mahakama ya kazi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2013
- 1,520
- 241
Raia wa China,Xu Wenze (29) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Mpanda akikabiliwa na tuhuma za kukamatwa na meno matatu ya fisi.Mwendesha mashitaka wa hifadhi ya wanyamapori ya mbuga ya Taifa ya Katavi,Pele Malima,alidai mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi Chiganga Tengwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo januari 3 mwaka huu,majira ya saa 6 mchana.Alidai raia huyo wa China ambaye anatengeneza barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mpanda kuelekea Sitalike,alikamatwa na meno hayo matatu wakati akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda muda mfupi kabda ya kupanda ndege kuelekea mjini Mwanza.Mtuhumiwa alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana ya shilingi milioni tano.Kesi itatajwa Aprili mwaka huu.
source;gazeti la tanzania daima.
ILA WADAU HIZI KAMPUNI ZA BARABARA ZINAIBA SANA MALIASILI ZA TANZANIA.
source;gazeti la tanzania daima.
ILA WADAU HIZI KAMPUNI ZA BARABARA ZINAIBA SANA MALIASILI ZA TANZANIA.