Mchezaji wa club ya saint-Etienne auawa na watu wasiojulikana

Mchezaji wa club ya saint-Etienne auawa na watu wasiojulikana

usser

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2015
Posts
13,956
Reaction score
14,032
Mchezaji wa Saint-Etienne auawa kwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyekuwa beki wa klabu ya Saint-Etienne inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1, William Gomis amefariki dunia usiku wa jana kwa kushambuliwa na risasi.

Duru za habari zinaeleza kuwa, Gomes mwenye umri wa miaka 19 ameshambuliwa na bunduki aina ya AK47 katika mitaa ya La Seyne-sur-Mer.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa kijana wa miaka 14 amefariki dunia katika tukio hilo huku jeshi la polisi likiwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo ya Kalashnikov (AK47).

Mmoja wa makaka wa kijana Gomis pia aliripotiwa kufa kwa kushambuliwa na risasi wiki chache tu zilizo pita huku klabu ya Saint-Etienne ikithibitisha tukio hilo la mchezaji wao hii leo siku ya Jumatatu..

Screenshot_20180911-104650.jpg
 
Watu wasiojulikana wameama tanzania wameenda ufaransa. Wasije wakaenda kwa fundi wangu Mario Balotelli
 
Pamoja na teknolojia yote ila bado kuwatia nguvuni wauaji
 
Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Saint-Etienne aliuawa ktk shambulizi linalodhaniwa kuwa linahushishwa na biashara za madawa ya kulevya. Eneo la tukio kulikutwa maganda 24 ya risasi toka ktk bunduki aina ya AK-47.

Shambulizi hilo limetokea ktk magorofa -makazi - fukara ya Berthe ktk kitongoji cha Toulon sehemu za La Seyne-sur-Mer, Cote d’Azur ktk pwani ya bahari ya Mediterranean nchini Ufaransa.

Mchezaji huyo umri miaka 19, mwenye wazazi asili ya Ki-Senegali alikutana na umauti akiwa ndani ya gari lake akiwa pamoja na kijana mwingine mwenye asili ya Ulaya ya mashariki.

Mwendesha mashitaka amebainisha kuwa kaka yake William Gomis pia alishambuliwa kwa risasi wiki kadhaa zilizopita.

William Gomis mchezaji chipukizi aliyekuzwa kwa miaka 5 ktk akademi ya klabu hiyo ya daraja la kwanza mwezi Juni 2018 alijitoa ghafla ktk timu hiyo baada ya kukataa mkataba/offer ya kuwa mchezaji wa akiba wa timu ya hiyo maarufu nchini Ufaransa.

Mchezaji mkongwe Bafetimbi Gomis ambaye hana uhusiano wa kindugu na marehemu William Gomis, ametuma salama za rambirambi ktk ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kufuatia msiba wa mchezaji huyo kinda.

Source : {{pageSmoTitle}}
 
Mchezaji wa Saint-Etienne auawa kwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyekuwa beki wa klabu ya Saint-Etienne inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1, William Gomis amefariki dunia usiku wa jana kwa kushambuliwa na risasi.

Duru za habari zinaeleza kuwa, Gomes mwenye umri wa miaka 19 ameshambuliwa na bunduki aina ya AK47 katika mitaa ya La Seyne-sur-Mer.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa kijana wa miaka 14 amefariki dunia katika tukio hilo huku jeshi la polisi likiwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo ya Kalashnikov (AK47).

Mmoja wa makaka wa kijana Gomis pia aliripotiwa kufa kwa kushambuliwa na risasi wiki chache tu zilizo pita huku klabu ya Saint-Etienne ikithibitisha tukio hilo la mchezaji wao hii leo siku ya Jumatatu..

View attachment 862759
Wakezawatusumu
 
Back
Top Bottom