Mchezo umeisha! Msumbiji huru sasa

Ukitaka kujua Kagame anaogopa Tanzania fuatilia siasa zake enzi za Magufuli.
Halafu watu wasichokijua huyo jamaa hana miaka 5 ataondoka kwenye hicho kiti tatizo je Rwanda itabaki salama? wahutu nao wanakula timing.
Kama Kagame ana akili ajitahidi kuleta biashara Tanzania kama Museveni alivyofanya (bomba la mafuta) ili moto ukiwaka tuwasaidie kwasababu za kiuchumi.
 
Kuna vijana ambao hawakupita JKT hapa wanaisifu Rwanda. Mjomba! Hakuna kiumbe yoyote anaweza tishia Tanzania. Na sio kwa vita tuu mpaka kisiasa. Tanzania ndiye imekomboa nchi nyingi za Afrika na itabaki kuwa hivyo.

Halafu naona wengi wanaoisifu Rwanda ni wale wa katiba mpya. Tulieni nyie
 
Kwanza kabisa rwanda hawana ndege za kijeshi vifaru havifiki hata 50 .tanzania ndani ya mwaka huu tumeagiza zaidi ya vifaru 25 kutoka urusi pia kuna pantsir air defense kama mbili zilipita eneo la msamvu morogoro nimepata tete tanzani tuna ndege za mig 29.tanzania drone za tech rahisi tunazo
 
USILETE SIASA KWENYE MAMBO YA JESHI. KATIBA MPYA ITAPATIKANA NA JWTZ NI BORA NA ITAKUWA BORA DAIMA.
 
Umeisahau Kenya
Unajua mkuu tukizungumzia drones ni term moja kubwa mno. Kuna drone hadi unaishika kwa mkono mmoja na kuirusha, ila kuna drone zina tani 7+ zinaruka na kukaa hewani masaa 26+. Drones za kufanya strikes kama hizi Predator zinauzwa bei ghali au hata surveillance drones kama Global Hawk zina bei sana. Hata MALE zina bei.

Sasa ukileta hizi kama Bairaktar za Uturuki hata sisi tunaweza jiumiza tukazimiliki ila kununua capable drones ni mlolongo mrefu. Na tatizo operating cost huwa ni kubwa. Bado training ni ndefu sana.

Provided jamaa kadokeza kuwa Rwanda alipewa drones na France alafu akaja vitani. Hizo zitakuwa ni vile vya kurusha kutoka kwenye arresting system. Kazi kubwa ni kupoint adui yuko wapi kwa camera, kisha mnamfata. Vina limited range. Hivo havitishi jeshi la nchi, yeyote anaagiza leo anajifunza kwa wiki kisha anatumia vitani. Hata Kenya kuwa navyo sio ajabu
 
Mkuu tutulie kwanza hapa. Naomba unipe tetesi hizo kwangu ni mpya.

Pantsir ndio iliyotajwa ile siku wanazindua kambi ya Morogoro Gen. Mabeyo akajichanganya kwenye speech akatoa siri. Sikuwahi sikia speech sijui walizitoa kwenye YouTube channels ila niliposoma kwamba kataja mifumo ya ulinzi, akili ya kawaida na shauku ikanituma niamini ni Pantsir. Kama ni kweli wamechukua chaguo sahihi kwa short range air defense

Hivyo vifaru kutoka Russia ni type gani. Naamini hatuwezi afford T-90 wala T-72 kirahisi. I bet ni modified T-64 ambazo ni outdated sasa. Kama tetesi zako ni sahihi, tulikuwa na option ya kuongeza Type 59 tulizonunua China ambazo somehow ziko vizuri kwa level yetu. Tanzania kiukweli kwenye vifaru tuko nyuma ila inventory huwa zinapigana gap. This time mfano Kenya wakinunua vifaru bora zaidi tunakuwa na vifaru inferior, next time tukiagiza vinakuwa superior. Hivo yani

Hizo boats ulizopost chini ya hii naona kama ni patrol boats unajua ni class gani. Hizi ndio zinazuia magaidi, wavuvi haramu na wauza madawa

Alafu siamini kama tuna uwezo wa kumiliki Mig-29. Gharama ya kununua tutajibana ila operating costs ni kubwa. Hata tukichukua units zitakuwa kidogo. India wana uzoefu nazo sana wanaweza tusaidia katika hili. Ila tunaweza opt kwa J-17 za China & Pakistan, naamini tunaziweza

Ila Tanzania inachukua silaha kimyakimya. Ni rahisi nikajua Kenya ina nini ila nikija kwetu nahangaika siambulii kitu
 
