Kamati kuwa, Kuanzia Tarehe 4 mpaka 6 Aprili, Maafisa Utamaduni na MaaFisa Michezo Nchi Nzima, watakutana Dodoma kwa ajili ya kikao kazi, kati Yao na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni Pamoja na mchakato wa maelekezo ya Mtaa kwa Mtaa Samia Cup Saka Vipaji Mtaani Kwako.
Samia Cup Saka Vipaji Mtaani Kwako
Jambo hili lilipokelewa kwa shangwe kubwa sana na kuungwa mkono na Wajumbe wote wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.