Mchezaji avunjiwa mkataba wake baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya VVU

shushushu VIP

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
4,799
Reaction score
4,312
Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, mkataba wake umevunjwa baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo anamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwa vyombo vya habari.

Mshambuliaji huyo ameitumikia Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.

Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August. Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.
 
Kwani wachezaji hua wanasaini mkataba kabla ya matokeo ya vipimo vya afya?
 
Kwani wachezaji hua wanasaini mkataba kabla ya matokeo ya vipimo vya afya?
Wengine huwa wanasign pre-contract pending to medical (Unasign mkataba tayari ,inabaki kufanya uchunguzi wa afya ukifaulu mkataba unakuwa valid ukifeli mkataba unakufa)
 
Wengine huwa wanasign pre-contract pending to medical (Unasign mkataba tayari ,inabaki kufanya uchunguzi wa afya ukifaulu mkataba unakuwa valid ukifeli mkataba unakufa)
Thanks Mkuu.
 
Samahani naomba kuuliza, hivi mchezaji akigundulika na maambukizi ya VVU kwenye sheria za CAF na FIFA inakipengele kinachoonyesha kukatisha mkataba ya mhusika au ni jambo la club husika?
 
Samahani naomba kuuliza, hivi mchezaji akigundulika na maambukizi ya VVU kwenye sheria za CAF na FIFA inakipengele kinachoonyesha kukatisha mkataba ya mhusika au ni jambo la club husika?
Sidhani kama anazuiliwa wanasema Misri ili upate work permit lazima upimwe Ukimwi
 
Samahani naomba kuuliza, hivi mchezaji akigundulika na maambukizi ya VVU kwenye sheria za CAF na FIFA inakipengele kinachoonyesha kukatisha mkataba ya mhusika au ni jambo la club husika?
Mchezaji kua na VVU ni hatari hata kwa wachezaji wenzake!

Fikiria kama akigongana na wenzake mpaka kupasuka hadi kupelekea damu kuvuja! Kuhusu kama ni sheria za CAF au FIFA hilo hata mimi binafsi sijui.
 
So kwann wamesema hadharan kuwa ana vvu bila consent yake?
 
Nisingekubali kucheza nae mara apate asira akungate?..ila kumuanika hadharani wamekosea wangesema tu haja qualifie vipimo vya afya yake
 
Wamempa support gani wakati wametangaza health status yake hadharani. Hili ni kosa na ni kinyume cha sheria zinazotaka privacy ya mtu ilindwe na kuheshimiwa. Wangeweza kuvunja mkataba bila kutaja sababu Ninachoona hapo ni ubaguzi tu

Ninaamini FIFA and/or CAF wataipiga fine hiyo timu.
 
Mhh huyu player anatafuta umaarufu to.. Mungu ampe maisha marefu
 
Huwenda yeye mwenyewe ametaka iwe hivyo "Hadharani" watu now wanatafuta kik bila kujali aliyonayo,hata kama hana ile kitu chini ilimradi apate umaarufu to.....
 
Huwenda yeye mwenyewe ametaka iwe hivyo "Hadharani" watu now wanatafuta kik bila kujali aliyonayo,hata kama hana ile kitu chini ilimradi apate umaarufu to.....
Wabongo ndiyo watafuta kick ila huko kwingine sina hakika
 
Nisingekubali kucheza nae mara apate asira akungate?..ila kumuanika hadharani wamekosea wangesema tu haja qualifie vipimo vya afya yake
hauwezi kuambukizwa kwa kungatwa ila inauma sana fikilia ndio ingekuwa ni ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…