Mchepuko hauna huruma

Mchepuko hauna huruma

Hii yote sababu tuu sheria inakutaka uoe mke mmoja. Aliyeleta huu utaratibu wa kuoa mke mmoja ndiye wa kubebeshwa lawama zote. Sex is fun, marriage is love.
 
Hii yote sababu tuu sheria inakutaka uoe mke mmoja. Aliyeleta huu utaratibu wa kuoa mke mmoja ndiye wa kubebeshwa lawama zote. Sex is fun, marriage is love.

Hii comment ipigwe lamination kabisa[emoji4]
 
Habari yako wapendwa poleni na changamoto za usafiri kwa wale wanaowahi sensa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Naomba moja kwa moja niende kwenye uzi husika bila kupoteza muda. Imekuwa ni tabia ya kawaida kwa baadhi ya wanaume kutafuta nyumba ndogo (mchepuko) kwa ajili ya starehe binafsi lakini pia kati yao wapo wanaume wengi ambao michepuka hiyo hiyo imewaponza hadi kupelekea mfarakano wa kifamilia.

Hebu fuatana nami kwenye simulizi hii ambayo imetokea kweli kabisa. Kama mjuavyo maisha ya kota ushirikiano wa hapa na pale huwa haukosi basi katika nyumba moja mfanyakazi mwenzetu aliingia kwenye mgogoro na mkewe hadi kupelekea mke wake huyo kuondoka.

Basi jamaa akabaki na watoto na baada ya muda akaoa mke mwingine maana jamaa umri ulikuwa umeenda kidogo basi baada ya kuishi na mke wake huyo wakabahatika kupata mtoto mmoja.

Baadaye jamaa akapata uhamisho wa kwenda kwenye kata nyingine basi maisha yakaendelea jamaa akapata kimada na hapo ndipo seke seke lilipoanza.

Kwa kuwa alikuwa anakaribia kustaafu huo mchepuko ukaona huo ndio wakati sahihi wa yeye kula hela za mzee huyo pindi atakapostaafu.

Huyo mstaafu mtarajiwa alidumu na huyo mchepuko kama miezi 6 hivi ghafla mke wake wa ndoa akaanza kuumwa ugonjwa haueleweki. Baada ya kupatiwa matibabu kama baada ya miezi 3 yule mwanamke akafariki.

Ndugu wa yule mwanamke sasa ikabidi waangalie na upande wa pili (ushirikina /kwenda kwa waganga wa kienyeji) basi walienda kwa waganga kama 4 kila mganga akasema yule mwanamke amerogwa na mchepuko wa mume wake ili huo mchepuko upate ndoa.

Wale ndugu wakafikisha ujumbe kwa Shemeji yao naye kwenda kuangalia akapewa jibu hilo hilo kwamba mchepuko ndio umehusika basi ikabidi jamaa afanye maamuzi magumu ya kuuacha huo mchepuko wake.

Baada ya kuuacha anataka arudishe majeshi kwa mke wake yule wa kwanza ili wale wote hela za kustaafu walee na watoto wao. Kwa watu ambao hawaamini ushirikina itakuwa ni vigumu sana kuamini hilo swala la mtu kurogwa hadi kufa.

Lakini ninachopenda kuwaambia ni kwamba kuwa na mchepuko sio tatizo lakini jitahidi mchepuko wako usifanye wewe kutengana au kukosana na familia yako

Usifanye watoto wako wakateseka sababu ya michepuko. Watoto wakakosa ada sababu ya mchepuko au nyumba ndogo

Tuwe wastaarabu visima ni vingi ila maji ni yale yale [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1488]
Chai....mara mke alifariki , mara akataka warudiane ....Duh
 
Chai....mara mke alifariki , mara akataka warudiane ....Duh
We ndo hujasoma ukaelewa, kasema mke wa kwanza waligombana akaondoka , akaoa mwingine akazaa nae mtoto, sasa aliyefariki kwa kulogwa ni huyu wa pili baada ya kuachana na yule wa kwanza, so mzee akaamua kurudi wa yule mke wa kwanza waliyeachana kwa ugomvi.
 
We ndo hujasoma ukaelewa, kasema mke wa kwanza waligombana akaondoka , akaoa mwingine akazaa nae mtoto, sasa aliyefariki kwa kulogwa ni huyu wa pili baada ya kuachana na yule wa kwanza, so mzee akaamua kurudi wa yule mke wa kwanza waliyeachana kwa ugomvi.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom