ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Bwana Isihaka Mchinjita amesema mwaka 2025 ni mwaka kuhakikisha kuwa vijana wa Tanzania hawatalia tena kutokana na ukosefu wa ajira na unyonyaji kazini.
Maneno hayo ameyasema leo Aprili 04, 2025 katika Mjadala wa Kitaifa wa Ajira uliofanyika katika Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni.
"Mwaka huu tunakwenda kuhakikisha kuwa fedha zote zinazoibwa zinasimamiwa na zinarejeshwa kwenye uchumi wa nchi kwa ajili ya miradi ya ajira. Aidha mishahara ya wafanyakazi inaboreshwa, haki za wafanyakazi zinalindwa, na sheria za kazi zinaheshimiwa bila upendeleo," alisema Mchinjita.
Katika hatua nyingine Mchinjita amesema hakuna taifa linaloweza kuendelea bila kushughulikia tatizo la ajira kwa vijana wake. Hakuna taifa linaloweza kustawi kwa kuwaruhusu wawekezaji na matajiri wachache kunyonya jasho la wananchi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Sisi ACT Wazalendo tupo imara kuhakikisha kuwa Tanzania mpya inajengwa—Tanzania yenye ajira kwa kila kijana, mazingira mazuri ya kazi kwa kila mfanyakazi, na uchumi unaonufaisha wananchi wote, siyo wachache.
Vijana wa Tanzania, wakati wenu ni sasa! Hatuwezi kusubiri tena. Mwaka 2025 ni mwaka wa mabadiliko!." Alisisitiza.
Mjadala huo wa Kitaifa wa Ajira uliandaliwa na Chama cha ACT Wazalendo kwa madhumuni ya kuwaleta pamoja Mawaziri Vivuli wa Chama hicho wanaohusika na ajira, wanafunzi wa vyuo vikuu na viongozi Umoja wa Vijana Wasiokuwa na Ajira(UYAM).
Ndugu zangu, Vijana wa Taifa letu! ACT Wazalendo! Taifa Kwanza, Leo na Kesho!
Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa Baraza la Mawaziri Kivuli la ACT Wazalendo kwa kuandaa kongamano hili muhimu ambalo linatupatia fursa ya kujadili moja ya changamoto kubwa kabisa kwa taifa letu—tatizo la ajira, maslahi ya wafanyakazi, na mustakabali wa vijana wa Tanzania. Aidha, napenda kuwashukuru wote mliohudhuria; wawakilishi wa Makundi mbalimbali (Wamachinga, Mamalishe, Madereva) Wanafunzi wa vyuo vikuu, wanaharakati wa haki za kijamii na vijana ambao ni kiini cha mjadala wetu wa leo.
Leo ninasimama mbele yenu kama Waziri Mkuu Kivuli wenu, si tu kama Kiongozi, bali kama mmoja wenu—Mtanzania anayeona masaibu yenu, ndoto zenu, na changamoto zenu. Wengi wenu hamna kazi, wengine mpo katika ajira za hali ya chini zisizo rasmi, au mmekuwa watazamaji wa uchumi ukikua bila kuwapa nafasi. Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana kiko karibu 8.5% miaka ya hivi karibuni, lakini hiki kinasitiri ukweli wa ajira dhaifu, ambapo 80% ya nguvu kazi yetu iko kwenye sekta isiyo rasmi, bila usalama, bila mafao, na bila matumaini ya kesho. Hii si kosa lenu—ni kushindwa kwa serikali ambayo imepuuza uwezo wetu na kusimamia vibaya rasilimali zetu.
