Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
Note 📝 NAHODHA wa JKT Tanzania, Edward Songo amesema uwepo wachezaji wa kigeni Championship, umeisaidia kuipa thamani kubwa ligi hiyo na inakuwa rahisi kwao kuonekana na timu za Ligi Kuu.
Akijitolea mfano baada ya kufanya vizuri msimu uliopita ambapo alikuwa kinara wa mabao 16 na sasa ana 11 kwamba alifuatwa na Azam FC iliyokuwa inahitaji huduma yake ila alishindwana nao.
Songo alisema Azam ilimwekea dau la usajili la Sh100 milioni na mshahara wa Sh.3 milioni, lakini aliona sio pesa inaoweza kumvua magangwa ya jeshi na aliamini hiyo pesa anaweza akapata mkopo serikalini kwa muda mfupi.
"Niliwaambia nahitaji Sh.250 milioni, lakini hatukufikia mwafaka, yote katika yote nilionekana kwenye Ligi ya Championship ndio maana nasema kwa sasa ina thamani kubwa na ina mashabiki; Aliongeza "Angalau maisha ya wachezaji wanaweza wakapata kitu, kikubwa ni wao wenyewe kuipa thamani kazi zao.