Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Nicklas Bendtner ahukumiwa kwenda jela

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Nicklas Bendtner ahukumiwa kwenda jela

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Denmark mwenye miaka 30 amehukumiwa kifungo cha siku 50 baada ya kupatikana na hatia ya kumdhalilisha mwendesha 'taxi' katika Mahakama ya mji wa Copenhagen

Hata hivyo kwa mujibu wa Wakili wake, Bendtner anayechezea klabu ya nchini Norway ya Rosenborg hajaenda jela akisubiri uamuzi wa rufaa aliyokata

Kwa mujibu wa ushahidi wa video, Bendtner anaonekana akimpiga usoni dereva huyo baada ya kubishana ni njia gani dereva huyo alitakiwa kuelekea

Bendtner alikubali makosa hayo ya kumpiga dereva lakini alisema ni baada ya kuhisi kutishiwa kutokana na derwva huyo kumrushia chupa walipoondoka bila kulipa
IMG_20181102_204209_770.jpeg
 
Back
Top Bottom