Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, amesema chama hicho kinapiga hatua kubwa kwa kasi isiyopimika, huku akidai kuwa serikali kwa kukosa utashi wa kisiasa wa kukuza demokrasia nchini.
Akizungumza Jumatatu katika maadhimisho ya miaka 11 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dar es Salaam, Mchinjita amesema chama hicho kimeendelea kuimarika licha ya vikwazo vinavyowekwa na serikali.
“ACT ni chama kinachokua kwa kasi hapa nchini kuliko chama chochote. Watu wote wanakubali kwamba kasi ya ACT Wazalendo haina vipimo vinavyojulikana. Kila anayetoka huko anapotoka anaiona ACT ikiamka mahali papya kesho,” amesema Mchinjita.