Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Kichwa chake hakiwezi kuwaka Moto maana si mgeni wa kushika pesa hivyo tusimpangie matumizi.
Tatizo watu wanakuja ku comment uku bila kusoma comment
Ishasemwa jamaa ni billionaire kitambo sas watu wanadhan ni mgen wa hela
 
hongera kubwa kwake...sasa walio karibu naye wamshauri aajiri wataalamu wabobezi wa maswala ya biashara na uchumi ili wamshauri na kumsimamia namna sahihi ya kuwekeza ili abaki kuwa juu yeye na kizazi chake forever.
Duuuh
 
Mng'ato, hebu fuatilia sualala huyu mchimbaji mdogo na namna alivyo - hustle for nine years hadi alipotoboa juzi! Huna haja ya kusaidiwa na Serikali pale unapoweza, ila pale parefu then kuna haja ya mkono wa Serikali. Hilo la kulisha wana Apolo wake ameliweza ndio chanzo cha hayo mafanikio. Ila itakapokuja kwenye uwekezaji MZITO wa huyu mchimbaji mdogo, nashauri yeye aihusishe Serikali ili imusaidie.
Jombi acha story za redio mbao huyo katoboa kitambo,anamiliki mall kubwa plus majumba...huyo mgodi miundo mbinu inazidi bilioni halafu unasema ametoboa
 
National museum wailinde vizuri haki ya nani huu mzigo unavutia wezi wenye akili.TRUST ME
 
Watu humu Kweli wageni hawajui Maisha halisi ya watu hko au watu wa madini
Sasa mtaalam wa biashara na uchumi wapi na wapi
Mtu Ana degree ya biashara wkt hajawahi kufanya hata biashara ya genge

Ova
Mtu unanunua mountmeru hotel kwa 30bn huna mkopo wowote huyu tutamwita nae kapata pesa awamu ya covid-19.laizer kwenye top ten ya wamiliki wa migodi yupo kitambo sio leo alikua na wachina ndio wamekata huo mgodi umetoa mawe sana 2013 na 2014 mpka kujenga hiyo mall na kununua majumba mjini
 
mount meru ni yake ?!
 
Mkuu iyo bei nzuri unayoizungumzia ilikua kabla ya covid-19 kwa Sasa uchumi umeyumba dunia nzima.tusipinge kila kitu mengine ni mambo mazuri ebu tuwapongeze VIONGOZI wetu ,tuwatie moyo waendelee kutupigania watanzania ili tuyafikie maisha bora.
Tanzanite zio chakula useme kitaharibika.

Hata miaka 10 ijayo watu watanunua na kuhifadhi.

Wawekezaji wengi watanunua kwa bei nzuri.
 
Jombi acha story za redio mbao huyo katoboa kitambo,anamiliki mall kubwa plus majumba...huyo mgodi miundo mbinu inazidi bilioni halafu unasema ametoboa
Mkuu watu wengine ni kuwaacha tu walivyo na ujuaji wao.....huko Pang'alu alipo akisikia laizer ni mchimbaji mdogo basi anajua jamaa anatumia sururu na mundu kuchimba hayo madini akichoka anabeba sururu yake begani analudi nyumbani na kidumu cha maji mkononi.
 
Nikiangalia structure ya hili jiwe, inawezekana alichoonesha ni sehem tu ya alichopata. Hili jiwe ni kubwa sana achunguzwe ameficha zaid ya nusu yake.

Kuna watu nilikuwa nawambia Swala kama hili mkuu wakawa wanabisha,hili niwe linaonekana lilikuwa kubwaa,jamaa kaficha vipande kadhaa,Kwa utaratibu wa govment yetu nani Wa kutoa Mzigo wote,Jamaa sio fala kiivyo.
 
Back
Top Bottom