Mchengerwa umefanya kazi gani kushughulikia kero za wananchi wakati Mwenezi Makonda amefanya mpaka kliniki za kusikiliza kero zianzishwe?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Mchengerwa anaongelea kushughulikia kerozipi kubwa wakati Mwenezi Makonda anakutana na watu kadha wa kadha wakiwa na kero lukuki mpaka zinaanzishwa kliniki za kusikiliza kero hizo?

Sekta zote zimevuliwa nguo na Mwenezi Makonda mpaka Mawaziri mnaonekana mifugo halafu unasema umefanya kazi kubwa toka uteuliwe? Kazi gani hiyo Mchengerwa?

Hatua kwa wala rushwa zinachukuliwa kwa vidagaa tu wakati wote wakati papa wanaachwa, sasa anajigamba kwa lipi? Ubadhirifu uliofanywa mwaka 2022, 2023 umeyeyuka umebaki tu ule uliofanywa kipindi cha Magufuli?
 
Kwani wezi si walewale Mr Mchengerwa?
Kwani wanatoka nje ya CCM mkuu?
Mkuu ccm wameharibu sana nchi hii kimaadili
 
Tusiingilie ugomvi wa familia!
 
Ila jamaa kapoa sana siku hizi tofauti na mwanzoni wakat anarudishwa hapo Tamisemi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…