Mchezaji kucheza mechi za ushindani siku mfululizo

Mchezaji kucheza mechi za ushindani siku mfululizo

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Naona kama hili linataka kupita bila kujadiliwa humu na wadau wa soka, sijajua kama limejadiliwa na wachambuzi wetu katika redio zetu za FM.

Nasor Saadun alicheza mechi ya ushindani akiwa na Azam dhidi ya Yanga tarehe 2/11/2024, na game ilikuwa ngumu sana.

Tarehe 3/11/2024, Nasor Saadun akacheza tena Taifa Stars dhidi ya Sudan akitokea benchi lakini. Jamaa akawa anacheza rafu tu mwisho wa siku akapewa kadi nyekundu.

Maswali:
1. Je, kiafya inakubalika?
2. Lengo lilikuwa ni nini kumchezesha ikiwa ametoka kwenye mechi ya ushindani jana yake?
3. Kama inawezekana kwa Nasor, kwahiyo hakuna haja ya kusimamisha mechi za ligi kwa baadhi ya vilabu pendwa yanapotokea mashindano ya kimataifa ili kuwapa nafasi wachezaji kujiandaa vyema mana Nasor kaonesha inawezekana kucheza leo na kesho yake!
 
Umesema neno la maana sana tunashindwa kuwaanda wachezaji wetu toka wadogo sasa inapo fika wakati wa mahitaji ya kitimu na mahitajio ya kitaifa tunashindwa kuwatumia vyema wachezaji wetu,
Hata ukiangalia ni kama alifanya makusudi ili atolewe na akafanikiwa lakini inaligharimu Taifa na viongozi wala hawaogopi wala hawaumii wala hawaoni aibukabisa, inaumiza sana kwakweli.
Taifa linahujumiwa kila upande , sasa sijui na hili tunahitaji nchi wa hisani?!
 
"Soka letu kivyetu vyetu".
Alisikika mtendandaji mmoja wa bodi ya ligi.
 
Ni kutaka kuharibu mwendelezo wake ulio Anza kuwa mzuri katika soka lake.
Hii inaonyesha ni kwajinsi Gani mpira wetu hakuna weredi katika ku uendesha.
Sasa unaweza kuelewa kwanini mechi za Ligi kuu Zina banana kwa kujifichia kwenye kichaka Cha masaa 72.

Hawaelewi kwamba baada ya kucheza timu Ina hitaji Recovery lakini wanasahau baada ya mechi kuchezwa kituo A wachezaji kwa timu nyingi watasafiri kwa njia ya barabara kwenda zaidi ya km 600 kituo B.

Hawajui kama miili ya wachezaji Ina chacha na kutengeneza uchovu mwingi.
Kwa ratiba za hovyo kama ivi ndani ya miezi 2 timu zita Anza kuwa na majeruhi wa kutosha.

Bodi ya Ligi isifananishe masaa 72 ya Ulaya na kwetu Africa, mbaya zaidi mchezji uyo mwenye uchovu anakuja kukutana na uwanja wa hovyo.

Kwenye uwanja wa hovyo mchezaji anautumia Nishati nyingi katika kumiliki na kucheza mpira.
 
Back
Top Bottom