Chipoku
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 254
- 181
Robert Mutabingwa - Kawe
Tar 8 Jan ,2022. Rais Samia alipombadilisha wizara Mchengerwa kutoka Utumishi kuja Michezo (Wizara anayo hudumu kwa sasa); zaidi ya 85% ya watumishi wa umma ni wapenda maendeleo na wazalendo.
Tulilia na kulalamika juu ya uamuzi huu na kujaribu kupaza sauti ikimpendeza Rais apate tafakuri ya kubadili uamuzi wake.
Tuliongea mengi husan katika mitandao ya kijamii ikiwemo hapa hapa JF; baadhi ya headlines zilikuwa👇👇👇
✅Tunaomba Rais Samia uangalie hili kwa jicho la utendaji
✅Mama kumtoa Mchengerwa Utumishi haijakaa poa
✅Rais utakuwa umedanganywa au hauna data za kutosha
✅Rais: Kupitia Mchengerwa imani ya watumishi juu ya Serikali yako ilianza kurudi
✅Mchengerwa is the right & great, au huna data Rais?
✅Watumishi tulipata mtetezi
✅Sema na Waziri
Mchengerwa kidijitali tulisema alitusikiliza, na kero zetu zilipatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi. Lakini hatukuwa na jinsi, mwenye maamuzi aliamua.
Tangu aje Wizara ya Michezo na Utamaduni Mchengerwa hajapoa wala hajaboa, hasinzii yeye wala timu yake, wizara iko moto!
▪️Tumeshuudia Timu ya Serengeti Girls ikifuzu Kombe la Dunia.
▪️Maafisa Utamaduni na Michezo nchi nzima wamepatiwa na wanaendelea kupatiwa mafunzo maalum ya kusimamia na kuibua vipaji kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa.
▪️Ukarabati wa viwanja vya michezo umewekewa bajeti katika mwaka wa Fedha 2022/23, ikiwemo viwanjwa vya Ben Mkapa na Uhuru DSM, Arusha, Tanga, Mwanza, Mbeya na Dodoma.
▪️Mkakati wa kutengeneza miundombinu ya michezo katika shule mbili katika kila mkoa Tanzania.
▪️Kusimamia TFF na ZFF kutafuta wachezaji watakao tumikia timu ya taifa.
▪️Ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Dodoma ambao upo kaatika hatua za utekelezaji, tayari Serikali imeshaanza kutenga fedha za ujenzi.
▪️Tanzania imeshiriki kwa mafanikio makubwa Jama Festival 2022 Burundi.
▪️Wizara ya michezo kugharamia Shindano la Walimbwende na Watanashati Viziwi la Kimataifa 2022
▪️Uhamasishaji mkubwa uliyopelekea kufanikiwa kwa kiwango cha juu zoezi la sensa na makazi 2022 kupitia #Sensabika.
▪️Wizara kupeleka kambi timu za Serengeti Girls uingereza na walemavu Uturuki.
▪️Mkutano Mkuu wa 44 wa CAF umefanyika nchini na kuleta tija kubwa katika michezo na utalii: Rais wa FIFA alihudhuria.
▪️Usimamizi bora wa wizara ukiongozwa na Waziri Mchengerwa umepelekea kupaatikana kwa medali nyingi katika michezo ya Jumuia ya Madola, muulize Simbu.
▪️Kuboresha sekta ya filamu, kusajiri wasanii nchini kidijitali
▪️Kukwa ya yote ni kutimiza dhamira yake ya kuwaongezea thamani wanamichezo na wasanii. Mpango wa utoaji mikopo kwa wanii bila riba ni rasmi sasa, muulize Mike T a.k.a Mnyalu(Mwenyekiti wa Wasanii akujuze).
✅Mchengerwa katika mawaziri wa awamu hii ya sita ni mfano mzuri wa ubunifu na utendaji uliyotukuka. Ni mtu wa kasi kwelikweli, akiamua jambo lake linawezekana.
Huyu ndiye Mh.Mchengerwa mtu kazi, Waziri kijana mdogo mwenye fikra za kimapinduzi na ambaye anafaa kila wizara.
Aliwahi kusema RC Mtaka (Njombe) kuwa Tanzania haijawahi kupata Waziri ma mfano wa Mchengerwa kwa uchapakazi toka uhuru.
Profesa Kitila Mkumbo akichangia bajeti ya Wizara ya Michezo 22/23 aliongeza bungeni kuwa Mchengerwa ndiye waziri anayeitendea haki wizara yake katika awamu ya 6.
✅Tuache kutumika kwa maslahi binafsi kumchafua kwani Haitawezekana, Watanzania wapenda haki na utekelezaji wa viwango tuko nyuma yake.
✅ Tusilazimishe kumrithisha uadui wetu wa Simba na Yanga, msanii na msanii, hapa. Tumuache atekeleze dhamira yake na ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia yakuona kuwa michezo, utamaduni na sanaa inakuwa inatoa ajira kwa Watanzania wengi ili kuchangia uchumi wa taifa, kuleta furaha na faraja kwa Watanzania kupitia sekta hizi.
Waziri endelea kuchapa kazi achana na kelele za chura.
Hakika Mchengerwa mtu kazi ni alama ya vijana wazalendo wa taifa hili na taswira halisi ya teuzi zenye tija za Rais Samia.
#Kaziiendeleee
#Mchengerwamtukazi