ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kwa mujibu wa Waziri wa Tamisemi bwana Mohammed Mchengerwa amenukuliwa akisema kuwa Rais Samia Ameridhia Iliyokuwa Halmashauri ya Rufiji kupewa Hadhi ya Mji ambapo Jengo kubwa la Makao Makuu la zaidi ya Bilioni 10 litajengwa Ikwiriri.
Kana kwamba haitoshi,ikumbukwe kwamba Mkuranga imeomba kuwa Manispaa ambapo Stendi kubwa ya Mabasi inaendelea na Ujenzi.👇👇
=======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia Kujenga soko kubwa la kisasa pamoja na Kituo kikuu cha Mabasi wilayani Rufiji Mkoani pwani mara baada ya kuipandisha hadhi wilaya hiyo na kuwa Halmashauri ya Mji wa Rufiji.
Kulingana na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara Ikwiriri wilayani humo, amesema utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa unatarajiwa kuanza rasmi mwanzoni mwa Mwezi Novemba mwaka huu 2024.
Mhe. Mchengerwa amewaambia wananchi wa Rufiji kuwa ujenzi wa soko hilo litakalokuwa na maduka zaidi ua 122, Vizimba zaidi ya 100 na vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo utagharimu fedha taslimu shilingi Bilioni 14 huku pia Serikali ya awamu ya sita ikiahidi kujenga Jengo la Utawala katika Halmashauri hiyo ya Mji litakalokuwa la Ghorofa tatu zenye Ofisi zaidi ya 50 na kugharimu takribani shilingi Bilioni 10.
My Take
Halmashauri zilizokidhi vigezo na kuwasilisha maomba mapema kabla ya kina Rufiji nazo zipandishwe hadhi pia mfano Mbalizi Kwa Mwamposa.
Pia soma: Rais Samia akataa ombi la kuipandisha hadhi Mbalizi kuwa Halmashauri ya mji