PreGE2025 Mchinjita: ACT ni chama kinachokua kwa kasi hapa nchini kuliko chama chochote

PreGE2025 Mchinjita: ACT ni chama kinachokua kwa kasi hapa nchini kuliko chama chochote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, amesema chama hicho kinapiga hatua kubwa kwa kasi isiyopimika, huku akidai kuwa serikali kwa kukosa utashi wa kisiasa wa kukuza demokrasia nchini.

Akizungumza Jumatatu katika maadhimisho ya miaka 11 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dar es Salaam, Mchinjita amesema chama hicho kimeendelea kuimarika licha ya vikwazo vinavyowekwa na serikali.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“ACT ni chama kinachokua kwa kasi hapa nchini kuliko chama chochote. Watu wote wanakubali kwamba kasi ya ACT Wazalendo haina vipimo vinavyojulikana. Kila anayetoka huko anapotoka anaiona ACT ikiamka mahali papya kesho,” amesema Mchinjita.

 
Aaahaaaha nilidhan propaganda zpo ccm tu kumbe kuna tu vyama ni hatari kwa propaganda ccm wakasome
 
huyu jamaa hana mvuto wa kisiasa hata kidogo, ACT watafute mtu mwengine kwenye hiyo nafasi
 
Back
Top Bottom