Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Malumbano na zogo kubwa Katika Basi lile,
Kati ya kondakta na Bwana mgambo yule,
Kondakta anadai nauli yake hee,
Na mgambo anataka kupanda bure anadai Yeye ni chombo cha dola,
Kondakta akaja juu akasema haiwezekani kupanda bure hee,
Nimeruhusiwa na jeshi la magereza,
Nimeruhusiwa na jeshi la polisi,
Kupanda buree nmeruhusiwa na chombo cha dola.
×2
 
Hii nyimbo unayo ??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ubeti wa pili: "Tulikuwa Maskini...." Huyo ni OMARI OMARI!
 
Sidhani kama hiyo Tulikuwa maskani ni Hisani hao, nadhani ni Omary Omary akiwa na Topaz, unaikumbuka night star ya Mkapa Sharp? Wakiwa na kina wamizoga
Yap Topaz chini ya Omary Omary ilisumbua sana na maskani yao yalikuwa pale Temeke Mwembe Yanga kijiwe chao Famagusta,bila kusahau Jagwa na miaka ya 2000 walipokuja Seven Survival chini ya ya Uongozi wake Jenerali Juma Mpogo a.k.a Lupozi na vibao vyao kama Usije Mjini, Baba wa Taifa, Mabomu Gongolamboto, Loliondo na Majanga Og na remix waliyomshirikisha Juma Nature.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo atomic na huyo marehem Omar omar.Nakumbuka marehem alianzia Topaz ngoma kabla ya kuunda Atomic
Omary Omary kilichokuwa kinamsaidia ni Dingi wake alikuwa na uwezo somehow miaka ile so alikuwa anampa support sana ya vifaa na fedha. Imagine mwaka 1990 karibu kata mbili mpaka tatu Temeke kulikuwa hakuna mwenye TV ni kwake tuu world cup ya 90 na 94 tulikuwa tunaangalia kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaah ilikuwa hivyo.Halafu kuna ile Tulikuwa maskani maskanii famagusta .
Mwendelezo umenitoka kidogo hapo mtu akikumbuka ashushe mistari hiyo
Hiki kisa ni cha kweli kabisa. Said Kipaka alikuwa mwizi wa hatari na anaogopeka kishenzi Temeke yote mpaka Buguruni. Alikuwa anaishi pale Temeke Sokota. Kuna siku alienda kuiba maeneo yale Wananchi wakala nae Kona kufika pale Sokota avuke barabara kuelekea upande wa shell akagongwa na Gari,alipogongwa tuu Wananchi wakammaliza Kwa Moto. Hata alipokufa yeye wakabaki wengine kwenye familia yao kuendeleza wizi,Kabwe akashika usukani. Dah longtime sana yale maisha ya uswazi plus mchiruku yalikuwa so excited aiseee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaah ilikuwa hivyo.Halafu kuna ile Tulikuwa maskani maskanii famagusta .
Mwendelezo umenitoka kidogo hapo mtu akikumbuka ashushe mistari hiyo
Hapo Famagusta Mwembe Yanga ndio kulikuwa Makao Makuu ya wezi na majambazi wote wa Temeke na Dar kiujumla. Wajinga walichimba mpaka handani la kuficha mali za wizi na pia ilikuwa ndio kama safehouse yao. Hali ilpokuwa tete Serikali ikaingilia kati ikavunja kila kitu na kugeuza lile eneo kuwa dampo jamaa ndipo wakahama kabisa wakasogea Mji mpya enzi hizo Mtoni Mtongani mpaka Mbagala Saba Saba ndio ikazaliwa Seven Survival chini yake Jenerali Juma Mpogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika watu waliokuwa hatari wanaoweza kulaza Mtaa mzima saa6 ya mchana ni huyo Nanga Boy Simela na wenzake wakina Chichi Baunsa. Dah tumekulia katika mazingira hatarishi sana kwa malezi ya kitaa,tunashukuru sana Mungu kutuepusha na vishawishi na mabaya yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jagwa- mama ashurá hii ngoma hatari sana mchiriku niliona wanaiperform germany
 
Wasela na wahuni wote wamemalizwa na unga waliobaki sasa hivi wanatumia (methodyn?) na kuokota makopo majalalani.
 
I hope someone angetengeneza documentary ya historia ya muziki wa mchiriku
 
Kama Tajiri ni mtu
Na masikini ni mtu
Kama Tajiri ana macho
Na masikini ana machoo
Hakuna sababu ya kunyanyasana
Sababu ya pesaa zako
Kama pesa ni zako
Na umaskini ni wangu
Amenipa Mungu Eehh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…