Mchezaji Mahiri wa Brazil, Ricardo Izecson dos Santos Leite 'Kaka' atundika daruga

Mchezaji Mahiri wa Brazil, Ricardo Izecson dos Santos Leite 'Kaka' atundika daruga

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Kiungo wa zamani wa Brazil Ricardo Kaka ametangaza kustaafu kucheza soka jana akiwa na miaka 35. Klabu ya mwisho kuichezea ni Orlando City ya Marekani.

Amewahi kutwaa Ballon d’Or mwaka 2007, Ikiwa ni mchezaji pekee kuweza kuwagagaza Messi na C.Ronaldo katika inyang'anyiro hicho.

Kaka alicheza mechi yake ya mwisho Oktoba Orlando walipomaliza msimu, na mwezi Novemba taarifa zilisema alikuwa amepewa kazi ya kuwa mkurugenzi katika klabu ya AC Milan.

Yeye ni miongoni mwa wachezaji wanane pekee waliowahi kushinda Kombe la Dunia, Kombe la Ulaya/Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na tuzo ya Ballon d'Or.

Wengine ni Bobby Charlton, Gerd Muller, Franz Beckenbauer, Paolo Rossi, Zinedine Zidane, Rivaldo na Ronaldinho.

Kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika;
kaka.PNG


Vilabu alivyochezea Kaka
Sao Paulo - 2001- 2003: (Apps 125, Goals 47)
AC Milan - 2003 - 2009: (Apps 270, Goals 95)
Real Madrid - 2009 - 2013: (Apps 120, Goals 29)
AC Milan - 2013 - 2014: (Apps 37, Goals 9)
Orlando City - 2015 - 2017: (Apps 78, Goals 25)
Sao Paulo (Loan) - 2014: (Apps 24, Goals 3)
 
Ricardo ernesto al mangungule kaka kibraza..

Nilikuwa naprnda kumuita hivi

Bongr la player, mzee wa curve ama ndizi, nilikuwa naprnda zaid driblling yake, akianza kuvutwa vutwa kama anaanguka sasa hiv kumbe mwamba anateleza.. aliupiga mwing sana milan ya kina sheva, gattuso, mviziaji inzaghi, golie dida, maestro pirlo, cafu, kaladze, nguli kitasa maldini, ambrosin, kitasa nesta, na maestro mwingine seerdorf..

Atakumbukwa daima yale aliyoutrndea mchezo wa soka.
 
Manchester hawana hamu nae akiwa Ac Milan alikuja pale pale OT akafanya yake.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Wakati ukuta. Ni mmoja kati ya wachezaji bora wa miongo miwili iliyopita. Aliwavuruga aana United. Pumzika tu.
 
Mourinho ni mduwanzi saana yule mzee.
Mourinyo hajuagi wachezaji wazuri, hata sajili zake huwa anavizia aone mchezaji gani anafukuziwa na team nyingi ndio anajichomeka pale

Refer Lukaku na Morata
 
Hii siku hakuna shabiki wa Manchester United aliyeangalia hii mechi ataisahau. Kaka aliwanyanyasa sana aiseee
Kaka kwenye ile match alikuwa anatuchua kama kichaka na kutukimbza afu na goli anatuweka,Daah siku ile tuliteseka sana.
 
Kaka alikua na uwezo wa hali ya juu. Katika miaka 12 iliopita Yupo nyuma ya Ronaldinho tu.
 
Back
Top Bottom