Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Yaah ilikuwa hivyo.Halafu kuna ile Tulikuwa maskani maskanii famagusta .
Mwendelezo umenitoka kidogo hapo mtu akikumbuka ashushe mistari hiyo
tulikuwa maskaani
maskani famagusta
kukaa kidogo kaja mtu
kaja anatuuliza
Kipaka kafa saa ngapi?
watu wote tukashangaa
tulikuwa hatuna habari
kwenda kuuliza kumbe kweli
Alihamdulillah


sio yeye peke yake
safari hii yetu sotee
yeye ametangulia
hata bwana Nanga na wewe utakwenda tu
sio yeye peke yake
yeye ametangulia
hata bwana Gusa utakwenda tu
........................
 
Mule mule swahiba yangu nimekumbuka mbali kiasi ya muongo mmoja na nusu.
 
Daaah, Mkuu utakuwa mkongwe mwenzangu!
Acha kabisa, jamaa alikiwa na mkwara sio mchezo, alikuwa na pingu kiunoni, bastola, Rungu na kifimbo cha polisi
 
Acha kabisa, jamaa alikiwa na mkwara sio mchezo, alikuwa na pingu kiunoni, bastola, Rungu na kifimbo cha polisi
Na sarakasi juu! Nilikuwa namuona TAIFA, siku za mechi. Atakuwa kastaafu.
 
Kumbe kicheko ni wa kitambo kwenye game ta muziki wa kitaaa.
 
Ah nalialia mama, nakulilia mama we,
Uko wapi mama, napata tabu mama we, sikuoni mama nakutafuta mama we
Hawa jamaa walikuwa wanaimba, kama kuna link ya kupata nyimbo za gali kubwa, 7 survivor, atomic nk aiweke hapa
 
Ah nalialia mama, nakulilia mama we,
Uko wapi mama, napata tabu mama we, sikuoni mama nakutafuta mama we
Hawa jamaa walikuwa wanaimba, kama kuna link ya kupata nyimbo za gali kubwa, 7 survivor, atomic nk aiweke hapa
7 survivor na jagwa ndo zinapatikana mtandaoni za gari kubwa hata hazionekani labda utafute wakongwe wanaweza kuwa nayo,
 
We jamaa ni noma sana.
 
Jamani hakuna mwenye kutoa msaada jinsi ya kuzipata nyimbo za mchiriku albam GARI KUBWA?
 
Kumbe kicheko ni wa kitambo kwenye game ta muziki wa kitaaa.
Naomba nikuweke sawa kaka mkubwa. Huyu KICHEKO w E-fm ambae kwa sasa yupo clauds, sio kicheko wa gari kubwa (HISANI). Wakati hisani wanapiga nyimbo zao enzi hizo kicheko huyu wa genge la singeli alikuwa mtoto mdogo sana. Wale hisani walikuwa wanapatikana mwananyamala wakati kicheko na dogo mfaume wote watoto wa temeke. Kicheko kazaliwa mikoroshini temeke. Hakuwahi kuimba mnanda. Hisani walikuwa dizain kama ya watu wazima kipindi hicho sasa angalia Age ya kicheko sasa hv ni viwili tofauti. Wakati jamaa wanatamba hata huyu marehemu omary omary, Allah amrehemu alikuwa bado mdogo vile vile. Wakati kicheko na omary omary bado ommy ni mkubwa. Hisani walishakuja maeneo ya tandika bandari enzi hizo parifurika watu ikawa historia, katika harakati za kuburudisha likatokea timbwili si unajua tena masela , ilikuwa balaa show ikafa watu walipotea na raia kama wawili walidedi. Hao waliodedi walikuwa masela waliochukuliana demu maana hiyo piga yake balaaa sijui silaha walizipigilia viunoni! Braza wangu alirudi hom na kandambili moja.
 
Hapana mkuu bado sijazipats
Nyimbo za hisani mtandaoni hakuna. Only cassette. Hata me nilikuwa nayo ila nilipata kumuazima rafiki yangu nae akanogewa akaja akampa mtu basi kadhulumiwa ikapotea. Ningeweza hata ku record nikatupia humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…