Mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida Fountain Gate tutegemee kuona makosa ya kibinadamu kutoka kwa marefa

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kutokana na kutumika nguvu kubwa na Figisu ili mradi tu lastborn wa TFF achukue kombe/au kuanza vizuri msimu ili arudishe unafuu na Imani kwa mashabiki zake.

Muundo wa timu nne na kuichezesha Yanga na Azam huku kukiwa na imani kubwa kuwa Yanga atapigwa lakini imekuwa ndivyo sivyo, kipigo kitakatifu kimemkuta Azam Fc.

Limeibuka kundi la wahuni/mashabiki wa Simba sc wanaanza kuilaumu Azam na kuikejeli huku wakisahau kuwa Azam Fc kakutana na bingwa aliyecheza fainali ya shirikikisho, hapo hapo wakasahu kuwa Yanga sc ndiyo bingwa mtetezi wa ngao ya jamii, kombe la Nbcpl na FA.

Kiufupi Azam Fc asilaumiwe kwa kuwa kakutana na Bingwa Hilo halina ubishi na anastahili sifa kwa uwezo aliounesha wa kupunguza magoli.

Achana na Goli la Aziz key, Wala usiulize kuhusu Clement mzize mtoto aliyepata baraka pale ikulu kutoka kwa Mh Raisi Samia suluhu kwa kutambulishwa.

Mchezo wa Singida fountain Gate na Simba leo wachezaji wa Singida watapewa kadi za njano nyingi mpaka kupelekea kadi nyekundu ili mradi tu Simba sc afike fainali.

Nawasilisha hoja.
 
Kwa Nini mnamdhaaki Azam kufungwa na Yanga wakati wakati mnaitaka yanga
Wote wamecheza kiwango cha chini, yeyote ambaye angeshinda angekuja kupoteza kwa Simba, labda kama kuna kikosi kingine cha kizuri zaidi ya vilivyocheza
 
Reactions: BRN
acha uoga moyoni mwako unajua kabisa unatamani kukutana na nani , hakuna jambo rahisi tunakuja tuna haja na Yanga.
 
Reactions: BRN
Azam na Yanga ilikuwa Ni mikamiano tu mpaka kocha wa Yanga alivyoamua kubadilsha mchezo kwa wachezaji wake wanapata magoli.
 
Bongo raha sana
Simba wakishinda watakuwa wamebebwa
Wakishindwa ni Simba mbovu

Alieanzisha Simba na yanga Ana akili sana
Katuachia vitu viwili vichafu na vibovu sana.Kila timu lazimu ifungwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…