Mchina jela miezi mitano kwa kuua tembo 511, Mtanzania jela miaka 60 kwa kukutwa na meno ya tembo na kiboko

Mchina jela miezi mitano kwa kuua tembo 511, Mtanzania jela miaka 60 kwa kukutwa na meno ya tembo na kiboko

Baadhi ya mahakama za Tanzania zinawapendelea sana wageni kuliko raia wake.

Soma hiyo habari chini utaona jinsi raia wa Tanzania wanavyo hukumiwa kifungo tofauti na raia wa nje ya Tanzania. Ni uonevu wa hali ya juu mahakama zetu.

ceb5f65a-c194-42b7-b267-abed5bfd3f3e.jpg
 
Mahakama ya Tz kama Tz..

Ussssssshuzi mtupu..

Double standard at it best
 
....Raia wa kigeni anamlazimisha dada wa kitanzania (lady of the nite )ku sex na mbwa, raia huyu anakamatwa na kuwekwa pale osterbay police station ofisini sio self, baada ya siku mbili au tatu anarudishwa kwao Ulaya, dada yetu anapewa onyo kali to shut her mouth na case inakua cold one.....,mambo haya tuna historia nayo kama taifa, as far as hakuna push back yataendelea.
 
Nimeona hii habari mtandaoni imenishangaza kama sio kosa la kiuandishi.Raia wa China amekutwa na kosa la kuua jumla ya tembo 511 wenye dhamani ya bilioni 7 amehukumiwa jela miezi mitano au kulipa faini ya laki tatu.

Kwa upande mwingine Mtanzania aliyekutwa na meno yenye dhamani ya milioni sitini na tisa kalambwa miaka 60

Wadau wa sheria tusaidieni hapa!

View attachment 2449142
Wachina ni marafiki zetu na wanatupa misaada.
 
Ni mpumbavu tu, atakaye weza kuelewa huu uwozo. Sheria ni msumeno inatakiwa ikate pande zote.
Shida ni sisi kwa sisi hatupendani. Tunathamini wageni kuliko wazawa hakika hii ni Sheria kandamizi inapaswa kuangaliwa upya.

Sheria Duniani bali Haki Mbinguni
Mafyatu pekee wataelewa mkuu,
Anyway let black be black
 
Mkuu nadhani "unatuchora", maana nakumbuka uliwahi kukiri kuwa mlienda vilingeni usiku na Mchana kuzuia aliyekuwa anapigana kuondoa hivyo vijiko vitatu ili asali ifike chini kutoka juu moja kwa moja!!
 
Adui mkubwa kuliko wote wa mwafrika ni umasikini wa fikra wake binafsi na wenzake pia.
Maamuzi ya baadhi ya viongozi na watumishi wa uma yana changamoto sana.
 
ndio maana viongozi wanawapa uraia watoto nchi za ulaya.wameona mbali.
mkiambiwa nyie mbuzi mnakuja kumuwakia lisu na mbowe. ndio haki yenu
 
Baadhi ya mahakama za Tanzania zinawapendelea sana wageni kuliko raia wake.

Soma hiyo habari chini utaona jinsi raia wa Tanzania wanavyo hukumiwa kifungo tofauti na raisa wanje ya Tanzania. Ni uonevu wa hali ya juu mahakama zetu.

View attachment 2449462
Raia wa kigeni wanalipa faini, polisi na hakimu. Mtz mwenzangu, hana pesa!
 
Raia wa kigeni wanalipa faini, polisi na hakimu. Mtz mwenzangu, hana pesa!
Raia wa nje wanalipa faini au wanatoa rushwa kwa vyombo husika?Huyo mchina amelitia hasara Taifa kwa gharama ya shilingi Billioni 7 Hakimu anamtoza Faini ya shilingi Millioni 50 na laki 3 iweje? Je Wakati huyo M-Tanzania Amekutwa na meno ya Tembo yenye Thamani ya shilingi Milioni 69.5. Amehukumiwa jela Miaka 60 hapo kweli kuna haki imetendeka ?
 
Mamlaka husika zijitafakari na Mahakama ifanye kazi kwa weledi.Thamani ya tembo Ni billion 7 , halafu Hakimu au DPP anakubali fidia ya milioni 50,wapi na wapi.
Hapo hakuna fidia,bali hasara ya hizo bilioni.
Pili hukumu haisemi, hizo pembe za tembo kama zimetaifishwa au kuteketezwa.
DPP ana Mamlaka makubwa sana na ndiyo unapokuja umuhimu wa Katiba Mpya.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nachokijua.

Watanzania wengine hupoteza kujiamini mbele ya Ngozi nyeupe (Mzungu, Mchina, Mwarabu, Mhindi nk) na ngozi nyeupe inajua hilo!

Pia, Wapo Watanzania wanapenda kuwashobokea wageni (Foreigners) wanapokuja Tanzania. Na hao Watanzania wapo tayari kushirikiana na wageni na kuwapa njia za kupita wawapo hapa Tanzania ili wafanikishe mambo yao!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mamlaka husika zijitafakari na Mahakama ifanye kazi kwa weledi.Thamani ya tembo Ni billion 7 , halafu Hakimu au DPP anakubali fidia ya milioni 50,wapi na wapi.
Hapo hakuna fidia,bali hasara ya hizo bilioni.
Pili hukumu haisemi, hizo pembe za tembo kama zimetaifishwa au kuteketezwa.
DPP ana Mamlaka makubwa sana na ndiyo unapokuja umuhimu wa Katiba Mpya.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app

bageni ya DPP kipindi cha JPM ndio matunda yake.mkopo tutalipaje.
 
Nimeona hii habari mtandaoni imenishangaza kama sio kosa la kiuandishi.Raia wa China amekutwa na kosa la kuua jumla ya tembo 511 wenye dhamani ya bilioni 7 amehukumiwa jela miezi mitano au kulipa faini ya laki tatu.

Kwa upande mwingine Mtanzania aliyekutwa na meno yenye dhamani ya milioni sitini na tisa kalambwa miaka 60

Wadau wa sheria tusaidieni hapa!

View attachment 2449142

Kaua tembo 511?????
Hii namba.
 
na mfundisha mwanangu kuiba bilioni sio elfu kumi.ndio ccm inatufundisha maana ukiiba bilioni kesi yako inakuwa ya J4 wa mwanza
Akikamatwa anapigwa miaka 60 na kazi ngumu iwe mfano kwa wengine alafu wanakandamizia kabisa kwamba alipaswa kuwa mzalendo kwa rasilimali za Taifa kwa maslahi mapana ya wananchi wote.

Lakini J4 si alimtungua mtu na pistol sio wizi (alafu jana nimeona taarifa ya habari ameachiwa huru japo amekamatwa tena)
 
Back
Top Bottom