LGE2024 Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72

LGE2024 Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakati upigaji kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ukiendelea maeneo mbalimbali nchini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema matokeo yote yatakuwa yametoka ndani ya saa 72.

Pia, Mchengerwa amewasihi Watanzania kuendelea kujitokeza kupiga kura kuwachagua viongozi hao na kudumisha amani.

“Ndani ya saa 72 Tamisemi itakuwa tayari imekusanya matokeo yote kwa ujumla na kuyatangaza lakini, tunaamini kwa mifumo tuliyonayo sasa shughuli itakuwa fupi, kuna maeneo kuanzia leo hadi kesho matokeo yatakuwa yametangazwa,” amesema Mchengerwa wakati akizungumza na wanahabari leo Novemba 27, 2024.

Aidha Mchengerwa amewaelekeza wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi kuwasaidia wapiga kura kusoma orodha ya majina vizuri ili wote waliojiandikisha wapate fursa ya kupiga kura.
Screenshot 2024-11-27 144748.png


Mchengerwa amesema hayo mara baada ya kupiga kura katika kituo chake alichojiandikishia cha Umwe Mchikichini kilichopo Ikwiriri Jimboni kwake Rufiji Mkoa wa Pwani, Waziri Mchengerwa amesema taarifa alizonazo mpaka sasa uchaguzi unaendelea kwa hali ya amani na utulivu nchi nzima.​

Soma pia: Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024



Chanzo: Mwananchi
 
Haoni hata aibu video za kura za wizi kusambaa hata vituo kabla havijafunguliwa ndil unaita uchaguzi?
 
DEMOKRASIA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema baada ya kukamilika kwa zoezi la Kupiga Kura, utaanza utaratibu wa kuhesabu Kura na ndani ya Saa 72 Matokeo yote yatakuwa yametangazwa.

Akizungumza kutoka Rufiki, Pwani, Mchengerwa amesema baada ya Walioshinda katika maeneo yao kutangazwa, TAMISEMI itakuwa imekusanya Matokeo yote kwa Ujumla kutokana na mifumo iliyopo na itayatangaza kwa Wananchi.
 
 
Back
Top Bottom