Mchezaji wa Kenya atorokea Tanzania baada ya kukosa kulipwa mshahara kwa miezi 5 mfululizo

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Mchezaji nyota wa Gormahiya na Harambe Star, ameamua kukimbilia Tanzania na kujiunga na Simba ya Tanzania baada ya kutolipwa mshahara kwa miezi mitano.

Ikumbukwe pia kwamba Kahata ambaye alitokea Gormahiya na kujiunga na Simba mwaka Jana, alitoa sababu ya kutolipwa mshahara kwa muda mrefu ndiyo iliyomsukuma kuja Tanzania.

Sass hivi Tanzania ndio kimbilio la wakenya wengi wakati hali ya maisha ikiendelea kuwa ngumu nchini Kenya.

Hii inaonyesha wazi kwamba uchumi wa Kenya ni uchumi wa makaratasi wakati Tanzania ndio nchi yenye uchumi wenye kuakisi ukweli.

Karibuni sana majirani katika nchi ya Maziwa na Asali.
 
Mimi ni Mtanzania, hata hivyo nimekuwa sipendezwi na threads za malumbano au ulinganishaji kati ya Tanzania na Kenya. Huu uzi ulipaswa kuwa ni wa kimichezo zaidi kuliko kisiasa. Michezo ni furaha, michezo huunganisha watu. Sisi sote ni ndugu, tunabaguana halafu eti tunapinga ubaguzi unaofanywa na watu wengine!
 
joto la jiwe,

Kwa EA Tanzania ndiyo inayolipa vizuri wachezaji, na ndiyo ligi bora kwa East Africa. Waliotuzidi ni congo pekee kwa central africa.

Hafu Tanzania kumbuka ndo nchi yenye mabilionea wengi zaidi hafu wapenda mpira. Utasugua sana kupata battle la kifedha kama la yanga na Simba kwa nchi maskini kama Kenya, Uganda na Rwanda.
 
Mimi ni Mtanzania, hata hivyo nimekuwa sipendezwi na threads za malumbano au ulinganishaji kati ya Tanzania na Kenya. Huu uzi ulipaswa kuwa ni wa kimichezo zaidi kuliko kisiasa. Michezo ni furaha, michezo huunganisha watu. Sisi sote ni ndugu, tunabaguana halafu eti tunapinga ubaguzi unaofanywa na watu wengine!
Hatulumbani, tunawaambia wakenya ukweli kuwa nchi yao na watu wao ni maskini sana wasijilinganishe na Tanzania
 
Sasa Kahata na wewe nani ana utajiri? Mwenzio amepata fursa, muache aitumie. Hata golikipa Ivo Mapunda aliondoka Tanzania akaenda kucheza Kenya
 
Kenya soka bado halija changamka japo kuna mashirikaa na makampuni mengi makubwa
 
Kuna watu mna kichaa Kama sio upuuzi kichwani. Kila Kitu mnaleta siasa mpaka kwenye michezo.

Mimi ni mtanzania ila huu upumbavu wa kubaguana sisi weusi wakati shida zimetujaa ni uchuro. Tubadirike.
Umesahau wakenya walivyowabagua watanzania kwa kuwafungia mipaka wasiende Kenya na kuzuia ndege za Tanzania kuingia Kenya huku wakiruhusu Wachina na wazungu wenye idadi kubwa ya Corona zaidi ya Tanzania?, wacha kujitia hamnazi, mpende anayekupenda, hapa ni "tit-for-tat.
 
Kwa EA Tanzania ndiyo inayolipa vizuri wachezaji, na ndiyo ligi bora kwa East Africa. Waliotuzidi ni congo pekee kwa central africa.

Hafu Tanzania kumbuka ndo nchi yenye mabilionea wengi zaidi hafu wapenda mpira. Utasugua sana kupata battle la kifedha kama la yanga na simba kwa nchi maskini kama Kenya, uganda na Rwanda.
Msikilize kahata
Utajua Kenya Ni Maneno tu
 
Mimi ni Mtanzania, hata hivyo nimekuwa sipendezwi na threads za malumbano au ulinganishaji kati ya Tanzania na Kenya. Huu uzi ulipaswa kuwa ni wa kimichezo zaidi kuliko kisiasa. Michezo ni furaha, michezo huunganisha watu. Sisi sote ni ndugu, tunabaguana halafu eti tunapinga ubaguzi unaofanywa na watu wengine!
Ndio maana kuna magroup mengi humu ukiona huku sio hobi yako unaweza kwenda hata kwenye urembo kule , umeingia mwenyewe ,umesoma habari mwenyewe hujalazimishwa na mtu halafu unalalamika kwani kuna group moja humu
 
Kwa hivyo TZ ni tajiri kushinda Kenya?
Kwa EA Tanzania ndiyo inayolipa vizuri wachezaji, na ndiyo ligi bora kwa East Africa. Waliotuzidi ni congo pekee kwa central africa.

Hafu Tanzania kumbuka ndo nchi yenye mabilionea wengi zaidi hafu wapenda mpira. Utasugua sana kupata battle la kifedha kama la yanga na simba kwa nchi maskini kama Kenya, uganda na Rwanda.
 
Kuna watu mna kichaa kama sio upuuzi kichwani. Kila kitu mnaleta siasa mpaka kwenye michezo.

Mimi ni Mtanzania ila huu upumbavu wa kubaguana sisi weusi wakati shida zimetujaa ni uchuro.

Tubadirike.
Kawaambia Nani mzungu hana shida?
 
Ndio maana kuna magroup mengi humu ukiona huku sio hobi yako unaweza kwenda hata kwenye urembo kule , umeingia mwenyewe ,umesoma habari mwenyewe hujalazimishwa na mtu halafu unalalamika kwani kuna group moja humu
Ni habari ya michezo lakini
 
Kwa hivyo TZ ni tajiri kushinda Kenya?
Tanzania uchumi wake upo mikononi mwa wa Tanzania na unawafikia watu wengi zaidi ya Kenya, Tanzania ina matajiri wengi ambao wamesambaa nchi nzima hadi vijijini, Kenya matajiri ni wachache na wengi huamisha pesa zao na kuziweka nchi za Ulaya na Marekani. Kenya uchumi wake upo mikononi mwa watu wachache sana hauwasaidii wananchi wa chini.
 
Back
Top Bottom