Siku za karibuni katika mtandao wa Whatsapp na Twitter imekuwa ikisambaa picha iliyounganishwa ikionesha hukumu za matukio mawili yanayohusisha watuhumiwa waliokamatwa na nyara za serikali (Meno ya tembo).
Ya kwanza ni taarifa ya Disemba 16 2019 inayomhusu Bi Haika Mgao na inasomeka:
"Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu, Haika Mgao (26) kutumikia kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno ya tembo na ya kiboko yenye thamani ya Shilingi milioni 69.5, mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
View attachment 2449815
Ya pili ni ya tarehe 15 Disemba 2019 inamhusu Rais wa China China, Liang Hu na inasomeka:
"Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu raia wa China, Liang Hu kulipa fidia TZS 50 milioni kwa kosa la kuua tembo 511 wenye thamani ya TZS 7 bilioni. Pia alitakiwa kulipa faini TZS 300,000 au kifungo cha miezi mitano jela. Mtuhumiwa aliandika barua kwa DPP kukiri makosa yake."
View attachment 2449819
Matukio yote mawili ni ya mwaka 2019 na hukumu zake zilipishana siku tano tu, tena ikianza ile ya raia wa kigeni kisha ikafuata ya binti wa miaka 26 tu.
"Wakati tunapiga kelele kusema alikuwa ra**s wa wanyonge tukumbuke alimfunga miaka 60 binti wa miaka 26 kisha akamuachia huru kinara na malkia wa mauaji wa tembo aliyeua tembo zaidi ya 510"