Mchezaji gani aliyestafu ungependa arudi uwanjani

Mchezaji gani aliyestafu ungependa arudi uwanjani

Ricardo Kaká huyu namwangalia anachipukia hadi anakuja kuvuruga kutransfer to madrid
akiwa mdogo kaka anamanage kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu akiwa na nguli wenye umri mkubwa kama carlos, maldin, Cafu, Crespo, Schevichenko, Nedved, na wengineo vijana wa siku hizi hichi kitu kinawashinda
Mchezaji wangu Bora wa muda wote Ricardo Kaka
kaka ni mrokole mkuu labda ndo maana alifanikiwa huwa hana makuu kabisa huyu jamaa.
 
Louis Saha.

Huyu bwana nahisi alionesha 1/4 tu ya kipaji chake sababu ya kuwa majeruhi mara kwa mara hasa akiwa pale Man U.

Kwa mujibu wa Wyne Rooney ni kwamba Saha ndiye favorite player wake ambaye amewahi kucheza naye.
hata mm huyu jamaa nilikuwa na muhofia sana pale alipokuwa hata akiingia dk ya 85 lazima mabeki wajipange
 
Mohamed chuma wa mtwara beki miaka 15 taifa starz na mashindano ya ndani hakuwahi kupata kadi nyekundu.
Jari litmannen chuma cha ajax hiki hakikuwa na mchezo na kuzifumania nyavu.
Litmanen na Ajax ile ya akina De Boer brothers, Patrick Kluivert, Finidi George, Edwin Van Der Sar wanabeba Uefa Champions League chini ya Jemedari Louis Van Gaal.
 
Mkuu huyo davo suker alipata tu kiki ile world cup na kuwa top scorrer yani ni kama man fongo na haina ushemeji.

Apart from ile world cup ya 2002 kama sikosei sidhani kama alisikika tena. Huyu ni kama James Rodriguez alivyopata ngekewa world cup 2014 but sa hivi kapotea pale madrid
Suker aling'aa World Cup ya mwaka 1998 pale Ufaransa.

Walishika nafasi ya tatu kama sikosei kulikuwa na fundi wa mpira aliyeitwa Zvonomir Boban jamaa alikuwa analijua kabumbu haswa ndio maana sikushangaa Haruna Moshi alipoiga jina la Boban.
 
Back
Top Bottom