KWELI Mchinjita: Mchango wa wakulima kwenye pato la taifa ni 26%, bajeti iliyopangwa 2024/2025 ni shilingi trilioni 49

KWELI Mchinjita: Mchango wa wakulima kwenye pato la taifa ni 26%, bajeti iliyopangwa 2024/2025 ni shilingi trilioni 49

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Mchinjita alikuwa na mkutano wa hadhara mkoani Mtwara ambapo amezungumzia masuala mbalimbali, tazama hapa hotuba yote.

mchinjita.jpg
 
Tunachokijua
Isihaka Mchinjita ni makamu mwenyekiti Bara wa Chama cha Act-Wazalendo ambaye alichaguliwa na mkutano mkuu wa chama hicho kwa kupata kura 517 sawa na asalimia 96.5, machi 6, 2024. Mchinjita alifanya mkutano wa hadhara mkoani Mtwara terehe 5/12/2024 ambapo akiwa huko alizunguzmia mambo mbalimbali na kutoa baadhi ya madai ambayo baada ya uhakiki yamebainika ni ya kweli.

Uhalisia wa madai kuwa mchango wa wakulima kwenye pato la taifa ni 26% mwaka 2023, rejea video hii dakika ya 43.

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa ni kweli mchango wa sekta ya kilimo kwenye pato la taifa ni 26%

Kwa mujibu wa wizara ya mipango na uwekezaji katika ripoti ya hali ya uchumi wa taifa katika mwaka 2023, inaeleza mchango wa Shughuli za Kiuchumi katika Pato la Taifa Mwaka 2023, ambapo shughuli ya kilimo iliongoza kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa wa asilimia 26.5 ikifuatiwa na ujenzi asilimia 13.2, madini asilimia 9.0 na biashara na matengenezo asilimia 8.3
screenshot-2024-12-11-153814-png.3174504


Madai kuwa bajeti iliyopangwa kwa ajili ya mwaka wa fedha 2024/2025 ni shilingi trilioni 49

Mchinjiti katika hotuba hiyo alieleza kuwa bajeti iliyopangwa kwa ajili ya mwaka wa fedha 2024/2025 ni shilingi trilion 49, ambapo trilion 36.4 inatarajiwa kukusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani ambayo ni sawa na asilimia 70 ya bajeti yote. Na fedha iliyobakia ambayo ni sawa na shilingi trilioni 14 inatarajiwa kutokana na mikopo na misaada.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa ni kweli kwa mwaka wa fedha 2024/2025 iliyosomwa bungeni na waziri wa fedha Dkt Mwigulu Lameck Nchemba alieleza kuwa serikali inatarjia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.35 sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/2024.

Bajeti hiyo inaeleza kuwa mapato ya ndani yanakadiriwa kuwa jumla ya shilingi trilioni 34.61 sawa na asilimia 70.1 ya bajeti yote. Aidha mapato mengine yanatarjiwa kupatikana kutokana na misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo ambayo ni sawa na shilingi trilioni 5.13. Na shilingi trilioni. Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 6.62 kutoka soko la ndani
Back
Top Bottom