TATIZO LA AJIRA NCHINI: CHANZO NA UHALISIA
Katika nchi yenye rasilimali lukuki kama Tanzania, ni aibu na fedheha kuona vijana wakihaha kutafuta ajira bila mafanikio, huku mazingira ya kufanya biashara yakiwa magumu, sekta kubwa ya uchumi ikiwa isiyorasmi, na hali ya wafanyakazi katika viwanda, migodini, na sekta binafsi ikiwa duni. Chanzo cha hali hii ni usimamizi mbovu wa uchumi unaoacha mianya mikubwa ya upotevu wa fedha, sera zisizofungamanisha uzalishaji wa sekta za kilimo na viwanda katika kutengeneza na mfumo wa kifisadi unaohujumu maendeleo ya wananchi masikini.
Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 33.5 ni sehemu ya nguvu kazi ya taifa letu, lakini ni watu milioni 3.5 tu wana ajira rasmi. Asilimia kubwa ya vijana wanajikuta kwenye sekta isiyorasmi, wakifanya kazi za kijungu jiko zisizoweza kuwapa uhakika wa maisha. Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), ajira zisizo rasmi nchini Tanzania zinafikia asilimia 85 ya ajira zote. Hii ina maana kuwa vijana wetu wanajihusisha na shughuli kama vile kilimo, umachinga, mamalishe, uchimbaji, bodaboda, wazoa taka ambao hawana usalama wa kazi zao, hawana bima ya afya, pensheni ya uzee, mafao ya ajali wala mshahara au kipato cha uhakika.
Vile vile, chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM), tumeshuhudia ucheleweshaji wa miradi mikubwa kama mradi wa kusindika gesi asilia wa Lindi ambao ungeweza kusaidia kuongeza ajira, fedha na kupunguza matumizi ya kuagiza bidhaa za mafuta na mbolea hivyo kuongeza uwezo wa Serikali kuajiri. Na miradi ya Mchuchuma na Liganga, ambayo ingeweza kutoa maelfu ya vijana.
Serikali ya CCM imeua Viwanda ambayo vilikuwa na mnyonyoro mkubwa katika si Kutengeneza ajira hata kupunguza matumizi ya taifa kuagiza nje. Unapoagiza nje bidhaa ambao una uwezo wa kuzalishia ndani unapunguza uwezo wa kuajiri na kuongeza utengemezi.
UPOTEVU WA FEDHA NA KUKOSEKANA KWA FURSA ZA AJIRA
Ni wazi kuwa fedha zinazopaswa kutumika kutengeneza ajira na kuboresha maslahi ya wafanyakazi zinapotea kupitia mianya ya kifisadi, biashara haramu ya fedha (illicit financial flows), na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa. Ripoti za mashirika ya kimataifa kama Global Financial Integrity zinaonesha kuwa Tanzania inapoteza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.5 kila mwaka kupitia utoroshaji wa fedha haramu nje ya nchi. Hii ni zaidi ya Shilingi trilioni 3.9, fedha ambazo zingetosha kuanzisha viwanda vingi, kuboresha miundombinu ya kilimo na uvuvi, na kuzalisha ajira kwa vijana wa Kitanzania.
Serikali ya CCM inashindwa kudhibiti mianya hii ya upotevu wa fedha kwa sababu inahifadhi mfumo wa kifisadi unaowanufaisha wachache. Matokeo yake ni kuwa badala ya kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji wenye tija kwa vijana, serikali inaendelea kukopa kwa masharti magumu, huku pesa zinazokusanywa zikiishia kwenye matumizi yasiyo na faida kwa wananchi wa kawaida.
Ubadhirifu wa fedha za umma. Tumeshuhudia watu wachache wakiendelea kutafuna fedha za umma bila kuchukuliwa hatua, Ripoti ya CAG kwa mwaka 2022/23 imebaini ubadhirifu wa Shilingi trilioni 3.2. Fedha hizi zingetumika kwa njia mbadala zingeweza kugharamia ajira za walimu 130,000 kwa mwaka mmoja au kuimarisha huduma za maji safi kwa zaidi ya kaya milioni 5 nchini.
