kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Kuna wakati sisi mashabiki wa Yanga tunatabiri sijui hawa watakufa 1 au mbili huko kwao, ila ukiangalia vizuri hawa Al Hilal japo siyo bora zaidi yetu, wao wana viongozi wazoefu kwenye mashindano haya.
Tutoke uko twende kwenye ufundi, hawa Al Hilal wakituchezea mipira ya juu kwa beki zetu zile na vimo vyao ni Mungu na maombi. Nilikuwa naona walivyokuwa wanapata shida ya kushinda mipira ya juu.
Pia Al Hilal mashambulizi yao mengi yanatoka pembeni sana, kwa hiyo naomba beki zetu wa pembeni wawe makini sana. Ikiwezekana wakabe "Batle kwa batle" yaani mtu kwa mtu siyo wampe nafasi ya kukimbia. Mawinga wa Al Hilal wana mbio sana kuzidi mabeki wetu.
Kwahiyo tukiwazuia huku tutakuwa tumeshinda mchezo. Kuhusu washambuliaji wetu sina mashaka, naona sura ya Fiston inaonesha hawa Al Hilal watafungwa tu, tatizo ni ulinzi wetu.