TANZIA Mchezaji wa Tenerife, Jesús de Miguel, afariki baada ya kugongana na kipa wa Andorra

TANZIA Mchezaji wa Tenerife, Jesús de Miguel, afariki baada ya kugongana na kipa wa Andorra

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mshambuliaji wa klabu ya CD Tenerife, Jesús de Miguel, amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kugongana na kipa wa klabu ya Andorra, Jesús Owono, wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la Pili nchini Hispania.

Klabu ya Tenerife imetangaza kifo cha mchezaji huyo kupitia taarifa iliyotolewa Jumanne, Novemba 3, 2026, ikieleza kuwa De Miguel alifariki saa 2:00 asubuhi (saa za Hispania).

Tukio hilo lilitokea Jumatatu wakati De Miguel, mwenye umri wa miaka 30, alipokuwa akipambana kuwania mpira katikati ya uwanja, kabla ya kugongwa kifuani na kipa Owono katika dakika za mwisho za mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Estadio Heliodoro Rodríguez López.

Baada ya tukio hilo, De Miguel alikimbizwa hospitalini kwa matibabu, huku mchezo huo uliokuwa ukielekea kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 ukisimamishwa katika dakika ya 108.

Baada ya taarifa ya kusikitisha ya straika wa Tenerife, Jesús de Miguel, kufariki dunia leo asubuhi kufuatia mgongano mkali na kipa wa Andorra, Jesús Owono katika mchezo wa LaLiga 2 uliochezwa Jumatatu.

Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) limetangaza kuahirishwa kwa michezo yote ya Copa del Rey na Copa de la Reina iliyokuwa imepangwa kuchezwa leo.
‎
‎Aidha, mchezo wa timu ya taifa ya Hispania U21 dhidi ya Japan pia umesimamishwa kufuatia tukio hilo la kusikitisha.Hata hivyo, michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) iliyopangwa kuchezwa nchini Hispania leo usiku inatarajiwa kuendelea kama ilivyopangwa.

ANDORA.jpeg




 
Mshambuliaji wa timu ya Tenerife, Jesus de Miguel, amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kugongana vibaya na kipa wa FC Andorra katika mchezo wa Ligi Daraja la Pili nchini Hispania.

De Miguel, mwenye umri wa miaka 30, alichezewa faulo katikati ya uwanja na kipa Jesus Owono, raia wa Guinea ya Ikweta, ambaye alikuwa ametoka langoni kwa kasi akijaribu kuondoa mpira.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mchezo uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez, huku timu hizo zikiwa sare ya mabao 2-2. Owono alionyeshwa kadi nyekundu na mchezo ulisitishwa na kuachwa kuendelea.

Vyombo vya habari vya Hispania viliripoti kuwa De Miguel alipata mshituko wa moyo (cardiac arrest) na alifanyiwa jitihada za kumrejesha katika hali ya kawaida. Mchezaji huyo alikimbizwa hospitalini na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Baadaye, klabu ya Tenerife ilitoa taarifa kuwa hali ya mchezaji huyo ilikuwa imezidi kuwa mbaya upande wa mfumo wa fahamu, kabla ya hatimaye kuthibitisha kifo chake.

"Nasikitika sana kwa kilichotokea. Pumzika kwa amani, Jesus," aliandika beki wa zamani wa Barcelona, Gerard Pique, ambaye ndiye mwanahisa mkuu wa klabu ya Andorra, kupitia mitandao ya kijamii.
 
Kifo huja kama masihara.

Ungemwambia marehemu ataweza kufa kifo chepesi kama hicho (yaani kufa akifanya kile alikuwa akikifanya siku zote bila shida) asingekuelewa na hii hata tulio hai leo tukiambiwa tunachokifanya kinaweza kuwa njia ya kutokea hapa duniani tunaweza kukataa but ndiyo ukweli wenyewe.
 
Halafu kipa aliyecheza faulo hata hakuwa na muda wa kumuangalia mwenzake kujua hali yake
 
Back
Top Bottom