PROPAGANDA ZA SERIKALI KUHUSU AJIRA
Badala ya kutatua tatizo, mara kadhaa serikali imekuwa ikitumia propaganda kukwepa wajibu wake kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini; Tunaisikia serikali ikitamka kuwa suala la kuajiri ni la sekta binafsi na kwamba jukumu lake ni kuboresha mazingira ya biashara tu. Hii ni mbinu ya kilaghai ya kukwepa wajibu wa kikatiba wa kuhakikisha ustawi wa wananchi. Hii ni kanuni ya nyikani, utawala wa wanyama sio serikali inayoongozwa na watu wenye utu na maarifa ambao watakataa nchi yao kugeuzwa maabara ya majaribio ya sera ambazo hazina mwelekeo wa kuzalisha ajira zenye tija kwa vijana wake.
Propaganda nyingine hatari ni zile zinazolenga kuwabebesha vijana lawama za kutokuwa na ajira kwa kuwataja kama wavivu, wasio wajasiriamali, au wasiokuwa na ujuzi wa kutosha. Mbinu hii ya kihadaa ina lengo la kuhamisha wajibu kutoka kwa serikali kwenda kwa wahanga wa mfumo wa kiuchumi usio na mwelekeo wa kutoa ajira. Ukweli ni kwamba kila mwaka vyuo vikuu, taasisi za kati na vyuo vya ufundi huzalisha maelfu ya wahitimu waliobobea katika taaluma mbalimbali, lakini soko la ajira halina nafasi kwao.
Kwa upande mwingine, kutangaza “ajira za muda” au “ajira zisizo rasmi” kama suluhisho. Ukweli ni kwamba ajira hizi hazina hakika, uendelevu wala hifadhi ya jamii. Huu ni ujanja wa kisiasa unaolenga kudhibiti shinikizo la kijamii pasipo kushughulikia mzizi wa tatizo.
Pia, wito wa vijana kwenye Kilimo; Serikali inawahimiza vijana waingie kwenye kilimo kama suluhisho, bila kuwekeza ipasavyo katika miundombinu, masoko na sera zinazowafanya vijana wapende kilimo.
Vile vile, tatizo hili si la nchi yetu pekee– Serikali inajenga hoja ya kulinganisha hali ya ajira na nchi nyingine ili kupunguza lawama na kuonyesha kuwa siyo tatizo lake peke yake.
MASLAHI DUNI YA WAFANYAKAZI NA UNYONYAJI KWENYE SEKTA BINAFSI
Tukiwa tunaelekea mwaka 2025, ni lazima tuzungumze kwa ujasiri kuhusu hali mbaya ya wafanyakazi katika sekta binafsi, viwandani, migodini, na sekta nyingine muhimu. Kiwango cha mishahara kipo chini ya kiwango cha maisha, hali ya mazingira ya kazi ni duni, na sheria za kazi hazitekelezwi ipasavyo. Katika migodi mingi nchini, wafanyakazi wanateseka kwa mishahara midogo huku kampuni kubwa za kimataifa zikivuna mabilioni kutoka kwenye rasilimali zetu.
Mifano ni mingi: wafanyakazi wa viwandani wakifanya kazi kwa zaidi ya saa 12 kwa malipo ya chini ya Shilingi 200,000 kwa mwezi, wachimbaji wadogo wakidhulumiwa na makampuni makubwa bila msaada wowote wa serikali, na wafanyakazi wa majumbani wakifanyishwa kazi katika mazingira ya kinyama. Huu ni mfumo wa unyonyaji ambao ACT Wazalendo inasimama imara kuupinga!
MPANGO WA ACT WAZALENDO KWA VIJANA
Lakini mabadiliko yanawezekana, na ACT Wazalendo iko hapa kuyaleta! Sisi ni chama cha “Taifa la Wote, Maslahi ya Wote”—na tuna jibu la kitendawili cha uchumi unaokua lakini hauzalishi ajira wala kuondoa umaskini.
Mwaka 2025 ni mwaka wa kupigania ajira kama kipaumbele cha juu kabisa, kwa sababu sisi tu ndio tunaweza kuleta suluhisho la kweli kwa vijana.
