PreGE2025 Mchinjita: Tunataka mabadiliko, Kassim Majaliwa usituhadae!

PreGE2025 Mchinjita: Tunataka mabadiliko, Kassim Majaliwa usituhadae!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Bwana Isihaka Mchinjita ameshangazwa na kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyoitoa bungeni kuwa hali ya demokrasia nchini imeimarika.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Aprili 10, 2025, Mchinjita amesema hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni ilitarajiwa kutoa uelekeo utakaoleta mwafaka wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi. Walakini hotuba imegeuka kuwa mwiba mkali kwa wadau wa uchaguzi kwani hakuna mwelekeo wowote wa mabadiliko wala utekelezaji wa sheria za uchaguzi.

Jana Aprili 09, 2025 Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha hotuba yake ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 amesema demokrasia nchini imekua na kuimarika katika utawala wa Awamu ya Sita.

Aidha Bwana Mchinjita amesema Serikali haina mpango wa mabadiliko yoyote kuelekea uchaguzi mkuu 2025; na kwamba hicho kinachoitwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni jina lisilobeba mabadiliko yoyote ya msingi ambayo wadau demokrasia wamekuwa wakiyapigania.

“Hata hivyo Waziri Mkuu anaeleza tu suala la kubadilishwa jina kwa iliyokua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) lakini haelezi chochote juu ya mwenendo wa kisheria wa tume hiyo.” Alisema Mchinita

Katika hotuba ya Mchinjita; ambayo mwenyewe anasema ni mbadala wa ileliyotoa Waziri Mkuu Bungeni, inasisitiza mambo sita ambayo ACT Wazalendo inayapigania kwa nguvu kubwa; mambo hayo ni ni yafuatayo:

1. Makamishna wa Tumehuru ya taifa ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindane
2. Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo
3. Mawakala wa vyama vya siasa wafanyekazi zao bila bughudha na wasizuiwe
4. Wagombea wasienguliwe
5. Pasiwe na kura feki
6. Vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie mchakato wa uchaguzi
 
Demokrasia gani ya uongo na kuhadaa wananchi?!
 
Back
Top Bottom