Sisi ndio Bahima empire kasome hiyo kwanza. Ndio utajua tumepenyeza Hadi sehemu gani ya East Africa.
Hamna kitu mnajisifia Sana Sisi nyie tunawatumia kuruta Tu wanawatosha [emoji23][emoji23][emoji23]watoto tuliowalea wenyewe hamtutishi.Tanzania mlikuja si Kwa sababu ya ukimbizi alafu tunawajua vizuri[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Rwanda wako kwenye ubora wao in term of military Power... Tuliwachokoza siku moja watatukojoza saana.
JK aliwachapa vizuri tu mwishoni mwa utawala wake, usilinganishe Rwanda na Tanzania kaka, watakucheka watu.
Kwa mtazamo wangu, kibiashara, Msumbiji ikiwa haina AMANI, Tanzania inafanya biashara vizuri zaidi kwa maana ya kupunguza upinzani wa bandari, huenda ndio sababu Tanzania haikupeleka jeshi huko, just thinking loudly.
 
We jamaa unaiongelea Rwanda ipi wewe? Hivi unajua miongoni mwa watu walikua wanaomba Mungu JK aondoke madarakani HARAKA, PK nae ni miongoni mwao? Unaikumbuka ile vita ya maneno kati ya JK na Kagame kule Ethiopia? JK alihutubia in a very polite language, Kagame akiwa anaaga jeshi kwenda zake ziara sijui ilikua Japan (uzi huo upo humu ) ali talk shit balaa kutuhusu, JK akaomba game Congo pale, unajua majeshi ya M23 yalikua ni muungano wa Uganda na Rwanda, walipigwa wale watu hadi wakaomba poo, Magufuli alivyoingia akawa na mtazamo tofauti; narudia, unaiongolea Rwanda ipi? Huenda sisi hatukupeleka majeshi Msumbiji kwasababu za kibaishara na sio kuwaogopa magaidi. Tulipigana na serikali ya makaburu kule kule Msumbiji, usicheze na bongo yaani
 
Ni muda mrefu sasa tumekuwa tukishuhudia mijadala mingi kuhusu kufananisha uwezo wa kijeshi kati ya tz na rwanda..na sijui ni kwa nini. Huenda kile kipindi cha jk ndo kimesababisha haya mana zilitaka zichapweee..huenda zikachapwaa siku moja lets keep watching. But mind you guys, being a little country geographically, doesn't make it to be inferior in millitary perspective, same applies to large country geographically. What it takes for a country to be superior is all about war tactics, level of military intelligence, the technological advancements in the arsenal, millitary equipments, economy and the likes.
So beware especially tz, we always drug things to our side. Our millitary should be (if not yet) transformed from conventional to more advanced system to combat any challenge from everywhere..
Refer to japan and china..then and now? Japan dominated china despite its size. But what about now? You have your answer.
What about britain?? And the very sound example is the political insrael they dominate middle east though some says they have been backed up by supper power(USA and EU).
 
Kipi kati ya ulivyotaja hapo Rwanda inaizidi Tanzania. Technology? Tactics? Weapons? Military intelligence?

Geographical size and terrain matters. You have various references, Operation Barbarossa between Nazi Germany & Red Army, Iran- Iraq war

Unaitumia China na Japan kama comparison, Japan at the time was superpower na China ilikuwa maskini wakutupwa ikiwa na utapiamlo na haina organized government. Sasa kwani Rwanda ni superpower au Tanzania iko disorganized

Case ya Israel ni special kabisa. Nchi gani nyingine duniani ambayo UN iliwapa eneo la kukaa tofauti na Israel, nchi gani nyingine ilitafitutiwa eneo la kukaa na mkoloni wa hilo eneo. Israel ilipobanwa mbavu na Egypt kwenye Yom Kippur war, sorties za allies zikaanza kushusha silaha ambazo hata hawakununua walipewa bure. Israel na Rwanda haviendani, Rwanda ni kanchi kanakolindwa kwa mtutu muda wowote Kagame akiondoka wanapigana tena
 
hiyo pantsir na mig 29 zimenunuliwa lin ?
 
Ila Tanzania tulikuwa na propaganda Mara tunaongoza kwa Vita ya chini Duniani!?

Mara sisi Ni wa pili Duniani kwa intelligensia. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Enzi za Mwl it was funny.
Una umri gani? Hizo picha zote sijaona mapigano sehemu yoyote zaidi ya show off ya vigali vichache, unajua tukipeleka platoon moja tu iliyotoka Congo na zana zake utajikojolea?
 
Wewe ni mwanajeshi au mwanasiasa au Mwana si hasa?
Tafuta habari za ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…