Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Damian Mrisho Kimti aliyekuwa akicheza katika nafasi ya ushambuliaji wa pembeni (Winger), alisifika kwa uwezo mkubwa wa kupiga chenga, mashuti makali na umahiri mkubwa wa kupachika mabao
Alikuwepo katika kikosi cha Simba kilichocheza fainali ya Kombe la CAF dhidi ya Stella Abidjan mnamo Novemba 29, 1993 katika Uwanja wa Uhuru, ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa goli 2-0
Baada ya kustaafu kucheza soka la ushindani, alikuwa akijishughulisha na kazi ya ualimu akifundisha somo la Kifaransa katika shule mbalimbali ikiwemo St. Mery ya Tabata
Kikosi cha Simba kilichotamba katika michuano hiyo ya Kombe la CAF mwaka 1993 chini ya Mfadhili Mkuu, Azim Dewji kilihusisha Wachezaji Kasongo Athumani, David Mihambo, Michael Paul ‘Nylon’, Twaha Hamidu na Mavumbi Omar
Wengine ni Often Martin, George Lucas ‘Gazza’, Mbuyi Yondan, Suleiman Pembe, Ramadhani Lenny, Edward Chumila, Hussein Marsha na Mwameja Mohammed
Aidha, alikuwepo Duwa Said (Hakucheza michuano hiyo kwa sababu hakusajiliwa alikuwa anacheza Ligi ya Tanzania Bara pekee), Iddi Selemani ‘Meya’, Damian Kimti na Deo Mkuki