Dah...kumbe walianza mwaka 1981 na Ali Hassan Mwinyi umeimbwa 1986
Kwenye hiyo interview waliyofanyiwa wasanii wa band ya Hisani Gari kubwa,kuna makosa mengi ya utunzaji wa kumbukumbu yamefanyika (Director wa interview ni Muddy Mwanaharakati).
Huo wimbo wa #Ally Mwinyi ulifyatuliwa kwenye albam no.1 (Vol.1) ya Hisani Gari kubwa iliyotoka mwaka 94.Na hata hivyo kwa kumbukumbu zilizo sahihi kabisa,hao Hisani Gari kubwa wimbo huo si wao bali ni mali ya band ya Night Star ya akina Haidary Kessy na Halfan Wamizoga chini ya umiliki wa Afande Mkama Sharp.
Historia sahihi ya mziki wa Mchiriku (mnanda)iko hivi:
Band ya kwanza kabisa iliyoanza kuingia studio na kufyatua albam ilikuwa ni band ya Dar Nyota ya akina Seleman Msasa mnamo mwaka 93.
Kwa wakati huo kulikuwa na band kubwa kuliko hii kama vile Night Star,Red Star, Zipolari,na zingine pia zilizokuwa zinapiga Mchiriku (mnanda) kwa kuchanganya na Magita.Tena zilikuwa maarufu kuliko Dar Nyota na hata hao Hisani Gari kubwa walikuwa bado kutambulika kwenye ramani ya mchiriku ipasavyo.
Dar Nyota wakiwa katika makumu yao (Band ya CCM mkoa wa Dar es Salaam) walipata mwaliko Dodoma kwenye shuguli za mambo ya chama,walipokuwa huko wakapata bahati ya kuingia studio ili kufyatua albam (RTD Dodoma),ndio wakatumia nafasi hiyo kufyatua albam ya kwanza ya miondoko ya Mchiriku mnamo mwaka 93 na kuiingiza sokoni.
Baada ya hapo band zingine nazo zikaanza kupata muamko wa kufyatua albam na hatimaye Mchiriku ukaanza kuwa maarufu.
Hisani Gari kubwa wao waliingia studio na kufyatua albam yao ya kwanza mwaka 94,na kwakuwa nyakati hizo hapakuwa na sheria za hati miliki (Copy Right) Hisani waliiba nyimbo nyingi za Night Star na kuzirecord.
Sasa basi,kilichowafanya Hisani Gari kubwa kukubalika kwa haraka na tapes zao (kanda) kuuza sana sokoni,ni kwa sababu wao wiliibuka na midundo tofauti kidogo na zile zilizokuwa zinajiita band kubwa kama vile Night Star ya Kariakoo na Zipolari ya Mtoni Kichangani kwa kuondoa mfumo wa magitaa na kupiga miondoko ya kisela na ya kuchezeka.
Kuanzia hapo ikawa ni mfululizo wa kuanzishwa band na kuingia studio chini ya makampuni ya usambazaji ya kihindi kama vile FK Mitha,Mamu Store na Mwananchi Store.Na hatimaye mziki unapata umaarufu na kushika kasi jijini Dar es Salaam na viunga vyake.
Kwahiyo kwa ujumla band ya Hisani Gari kubwa itabaki kuwa ni miongoni mwa band kongwe tu za mziki wa mchiriku nchini Tanzania lakini katu sio waasisi [emoji125][emoji125][emoji125]