Mchezo dhidi ya Uganda kesho, Tusiende na matokeo mfukoni!

Mchezo dhidi ya Uganda kesho, Tusiende na matokeo mfukoni!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Mchezo dhidi ya Uganda kesho ni mgumu mno. Uganda wamekuwa na trend ya kutufunga mfululizo na yumkini hata mchezo uliopita hawakutegemea surprises za kocha wetu mpya na hawakutegemea kupoteza kwetu.

Kucheza na mabeki wa kati 3 na viungo wa asili wa kuzuia 4 ulikuwa ukuta mgumu sana sana kuuvunja! Kocha Micho mwenyewe amekiri kukutana na mabeki na viungo wagumu mno kuliko alivyotarajia.

Sasa tukienda na matokeo yaliyopita mfukoni tukakosa nidhamu tutaadhibiwa vibaya. Kocha Micho kwenye press amegusia kuandaa timu yake kucheza na ule ukuta wa Berlin au plan ya kucheza na akina Kapombe na Tshabalala.

Kocha wetu arudi na approach ile ile ya viungo wengi lakini alainishe kidogo ili boli litembee. Toa Mudathiri weka Feisal na toa Himid Mao weka Bajana! Kwingine kubaki vile vile.

Hatari ninayonusa ni kama tukiamua kupishana na Uganda ambao wana nguvu na mchanganyiko mzuri wa wakongwe na vijana watatuadhibu.

Kocha awatumie Kapombe na Tshabalala ikiwa tumepoteza na tunahitaji kusaka magoli lakini kinidhamu na kushambulia kwa ghafla timu ibakie vile vile na mabadiliko kidogo kama nilivyopendekeza.

Kila lakheri National Team [emoji1241]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Waganda ni wazuri kwa mipira ya juu kwasababu wana nguvu, mipira ya kona, free kicks ni wapiga vichwa wazuri sana, hapo kwanza tujue namna ya kuwatuliza..

Kisha kwa maoni yangu, tukifanikiwa kwenye hilo, tofauti nawe mleta mada unavyofikiria, mimi siogopi kupishana na waganda kwa kuweka mpira chini, hawana speed kutuzidi, tuko vizuri kwenye hilo.
 
Naiona mechi ikiwa nzuri Sanaa, kwasababu Uganda nao najua wanataka matokeo aidha wacheze( wamiliki) au watumie mbinu hapo naamini kutakuwa na burudani.
 
Nyie Simba hamna maajabu. Kapombe na Tshabalala ni uchochoro wanapigwa matobo TU pelekeni wakaivae Raja , Taifa Stars SiO Kwa tena. Timu ni Ile Ile iliyoshinda Kwa kawaida timu inayoshinda Huwa haibadilishwi. Acheni miluzi mingi ya kumpoteza kocha
 
Timu ibaki vilevile, kutaka kuibadilisha bila kujua mwenzako anakujaje ni unprofessional.

Mwache kocha wa Uganda aendelee kutafuta jawabu la maswali aliyo ulizwa, ikionekana amekuja na kutuzidi basi kocha wetu abadilishe mbinu au wachezaji.
 
Mimi kesho nahamia Uganda, una kikosi kimekupa ushindi ila kwa sababu ya shinikizo unaamua kuwaita kikosini wachezaji ambao hukuwaamini mwanzo.
 
Cha msingi ni kutambua tu kwamba hiyo ni Taifa stars na sio simba
 
Nyie Simba hamna maajabu. Kapombe na Tshabalala ni uchochoro wanapigwa matobo TU pelekeni wakaivae Raja , Taifa Stars SiO Kwa tena. Timu ni Ile Ile iliyoshinda Kwa kawaida timu inayoshinda Huwa haibadilishwi. Acheni miluzi mingi ya kumpoteza kocha
Pombe ziki kata njoo tuichambue stars kaka

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Mchezo dhidi ya Uganda kesho ni mgumu mno. Uganda wamekuwa na trend ya kutufunga mfululizo na yumkini hata mchezo uliopita hawakutegemea surprises za kocha wetu mpya na hawakutegemea kupoteza kwetu...
Naiona Taifa stars atapandia The Cranes kufuzu AFCON kama Simba alivyopamdia kwa Vipers kufuzu robo fainali
 
1.Manula
2.Kapombe
3.Zimbwe
4.Job
5.Bacca
6.Mzamiru
7.Msuva
8.Miroshi
9.Samatta
10.Fei Toto
11.Sop

Ningekuwa Kocha..ningeanza na jeshi hili leo
 
Hapa duniani kuna timu unaweza kuziwekea dhamana! Ila siyo Taifa Stars.
 
Kocha wetu muoga sana! Sub mbovu na muda usio sahihi. Central back watatu na typical viungo wakabaji utegemee nini! Hiyo inafaa away lakini Taifa angelainisha timu kidogo.

Bajana anaweza kukaba na kucheza, Feisal anaweza kukaba na kucheza! Huwezi kuwa home alafu unajaza Central back namna ile. Ni dalili za uoga na udhaifu kimbinu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Mchezo dhidi ya Uganda kesho ni mgumu mno. Uganda wamekuwa na trend ya kutufunga mfululizo na yumkini hata mchezo uliopita hawakutegemea surprises za kocha wetu mpya na hawakutegemea kupoteza kwetu.

Kucheza na mabeki wa kati 3 na viungo wa asili wa kuzuia 4 ulikuwa ukuta mgumu sana sana kuuvunja! Kocha Micho mwenyewe amekiri kukutana na mabeki na viungo wagumu mno kuliko alivyotarajia.

Sasa tukienda na matokeo yaliyopita mfukoni tukakosa nidhamu tutaadhibiwa vibaya. Kocha Micho kwenye press amegusia kuandaa timu yake kucheza na ule ukuta wa Berlin au plan ya kucheza na akina Kapombe na Tshabalala.

Kocha wetu arudi na approach ile ile ya viungo wengi lakini alainishe kidogo ili boli litembee. Toa Mudathiri weka Feisal na toa Himid Mao weka Bajana! Kwingine kubaki vile vile.

Hatari ninayonusa ni kama tukiamua kupishana na Uganda ambao wana nguvu na mchanganyiko mzuri wa wakongwe na vijana watatuadhibu.

Kocha awatumie Kapombe na Tshabalala ikiwa tumepoteza na tunahitaji kusaka magoli lakini kinidhamu na kushambulia kwa ghafla timu ibakie vile vile na mabadiliko kidogo kama nilivyopendekeza.

Kila lakheri National Team [emoji1241]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Ulikuea mbele ya muda mkuu...hongera mkuu
 
Back
Top Bottom