MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Mchezo dhidi ya Uganda kesho ni mgumu mno. Uganda wamekuwa na trend ya kutufunga mfululizo na yumkini hata mchezo uliopita hawakutegemea surprises za kocha wetu mpya na hawakutegemea kupoteza kwetu.
Kucheza na mabeki wa kati 3 na viungo wa asili wa kuzuia 4 ulikuwa ukuta mgumu sana sana kuuvunja! Kocha Micho mwenyewe amekiri kukutana na mabeki na viungo wagumu mno kuliko alivyotarajia.
Sasa tukienda na matokeo yaliyopita mfukoni tukakosa nidhamu tutaadhibiwa vibaya. Kocha Micho kwenye press amegusia kuandaa timu yake kucheza na ule ukuta wa Berlin au plan ya kucheza na akina Kapombe na Tshabalala.
Kocha wetu arudi na approach ile ile ya viungo wengi lakini alainishe kidogo ili boli litembee. Toa Mudathiri weka Feisal na toa Himid Mao weka Bajana! Kwingine kubaki vile vile.
Hatari ninayonusa ni kama tukiamua kupishana na Uganda ambao wana nguvu na mchanganyiko mzuri wa wakongwe na vijana watatuadhibu.
Kocha awatumie Kapombe na Tshabalala ikiwa tumepoteza na tunahitaji kusaka magoli lakini kinidhamu na kushambulia kwa ghafla timu ibakie vile vile na mabadiliko kidogo kama nilivyopendekeza.
Kila lakheri National Team [emoji1241]
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app