Mchezo wa ngumi ni wa kupigwa marufuku duniani

Mchezo wa ngumi ni wa kupigwa marufuku duniani

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Huu mchezo sio kabisa na hata kuita mchezo ni makosa kabisa. Watu wanaumizana huku wengine wanashangilia halafu eti unaitwa mchezo.

Najua ngumi ni biashara kubwa duniani na ni ajira kwa watu wengi ukiacha mabondia wenyewe, ila ukweli unabaki pale pale kuwa huu mchezo haufai kabisa.

Bahati mbaya na wanawake nao eti wanapigana kama tunavyoona muda huu kupitia Azam tv.

Hivi hata Mungu si hataki mambo haya?
 
Huyu fadhili majiha atamuua huyu babu wa South Afrika.

Kamuelemea saana japo kwenye ngumi kosa moja mchezo umeisha, awe makini
 
Huyu fadhili majiha atamuua huyu babu wa south afrika.
Kamuelemea saana japo kwenye ngumi kosa moja mchezo umeisha, awe makini
Mahlangu sio mnyonge mkuu, ana balaa huyo usiongee sana subiri pambano liishe, Fadhili awe makin.
 
Mahlangu sio mnyonge mkuu, ana balaa huyo usiongee sana subiri pambano liishe, Fadhili awe makin.
Sijasema ni mnyonge ni bondia mzuri, nazungumzia kipindi kile hali ilivyo, baadae bongani kabadilika na majiha kuna kazingua alijifanya anamuweza kibabu.

Game nzuri, hili pambano hata kama ingekuwa ni saa 8 za usiku bado lina hadhi ya kuuchukua usingizi wangu.
 
Back
Top Bottom