Maono yetu ni “Taifa la Wote, Maslahi ya Wote”—taifa linalowajumuisha wote, kwa maslahi ya wote—na tutaunda uchumi unaowafanyia kazi nyinyi.
Kwanza, tutakipa kipaumbele kilimo ili kuwapa kazi. Tutapigania msamaha wa mikopo kwa wahitimu wa ugani wa kilimo wanaofanya kazi vijijini, ili kuongeza uzalishaji. Tutaendelea kudai kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha mbolea haraka, kupunguza gharama za pembejeo na kutoa kazi za viwandani za kudumu. Tutapigania kupandishwa kwa bajeti ya kilimo hadi 10%, kuhakikisha mnapata vifaa vya kilimo ili kilimo kiwe kazi ya maisha, si ya kujikimu tu.
Pili, ni mwaka wa kupinga unyonyaji wa wakulima ili kuimarisha mnyororo wa kilimo—kuhakikisha bidhaa za kilimo kama vile matunda, viazi na mboga za majani zinachakatwa nchini Kutengeneza kazi za viwandani.
Tatu, tutaharakisha miradi mikubwa kama kiwanda cha gesi asilia na madini, kuunda kazi za ujenzi na uendeshaji, pamoja na kazi za ziada za mnyororo wa thamani. Hii itaimarisha uchumi na kuwapa nafasi katika nishati na madini.
Lakini hatutasimama hapo. Tutawekeza katika umeme vijijini, barabara, na bandari kuunda kazi za ujenzi na kuunganisha vijana na masoko. Tutapunguza taratibu ngumu za biashara, kuondoa ada zisizo rasmi, ili muanze Biashara rasmi bila vizuizi. Na tutawapa elimu na mafunzo ya ufundi ili muwe na ujuzi wa kazi hizi mpya.
CCM wamewashika vibaya wakulima wetu, wamepuuza vijana wetu, na wamechukua rasilimali zetu kwa manufaa yao binafsi, wakiacha vijana bila ajira wala maendeleo ya kweli. Lakini sisi, ACT Wazalendo, tuna jibu la kitendawili hicho—tutawakomboa wakulima, tutawapa nguvu vijana, na tutajenga uchumi wa wote, si wa wachache tu. Ajira itakuwa ajenda tunayoipigania kila uchao. Hii ni vita dhidi ya ukosefu wa ajira na vita kwa ajili ya mustakabali wa vijana wa Tanzania
MSIMAMO WA ACT WAZALENDO NA WITO KWA WATANZANIA
ACT Wazalendo mwaka 2025, ni lazima tuhakikishe kuwa vijana wa Tanzania hawatalia tena kutokana na ukosefu wa ajira na unyonyaji kazini. Tutapambana kwa dhati kuhakikisha kwamba:
Vijana wa Tanzania, wakati wenu ni sasa! Hatuwezi kusubiri tena. Mwaka 2025 ni mwaka wa mabadiliko!
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza! Viva Vijana viva!
#AjiraNiSasa, #SasaNiAjira
Asanteni.

=================================
HOTUBA KAMILI...Ndugu zangu, Vijana wa Taifa letu! ACT Wazalendo! Taifa Kwanza, Leo na Kesho!

- Fedha zote zinazoibwa zinasimamiwa na kurejeshwa kwenye uchumi wa nchi kwa ajili ya miradi ya ajira.
- Mishahara ya wafanyakazi inaboreshwa, haki za wafanyakazi zinalindwa, na sheria za kazi zinaheshimiwa bila upendeleo.
- Makampuni yote ya kimataifa yanayowekeza nchini yanahitajika kuajiri asilimia kubwa ya Watanzania kwa ajira rasmi zenye mikataba na hifadhi ya jamii
- Tutaimarisha mfumo wa uwezeshaji wa biashara kwa vijana na kuwahakikishia mazingira mazuri ya kiuchumi ili waweze kujiajiri kwa tija.